Rais wa Shirikisho la Wafanyabiashara wa
Madini, John Bina akizungumza katika Kongamano baina ya Wafanyabiashara
wa sekta ya madini na Tume ya Madini kwa kushiriakana na Mamlaka ya
Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) lililofanyika leo Jumatatu
(Julai 8, 2019) wakati wa Maonesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa
yanayoendelea katika Viwanja vya Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Madini
la Taifa (STAMICO) akizungumza katika Kongamano baina ya Wafanyabiashara
wa sekta ya madini na Tume ya Madini kwa kushiriakana na Mamlaka ya
Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) lililofanyika leo Jumatatu
(Julai 8, 2019) wakati wa Maonesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa
yanayoendelea katika Viwanja vya Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo
akizungumza katika Kongamano baina ya Wafanyabiashara wa sekta ya madini
na Tume ya Madini kwa kushiriakana na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara
Tanzania (TANTRADE) lililofanyika leo Jumatatu (Julai 8, 2019) wakati wa
Maonesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika Viwanja
vya Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo
akimkabidhi mmoja wa wafanyabiashara wa sekta ya madini, cheti maalum
cha ushiriki wa kongamano baina ya wafanyabiashara baina ya
Wafanyabiashara wa sekta ya madini na Tume ya Madini kwa kushiriakana na
Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) lililofanyika leo
Jumatatu (Julai 8, 2019) wakati wa Maonesho ya 43 ya Biashara ya
Kimataifa yanayoendelea katika Viwanja vya Julius Nyerere Jijini Dar es
Salaam.

(NA MPIGAPICHA WETU)
…………………..
Na Mwandishi Wetu,MAELEZO
DAR ES SALAAM
NAIBU Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo
amesema Serikali ipo macho masaa 24 katika siku 7 za wiki na itaendelea
kuwabaini kuwakamata na kuwatia hatiani watoroshaji wa madini sambamba
na kulinda rasilimali hizo, kwa kuwa watoroshaji hao wamekuwa
wakiwahujumu Watanzania na kurudisha nyuma maendeleo yao.
Akizungumza katika Kongamano baina ya
Wadau wa Madini lililoandaliwa na Tume ya Madini kwa kushirikiana na
Mamlaka ya Maendeleo ya Baiashara Tanzania (TANTRADE) leo (Jumatatu
Julai 8, 2019) katika Maonesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa
yanayoendelea katika Viwanja vya Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam,
Waziri Nyongo alisema kitendo cha utoroshaji wa madini ni kosa kisheria
na hivyo Wafanyabiashara wote wanatakiwa kufuata utaratibu uliowekwa na
Serikali.
Kwa mujibu wa Waziri Nyongo katika mwaka
wa fedha 2018/19 Serikali kupitia Tume ya Madini imevunja rekodi katika
ukusanyaji wa mapato ya madini hatua iliyotokana na jitihada mbalimbali
zilizofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano, ambapo kiasi cha Tsh Bilioni
310 ziliweza kukusanywa hatua iliyotokana na kudhibiti mianya ya
utoroshaji wa rasilimali za madini.
“Tangu uhuru nchi yetu haikuwahi
kukusanya kiasi kikubwa cha fedha ambacho ni mapato yatokanayo na madini
ya kiasi cha Tsh Bilioni 310, hivyo Serikali itaendelea kuweka mkazo
kuzuia njia za panya ambazo zimekuwa zikitumiwa na watoroshaji wa madini
kutorosha madini yetu na hivyo kuikosesha Serikali mapato” alisema
Nyongo.
Aidha Waziri Nyongo alisema katika mwaka
wa fedha 2019/2020 Serikali kupitia Tume ya Madini imepanga kukusanya
kiasi cha Tsh Bilioni 470 na hivyo aliwataka watendaji wa Tume hiyo
kuhakikisha kuwa malengo hayo yanafikiwa kwa kufanya kazi kwa kuzingatia
kanuni, sheria na taratibu ikiwemo kuendelea kuwafichua na kuwakamata
Wafanyabiashara wasiotaka kufuata sheria.
Naibu Waziri Nyongo alisema Serikali
kupitia Tume ya Madini kamwe haitomwonea mfanyabiashara yoyote
anayafanya biashara zake kwa kufuata sheria ikiwemo kuuza madini yake
katika masoko yaliyofunguliwa na Serikali kwani kwa kufanya hivyo
kutawezesha Serikali kukusanya kodi yake pamoja na kuweza kuongeza
mapato ya serikali.
Aliongeza kuwa hadi sasa kuna jumla ya
masoko ya madini 29 yaliyofunguliwa katika maeneo mbalimbali nchini na
kusema Serikali imeweza mazingira wezeshi kwa wafanyabiashara kuuza
madini katika maeneo hayo katika masoko hayo kwa kuwa ni salama kwao na
pia yataiwezesha Serikali kutambua kiasi cha madini kinachozalishwa na
kuuzwa nchini.
Akifafanua zaidi Naibu Waziri Nyongo
aliitaka Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) kuendelea
kujenga mazingira wezeshi kwa wafanyabiashara na wadau wa sekta ya
madini ikiwemo kuwatafutia masoko na kuwatakutanisha mara kwa mara ili
kuweza kutambuana pamoja na kuweza kupeana ujuzi na maarifa mbalimbali.
Kwa upande wake Naibu Mkurugenzi Mkuu wa
TANTRADE Zanzibar, Latifa Hamisi alisema Ofisi yake itaendelea
kuimarisha ushiriakiano na wadau wote wa sekta ya biashara nchini
ikiwemo wadau wa madini kwa kuwajengea uwezo sambamba na kuwafutia
masoko ya uhakika wa bidhaa zao ndani na nje ya nchi.
Aliongeza kuwa TANTRADE itaendelea
kutumia majukwaa yake ya kibiashara ikiwemo mikutano ya mara kwa mara
baina yake na Wafanyabiashara pamoja na kutoa mafunzo kwa
wafanyabiashara hao ili kuhakikisha kuwa wanakuwa na uwezo wa kuzalisha
bidhaa bora zinazokithi masoko ya ndani na nje ya nchi.
Naye Rais wa Shirikisho la
Wafanyabiashara wa Madini Nchini (FEMATA) John Bina aliiomba TANTRADE
kuweka utaratibu wa kuwatembelea wachimbaji wadogo wa madini katika
maeneo mbalimbali nchini ili kuweza kuzitambua changamoto zao kwa kuwa
kupitia utaratibu huo utawawezesha kutambua mchango wao katika
uzalishaji wa madini na nafasi waliyonayo katika kukuza uchumi wa nchi.
0 comments:
Post a Comment