Naibu Katibu Mkuu Ofisi
ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Balozi Joseph Sokoine leo
amefungua Mafunzo ya Msasa ya Uwezeshaji kuhusu Mashamba darasa kwa
Maafisa viungo wa mradi kutoka Wizara na timu za uwezeshaji za wilaya wa
mradi wa kurejesha ardhi iliyoharibika na kuongeza usalama wa chakula
katika maeneo kame ya nch (LDFS), yanayofanyika katika Chuo Kikuu cha
Sokoine cha Kilimo, Morogoro
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu
wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Balozi Joseph Sokoine akizungumza na
Profesa Henry Mahoo wa Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (katikati) na Dkt.
Moses Temi Mkufunzi Mkuu wa Shamba Darasa katika kituo cha Mafunzo ya
Kilimo Nkindo wilaya ya Mvomero mara baada ya kufunguaMafunzo ya Msasa
ya Uwezeshaji kuhusu Mashamba darasa kwa Maafisa viungo wa mradi kutoka
Wizara na timu za uwezeshaji za wilaya wa mradi wa kurejesha ardhi
iliyoharibika na kuongeza usalama wa chakula katika maeneo kame ya nchi
(LDFS), yanayofanyika katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo, Morogoro
…………………………………………….
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu
wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Balozi Joseph Sokoine leo amefungua
Mafunzo ya Msasa ya Uwezeshaji kuhusu Mashamba darasa kwa Maafisa viungo
wa mradi kutoka Wizara na timu za uwezeshaji za wilaya wa mradi wa
kurejesha ardhi iliyoharibika na kuongeza usalama wa chakula katika
maeneo kame nchini (ldfs), katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo,
Morogoro.
“Ni matumaini yangu kuwa elimu na ufahamu mtakauopata kupitia
mafunzo haya, mtaitumia katika kufanikisha uanzishaji wa mashamba darasa
katika maeneo ya mradi” alisema Balozi Sokoine.
Mafunzo hayo ya siku 5 yanalenga kujenga uwezo kwa washiriki
katika uanzishaji wa mashamba darasa katika vijiji na shehia ambako
mradi wa LDFS unatekelezwa.
Tanzania kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo wamekuwa
wakitekeleza miradi inayolenga kuongeza uzalishaji wa mazao ya kilimo na
mifugo kwa kusogeza karibu teknolojia kwa wakulima. Lengo likiwa ni
kuongeza usalama wa chakula na kuongeza kipato cha jamii. Mradi wa LDFS
ambao umeandaa mafunzo haya ni mfano wa juhudi hizo za Serikali. Juhudi
hizi zinahusisha uingizaji na matumizi ya teknolojia mpya ikiwemo
matumizi sahihi ya mbolea, mbegu zenye ubora; uboreshaji wa nyanda za
malisho; utoaji wa huduma za ugani na mafunzo kupitia shamba darasa.
Juhudi hizi zote zina lengo la urejesha ardhi iliyoharibika ili iweze
kuendelea kuzalisha mazao ya kilimo, mifugo na misitu.
Kwa upande wake Mratibu wa Mradi huo wa LDFS Bw. Joseph Kihaule
amesema mradi huo utajumuisha na uanzishwaji wa mashamba darasa 100.
Wawezeshaji wa mradi huo ni Shirika la Kilimo na Chakula Duniani
(FAO), Chuo cha Kilimo cha Sokoine (SUA) na Wakala wa Taifa wa Mbegu za
Miti Tanzania (TTSA) ambapo washiriki wa mafunzo hayo wametoka Wizara
za Kilimo, Maliasili na Utalii, Maji, Mifugo na Uvuvi, Ofisi ya Makamu
wa Rais, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Idara ya Mazingira,
Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Zanzibar. Aidha, washiriki
wengine ni kutoka katika Halmashauri zinazotekeleza Mradi za Mkalama,
Micheweni, Magu, Nzega na Kondoa, pamoja waalikwa rasmi Daktari Moses
Temi na Bwana Charles Mjema.
Sehemu ya Wajumbe walioshiriki
Mafunzo ya Msasa ya Uwezeshaji kuhusu Mashamba darasa kwa Maafisa viungo
wa mradi kutoka Wizara na timu za uwezeshaji za wilaya wa mradi wa
kurejesha ardhi iliyoharibika na kuongeza usalama wa chakula katika
maeneo kame ya nchi (LDFS), yanayofanyika katika Chuo Kikuu cha Sokoine
cha Kilimo, Morogoro . (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu
wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Balozi Joseph Sokoine
(katikati)akihutubia wakati wa ufunguzi Mafunzo ya Msasa ya Uwezeshaji
kuhusu Mashamba darasa kwa Maafisa viungo wa mradi kutoka Wizara na timu
za uwezeshaji za wilaya wa mradi wa kurejesha ardhi iliyoharibika na
kuongeza usalama wa chakula katika maeneo kame ya nchini (LDFS),
yanayofanyika katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo, Morogoro,
wengine pichani ni Mratibu wa Mradi huo Bw. Joseph Kihaule (kushoto) na
Kaimu Mkurugenzi wa Mazingira Bw. Faraja Ngerageza. (Picha na Ofisi ya
Makamu wa Rais)
Sehemu ya Wajumbe walioshiriki
Mafunzo ya Msasa ya Uwezeshaji kuhusu Mashamba darasa kwa Maafisa viungo
wa mradi kutoka Wizara na timu za uwezeshaji za wilaya wa mradi wa
kurejesha ardhi iliyoharibika na kuongeza usalama wa chakula katika
maeneo kame ya nchi (LDFS), yanayofanyika katika Chuo Kikuu cha Sokoine
cha Kilimo, Morogoro . (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Sehemu ya Washiriki wa Mafunzo ya
Msasa ya kuhusu Uwezeshaji Mashamba darasa kwa Maafisa viungo wa mradi
kutoka Wizara na timu za uwezeshaji za wilaya wa mradi wa kurejesha
ardhi iliyoharibika na kuongeza usalama wa chakula katika maeneo kame ya
nchi (ldfs),wakiwa kwenye uchambuzi yakinifu wa mimea na ikolojia
shambani katika Chuo Kikuu cha Sokoine (SUA) mkoani Morogoro. (Picha na
Ofisi ya Makamu wa Rais)
Sehemu ya Washiriki wa Mafunzo ya
Msasa ya kuhusu Uwezeshaji Mashamba darasa kwa Maafisa viungo wa mradi
kutoka Wizara na timu za uwezeshaji za wilaya wa mradi wa kurejesha
ardhi iliyoharibika na kuongeza usalama wa chakula katika maeneo kame ya
nchi (ldfs),wakiwa kwenye makundi kufanya uchambuzi yakinifu wa mimea
na ikolojia shambani katika Chuo Kikuu cha Sokoine (SUA) mkoani
Morogoro. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

0 comments:
Post a Comment