Naibu Waziri ,Ofisi ya Waziri Mkuu
,anayeshughulikia masuala ya watu wenye Ulemavu Mhe.Stella Ikupa
akiwasili katika ukumbi wa CCM Mkoa Dodoma kwa ajili ya kufungua Kikao
cha Baraza Kuu la wanawake Tanzania (UWT) kwa Mkoa wa Dodoma
Naibu Waziri ,Ofisi ya Waziri Mkuu
,anayeshughulikia masuala ya watu wenye Ulemavu Mhe.Stella Ikupa
akisalimiana na Mjumbe wa Baraza Kuu Taifa UWT,Bi.Chiku Mugo alipowasili
katika ukumbi wa CCM Mkoa Dodoma kwa ajili ya kufungua Kikao cha Baraza
Kuu la wanawake Tanzania (UWT) kwa Mkoa wa Dodoma
Naibu Waziri ,Ofisi ya Waziri Mkuu
,anayeshughulikia masuala ya watu wenye Ulemavu Mhe.Stella Ikupa
akisalimiana na Mbunge wa viti maalum Mariam Ditopile alipowasili katika
ukumbi wa CCM Mkoa Dodoma kwa ajili ya kufungua Kikao cha Baraza Kuu la
wanawake Tanzania (UWT) kwa Mkoa wa Dodoma
Naibu Waziri ,Ofisi ya Waziri Mkuu
,anayeshughulikia masuala ya watu wenye Ulemavu Mhe.Stella
Ikupa,akibadilishana mawazo na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake
Tanzania(UWT) Jesca Mbogo wakati wa kufungua Kikao cha Baraza Kuu la
wanawake Tanzania (UWT) kwa Mkoa wa Dodoma.
Sehemu ya wajumbe wakifatilia kikao cha baraza Kuu la UWT mkoa wa Dodoma
Naibu Waziri ,Ofisi ya Waziri Mkuu
,anayeshughulikia masuala ya watu wenye Ulemavu Mhe.Stella Ikupa,akiwa
pamoja na wajumbe wakipitia taarifa wakati wa kufungua Kikao cha Baraza
Kuu la wanawake Tanzania (UWT) kwa Mkoa wa Dodoma.
Naibu Waziri ,Ofisi ya Waziri Mkuu
,anayeshughulikia masuala ya watu wenye Ulemavu Mhe.Stella
Ikupa,akizungumza na wajumbe wakati wa kufungua Kikao cha Baraza Kuu
la wanawake Tanzania (UWT) kwa Mkoa wa Dodoma upande wa kushoto ni
Mwenyekiti wa UWT mkoa Neema Majule.
……………………
Na.Alex Sonna,Dodoma
Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri
mkuu,anayeshughulikia masuala ya watu wenye Ulemavu Mhe.Stella Ikupa
amesema watu wanaombeza na kupinga jitihada kubwa zinazofanywa na Rais
Dkt.John Magufuli watakuwa wanapingana na Mungu Mwenyewe.
Mhe.Ikupa amesema hayo jijini
Dodoma wakati akifunga kikao cha Baraza kuu la Umoja wa Wanawake
Tanzania [UWT]Kwa mkoa wa Dodoma.
Mhe.Ikupa amesema mambo Mengi
yaliyokuwa kwenye ilani ya Uchaguzi mkuu mwaka 2015 kwa Chama Cha
Mapinduzi yametekelezwa na kubainisha kuwa mtu ambaye hajaguswa na
jitihada za Rais Magufuli atakuwa Muongo.
Aidha,Ikupa ametaja Nyanja ambazo
Serikali ya awamu ya Tano imetekeleza ikiwa ni pamoja na kupambana na
Dawa za kulevya ambazo zilikuwa zikipoteza vijana na kurudisha nyuma
uchumi wa nchi,Uimarishaji wa Miundombinu ni pamoja na
Umeme,Barabara,Reli na Usafiri wa anga pamoja na uwezeshaji wa Mikopo
kwa makundi maalum ikiwa ni pamoja na vijana,wanawake na watu wenye
ulemavu.
Hata hivyo ,Naibu Waziri huyo
amechangia Jumla ya mabati 10 yenye thamani ya Tsh.360,000 Kwa UWT
Dodoma kwa ajili ya utekelezaji wa Mradi wa Elimu huku jumla ya
Tsh.milioni moja ,laki nane na hamsini elfu zikichangiwa kwenye harambee
ya baraza hilo.
Awali akizungumza katika kikao
hicho,mwenyekiti wa UWT mkoa Neema Majule amesema tangu wanaingia
madarakani waliahidi mambo matatu ikiwemo kujenga UWT yenye upendo,umoja
na mshikamano na kupitia mikutano mbalimbali tuliyoifanya hilo
wamefanikiwa.
“Kwa sasa tumebaini na
kushughulikia upatikanaji wa viwanja vya uwekezaji,na hili tumelifanya
kila wilaya nia yetu tujitegemee na tusiwe tegemezi,”alisema mwenyekiti
huyo.
Kwa upande wake mjumbe wa Baraza
kuu Taifa UWT,Chiku Mugo amempongeza Naibu Waziri Ikupa Kwa Mchango huo
huku akiwapongeza wadau wengine kwa kuendelea kuiunga UWT Katika
kufanikisha miradi mbalimbali ya
Maendeleo.
0 comments:
Post a Comment