NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID
WANAHISA zaidi ya 400 wa Mwalimu Commercial Bank
Plc (MCB) wamekutana mjini Mtwara katika mkutano wa mwaka (AGM) na kupokea taarifa ya kiutendaji ya benki hiyo kwa mwaka 2018.
Plc (MCB) wamekutana mjini Mtwara katika mkutano wa mwaka (AGM) na kupokea taarifa ya kiutendaji ya benki hiyo kwa mwaka 2018.
Afisa
Mtendaji Mkuu (CEO) wa benki hiyo, Bw.Richard L. Makungwa amesema
Mkutano huo wa tatu ni wa kawaida ambao lengo lake ni kuwapa taarifa ya
kiutendaji ya benki ambapo wanahisa wataijadili na kuweka maazimio
mbalimbali ya kiutekelezaji kwa wakati ujao.
“Sisi
kama taasisi ya kifedha, kila mwaka huwa tunafanya mkutano wa wanahisa
ili kuwaeleza hali ya benki yao, Shughuli zilizofanyika kwa mwaka mzima,
mafanikio yaliyopatikana, changamoto na matarajio ya baadaye, lakini
pia kupokea maoni
kutoka kwa wanahisa wetu ambao pia ni wateja wetu wanayo nafasi kubwa sana ya kutoa maoni yao kwa nia ya kuboresha uendeshaji wa benki.” Alifafania Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo Bw. Makungwa.
kutoka kwa wanahisa wetu ambao pia ni wateja wetu wanayo nafasi kubwa sana ya kutoa maoni yao kwa nia ya kuboresha uendeshaji wa benki.” Alifafania Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo Bw. Makungwa.
Alisema wengi wa Wanahisa wa Mwalimu Commercial Bank Plc
ni walimu lakini pia wako wanahisa ambao sio walimu, kuna mashirika na
taasisi nyingine kwani benki hii ipo kuhudumia Watanzania wote.
Mwalimu Commercial Bank Plc kama zilivyo benki nyingine za biashara inafanya shughuli zote za kibenki ikiwa ni pamoja na kutoa mikopo kwa wateja wake.
“Benki
yetu inatoa mikopo ya binafsi, mikopo ya biashara zikiwemo biashara
ndogo ndogo na kwakweli tumekuwa na mafanikio makubwa, wateja wetu ni
waaminifu wanarejesha
mikopo waliyopewa pamoja na changamoto za hapa na pale lakini bado tunafanya vizuri katika eneo hilo.” Aibainisha.
mikopo waliyopewa pamoja na changamoto za hapa na pale lakini bado tunafanya vizuri katika eneo hilo.” Aibainisha.
Alisema
licha ya benki kutumia mifumo yake ya kawaida katika kutoa huduma
lakini pia inakusudia kuendeshwa kidigitali ili mteja popote alipo aweze
kufanya miamala bila shida yoyote na hivi karibuni benki itajiunga na
mtandao wa VISA ambao utawawezesha wateja wetu kupata huduma za kibenki
mahala popote walipo.
“Benki inaendelea kuboresha huduma zake, wanahisa na wateja wetu wategemee
kuwa benki yao inaendelea kuboresha huduma zake na kuimarika walimu
wetu ambao ndio wateja wetu wakubwa wako nchi nzima na tunajitahidi
kuhakikisha huduma zetu zinawafikia kwa urasihi.” Alifafanua.
Alitoa hakikisho kuwa Mwalimu Commercial Bank Plc iko katika hali nzuri na mtaji wake uko vizuri na unakidhi matakwa ya msimamizi wa mabenki yaani BoT.” Alisema.
Akifungua Mkutano huo Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Mwalimu Commercial Bank Plc,
Bw. Herman Kessy alisema, benki imepata leseni ya uwakala wa bima na
hivyo itawaomba wadau Chama cha Walimu (CWT), Mfuko wa Pensehni kwa
Watumishi wa Umma (PSSSF) na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF)
kutumia huduma hiyo kwa faida ya benki na wanahisa wote.
Pia
Bw. Kessy alisema katika mafanikio ya benki kwa mwaka 2018 ni pamoja na
kuongeza tawi la pili pale Mlimani city, lakini kufungua ofisi kwa
ajili ya kutoa huduma kwenye mikoa ya Morogoro na Mwanza na Mbeya.
Awali
wajumbe wa mkutano huo walipatiwa semina iliyoendeshwa na Meneja wa
Huduma za kidijitali Bw. John Mhina iliyolenga kuwaelimisha nidhamu ya
matumizi ya fedha
na umuhimu wa kuweka akiba.
na umuhimu wa kuweka akiba.
Wajumbe
pia walipata elimu kuhusu soko la hisa umuhimu wa walimu kununua hati
fungani ambapo Mkuu wa Uendeshaji na Fedha wa kampuni ya Core Security Limited
ambayo ni wakala wa soko la hisa la Dar es Salaam,Bi. Mary Kessy
alifafanua kuhusu namna ambavyo mtu anaweza kununua hati fungani.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Mwalimu Commercial Bank Plc,
Bw. Herman Kessy, (kuli), akizungumza wakati wa Mkutanio Mkuu wa tatu
wa Mwaka wa Wanahisa wa benki hiyo kwenye ukumbi wa BoT mkoani Mtwara
leo Agosti 22, 2019. Wengine kiutoka kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa
Benki hiyo, Bw. Richard Makungwa, na Mjumbe wa Bodi Bw. Said Kambi.
Bw. Kessy akihutubia wajumbe.
Afisa
Mtendaji Mkuu (CEO) wa benki hiyo, Bw.Richard L. Makungwa, akizungumza kwenye mkutano huo.
Mtendaji Mkuu (CEO) wa benki hiyo, Bw.Richard L. Makungwa, akizungumza kwenye mkutano huo.
Baadhi ya Wanahisa wakifuatilia hotuba za viongozi.
Wanahisa wakipitia taarifa mbalimbali kuhusu utendaji wa benki hiyo kwa mwaka 2018.
Baadhi ya Wanahisa wakifuatilia hotuba za viongozi.
Mwanahisa akipitia taarifa hiyo ya utendaji wa benki hiyo kwa mwaka 2018.
Baadhi ya wajumbe wa bodi wakiwa pamoja na wanahisa wa benki hiyo wakifuatilia hotuba mbalimbali za viongozi.
Wajumbe wa bodi Profesa Tadeo Satta (kulia) na Bw.Framncis Ramadhani wakizungumza jambo.
Mwanasheria wa benki akitoa ufafanuazi wa masuala mbalimbali yahusuyo mkutano huo.
Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Bw. Deus Seif (aliyesimama), akizunguzma kwenye mkutano huo.
Wageni waalikwa kutoka Benki Kuu ya Tanzania nao walikuwepo.
Afisa Mtendaji Mkuu Mwalimu Commercial Bank Plc, Bw. Richard Makungwa (kulia), akizungumza jambo na Mkuu wa Rasilimali wa tu wa benki hiyo, Bi. Ellijalia Mabiki. |
Bw.Makungwa (kushoto), akizungumza jambo na Mkuu wa Fedha wa MCB, Bw. Selemani Kijori wakati wa mkutano huo.
Wajumbe wakipatiwa makabrasha yenye maelezo na ripoti ya mwaka ya benki hiyo.
Picha ya pamoja wajumbe wa bodi na baadhi ya viongozi wa chama cha walimu CWT.
0 comments:
Post a Comment