Tuesday, July 16, 2019

UMASKINI NI KIKWAZO VITA DHIDI YA MIMBA ZA UTOTONI

MKURUGENZI wa Maendeleo ya jamii kutoka Wizara ya Afya maendeleo ya jamii jinsia  wazee na watoto, Patrick Golwike,akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha ya tathimini khusu ndoa za utotoni iliyoitishwa na Shirika la Save the Children iliyofanyika jijini Dodoma.

Mkurugenzi kutoka Save the Children Makao Makuu Dar es Salaam Bi.Angela Makota akitoa taarifa wakati wa ufunguzi wa warsha ya tathimini khusu ndoa za utotoni iliyoitishwa na Shirika la Save the Children iliyofanyika jijini Dodoma.

Mkurugenzi Idara ya Watoto wizara ya Afya Sebastian Kitiku,akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha ya tathimini khusu ndoa za utotoni iliyoitishwa na Shirika la Save the Children iliyofanyika jijini Dodoma.

Mratibu wa ufuatiliaji wa Shirika la Save the Children, Kanuty Munishi,akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani)wakati wa ufunguzi wa warsha ya tathimini khusu ndoa za utotoni iliyoitishwa na Shirika la Save the Children iliyofanyika jijini Dodoma.

Sehemu ya wadau wakifatilia wakati wa ufunguzi wa warsha ya tathimini khusu ndoa za utotoni iliyoitishwa na Shirika la Save the Children iliyofanyika jijini Dodoma.

MKURUGENZI wa Maendeleo ya jamii kutoka Wizara ya Afya maendeleo ya jamii jinsia  wazee na watoto, Patrick Golwike,akiwa katika picha ya pamoja na viongozi kutoka Shirika la Save the Children na wadau mara baada ya kufungua warsha ya tathimini khusu ndoa za utotoni iliyoitishwa na Shirika la Save the Children iliyofanyika jijini Dodoma.


…………………….

Na.Alex Mathias,Dodoma

MKURUGENZI wa maendeleo ya jamii kutoka Wizara ya Afya maendeleo ya jamii jinsia  wazee na watoto, Patrick Golwike, ametaja miongoni mwa vitu vinavyosababisha watoto wa kike kuolea katika umri mdogo kwamba ni uelewa mdogo kuhusu watoto wa kike kuwa wana soko hivyo hutolewa ng’ombe wengi, kukubali kutaliwa na waume zao na umasikini wa kipato.

Hayo ameyabainisha leo ijini Dodoma, alipokuwa anamuwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara hiyo kitengo cha maendeleo ya jamii, John Jingu, wakati wa ufunguzi wa warsha ya tathimini kuhusu ndoa za utoto iliyoitishwa na Shirika la Save the Children ambapo amesema mabinti wadogo hutolewa ng’ombe kati ya 25 hadi 50 kiwango ambacho hakifikii kwa mwanamke mtu mzima.

BW.Golwike amesema pamoja na juhudi kubwa za serikali katika vita hiyo, bado kuna tatizo katika jamii ambalo linaendelea katika kwani wanafanya mambo hayo wakati wanatambua ni kosa kisheria na wanawanyima haki watoto wa kike.

“Hizi imani za ng’ombe wengi ndizo huchangia kuwafanya watoto wa kike waendelee kuolewa katika umri mdogo, ni kosa tena kosa kisheria, lazima tuungane na mashirika kupinga vitengo hivyo, tumpe nafasi mtoto wa kike asome,” amesema Golwike.

Ametaja baadhi ya mikoa ikiwemo ya Shinyanga, Dodoma, Mara, Rukwa, Katavi na Tabora bado kuna malalamiko mengi kuhusu vitendo hivyo ambavyo vinafanyika usiku na mchana.

Awali Mkurugenzi kutoka Shirika la Save the Children Makao makuu Dar es Salaam Bi.Angela Makota,amesema kuwa ndoa za utotoni zimekuwa kikwazo kwa watoto na kuwanyima haki za kupata Elimu pamoja na mahitaji muhimu ya watoto.

”Watoto wadogo wamekuwa wakipata madhara wakiwa kwenye ndoa kwani hupata shida kuhimili maumbile kutoka kwa wanaume walio na umri mkubwa”amesema Bi.Makota

Kwa upande wake mratibu wa ufuatiliaji wa Shirika la Save the Children, Kanuty Munishi, amesema mradi wa mapambano hayo ulianza tangu 2017 wakijikita zaidi katika wilaya za Kishapu na Ushetu zote za mkoa wa Shinyanga lakini akakiri licha ya uelewa wa tatizo hilo, bado kunahitajika usimamizi wa kutosha.

Bw.Munishi amebainisha kuwa hawajafanikiwa kwa asilimia kubwa kutokana na muda ambao walipewa na mfadhiri ambao ni miaka miwili kwani kubadiri tabia za watu ambao wamezirithi kutoka mababu zao.

Vile vile amesema watoto wengi wamekuwa na mbinu za uelewa wa kujikinga na madhara hayo kwani wanaposhauriwa kwamba wasifanye vizuri katika mitihani ya darasa la saba ili waolewe, huitikia lakini kwa vitendo hawafanyi hivyo.

Naye Bw.Paul Robert kutoka Ushetu amekiri kuwa wazazi wengi bado wanakutana na tatizo hilo ambalo amesema ili kulimaliza, haihitajiki nguvu kubwa bali ni uelewa tu kuhusu thamani ya mtoto wa kike.

No comments:

Post a Comment