MKURUGENZI wa Maendeleo ya jamii kutoka
Wizara ya Afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto, Patrick
Golwike,akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha ya tathimini khusu ndoa
za utotoni iliyoitishwa na Shirika la Save the Children iliyofanyika
jijini Dodoma.
Mkurugenzi kutoka Save the Children Makao
Makuu Dar es Salaam Bi.Angela Makota akitoa taarifa wakati wa ufunguzi
wa warsha ya tathimini khusu ndoa za utotoni iliyoitishwa na Shirika la
Save the Children iliyofanyika jijini Dodoma.
Mkurugenzi Idara ya Watoto wizara ya Afya
Sebastian Kitiku,akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha ya tathimini
khusu ndoa za utotoni iliyoitishwa na Shirika la Save the Children
iliyofanyika jijini Dodoma.
Mratibu wa ufuatiliaji wa Shirika la Save
the Children, Kanuty Munishi,akiongea na waandishi wa habari (hawapo
pichani)wakati wa ufunguzi wa warsha ya tathimini khusu ndoa za utotoni
iliyoitishwa na Shirika la Save the Children iliyofanyika jijini Dodoma.
Sehemu ya wadau wakifatilia wakati wa
ufunguzi wa warsha ya tathimini khusu ndoa za utotoni iliyoitishwa na
Shirika la Save the Children iliyofanyika jijini Dodoma.
MKURUGENZI wa Maendeleo ya jamii kutoka
Wizara ya Afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto, Patrick
Golwike,akiwa katika picha ya pamoja na viongozi kutoka Shirika la Save
the Children na wadau mara baada ya kufungua warsha ya tathimini khusu
ndoa za utotoni iliyoitishwa na Shirika la Save the Children
iliyofanyika jijini Dodoma.
…………………….
Na.Alex Mathias,Dodoma
MKURUGENZI wa maendeleo ya jamii kutoka
Wizara ya Afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto, Patrick
Golwike, ametaja miongoni mwa vitu vinavyosababisha watoto wa kike
kuolea katika umri mdogo kwamba ni uelewa mdogo kuhusu watoto wa kike
kuwa wana soko hivyo hutolewa ng’ombe wengi, kukubali kutaliwa na waume
zao na umasikini wa kipato.
Hayo ameyabainisha leo ijini Dodoma,
alipokuwa anamuwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara hiyo kitengo cha
maendeleo ya jamii, John Jingu, wakati wa ufunguzi wa warsha ya
tathimini kuhusu ndoa za utoto iliyoitishwa na Shirika la Save the
Children ambapo amesema mabinti wadogo hutolewa ng’ombe kati ya 25 hadi
50 kiwango ambacho hakifikii kwa mwanamke mtu mzima.
BW.Golwike amesema pamoja na juhudi kubwa
za serikali katika vita hiyo, bado kuna tatizo katika jamii ambalo
linaendelea katika kwani wanafanya mambo hayo wakati wanatambua ni kosa
kisheria na wanawanyima haki watoto wa kike.
“Hizi imani za ng’ombe wengi ndizo
huchangia kuwafanya watoto wa kike waendelee kuolewa katika umri mdogo,
ni kosa tena kosa kisheria, lazima tuungane na mashirika kupinga vitengo
hivyo, tumpe nafasi mtoto wa kike asome,” amesema Golwike.
Ametaja baadhi ya mikoa ikiwemo ya
Shinyanga, Dodoma, Mara, Rukwa, Katavi na Tabora bado kuna malalamiko
mengi kuhusu vitendo hivyo ambavyo vinafanyika usiku na mchana.
Awali Mkurugenzi kutoka Shirika la Save
the Children Makao makuu Dar es Salaam Bi.Angela Makota,amesema kuwa
ndoa za utotoni zimekuwa kikwazo kwa watoto na kuwanyima haki za kupata
Elimu pamoja na mahitaji muhimu ya watoto.
”Watoto wadogo wamekuwa wakipata madhara
wakiwa kwenye ndoa kwani hupata shida kuhimili maumbile kutoka kwa
wanaume walio na umri mkubwa”amesema Bi.Makota
Kwa upande wake mratibu wa ufuatiliaji wa
Shirika la Save the Children, Kanuty Munishi, amesema mradi wa
mapambano hayo ulianza tangu 2017 wakijikita zaidi katika wilaya za
Kishapu na Ushetu zote za mkoa wa Shinyanga lakini akakiri licha ya
uelewa wa tatizo hilo, bado kunahitajika usimamizi wa kutosha.
Bw.Munishi amebainisha kuwa
hawajafanikiwa kwa asilimia kubwa kutokana na muda ambao walipewa na
mfadhiri ambao ni miaka miwili kwani kubadiri tabia za watu ambao
wamezirithi kutoka mababu zao.
Vile vile amesema watoto wengi wamekuwa
na mbinu za uelewa wa kujikinga na madhara hayo kwani wanaposhauriwa
kwamba wasifanye vizuri katika mitihani ya darasa la saba ili waolewe,
huitikia lakini kwa vitendo hawafanyi hivyo.
Naye Bw.Paul Robert kutoka Ushetu amekiri
kuwa wazazi wengi bado wanakutana na tatizo hilo ambalo amesema ili
kulimaliza, haihitajiki nguvu kubwa bali ni uelewa tu kuhusu thamani ya
mtoto wa kike.
0 comments:
Post a Comment