Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia Profesa. Joyce Ndalichako amekagua maendeleo ya ukarabati na
upanuzi wa shule ya msingi Mwisenge na kuridhishwa na kasi na ubora wa
kazi ya ukarabati inayoendelea ambao umefikia asilimia 60.
Ukarabati wa Shule ya
Mwisenge ambayo alisoma baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere
ulianza kufanyika baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.
Dkt John Pombe Joseph Magufuli kuitembelea na kuagiza ikarabatiwe na
kujengewa ukuta.
Akizungumza akiwa katika
ziara ya kukagua maendeleo mradi huo amesema ameridhishwa na kasi hiyo
ya ujenzi huo ambao unahusisha ukarabati wa majengo ya kale, ukarabati
wa madarasa, mabweni, ujenzi wa madarasa na mabweni mapya, ujenzi wa
uzio kuzunguka shule hiyo, ukarabati wa mnara wa kumbukumbu pamoja na
uboreshajii wa mazingira ya nje.
Mradi huo unaogharimu kiasi
cha sh Milioni 706 ambazo zimetolewa na Wizara ya Elimu,Sayansi na
Teknolojia unatarajiwa ulianza Mwezi April na utakamilika na kukabidhiwa
mwezi Septemba mwaka huu.
“Nimefurahishwa na hatua
iliyofikiwa mpaka sasa na viwango vya ujenzi wa madarasa na mabweni nao
ni imara, hata ujenzi wa ukuta unafanyika vizuri, kuta za mabweni ni
ndefu na zitawafanya watoto wakiwa ndani wapate hewa vizuri”alisema
Profesa Ndalichako.
Shule hiyo awali ilikuwa
haina ukuta kabisa hali ambayo ilisababisha mazingira kuwa hatarishi kwa
watoto hasa wenje ulemavu wa Ngozi. Ukuta huo umeshajengwa kuzunguka
shule yote.
Katika hatua ingine
ilionekana ukarabati wa baadhi ya majengo ya kihistoria katika shule
hiyo ambapo moja ya jengo linalengwa kuwa zahanati itakayotumika kwa
ajili ya wanafunzi umesimama. Akitoa taarifa ya ujenzi Mkuu wa Shule
hiyo…. amesema majengo hayo yalisimama kutokana na Idara ya Mambo ya
Kale kutowasilisha maoendejezo yao baafa ya kufanya tathmini.
Waziri Ndalichako amewataka
watalaam hao kufika mara moja ili kutoa muongozo unaohitajika kuwezesha
kukamilisha ukarabati wa majengo hayo kwa wakati.
“Ni vizuri ndugu zetu wa
Mambo ya Kale wafike mara moja ili kutoa muongoza wa namna bora wa
kufanya ukarabati wa majengo haya ya kihistoria yanapaswa kukarabatiwa
kuwezesha ujenzi huo kukamilika mapema kuwezesha wanafunzi kupata fursa
ya kuyatumia, kwani kuendelea kuchelewesha taarifa hiyo ni kukwamisha
utekelezaji wa mradi.
Prof. Ndalichako amesema
lengo la wizara ni kuona shule hiyo inakamilika mapema ili kutimiza
maagizo aliyoyatoa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.
Jonh Pombe Magufuli ya kutaka shule hiyo ikarabatiwe iwe na hadhi ya
Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Nyerere kuweka kumbukumbu nzuri ya
shule aliyosoma.
Ndalichako ameshauri
wajitahidi hiyo ikamilike mapema ikiwezekana kabla ya tarehe 14 Oktoba,
siku ya kumbukumbu ya Baba wa Taifa ili iwe sehemu ya maadhimisho hayo.
Mapema Mkuu wa Wilaya ya
Musoma , Dkt. Vicent Anney alimweleza waziri kuwa baadhi ya majengo
hayajakamilika kutokana na kusimamishwa kwa ukarabati wa majengo hayo ya
kihisitoria katika shule hiyo na Ofisi ya Mambo ya Kale yenye jukumu la
kutoa muongozo wa namna gani ukarabati unapaswa kufanywa, ingawa toka
kusimamishwa wataalam hao bado hawajafika kutoa maelekezo yeyote yale na
tayari wameshawaandikia barua ya kuwakumbusha.
“Lengo letu ni kuhakikisha
ifikapo Oktaba 30 ukarabati huu uwe yamekamilika kabisa, lakini
changamoto iliyopo sasa ni kukwama kwa ukarabati wa baadhi ya majengo ya
kihistoria ambayo wenzetu wa mambo ya kale waliagiza ukarabati wake
usimame mpaka watakapofika na kutoa maelekezo ya namna gani ufanyike
lakini mpaka sasa hakuna mtaalam yeyote aliyefika pamoja na kuwaandikia
barua, Amesema Dkt. Anney.
Dkt. Anney ameishukuru wizara
kwa kuipatia Wilaya ya Musoma fedha za kutekeleza miradi mbalimbali
inayoendelea ikiwemo shilingi milioni 152 kwa ajili ya ujenzi wa ofisi
za udhibiti ubora wa shule, ukarabati wa shule ya sekondari ya ufundi
musoma ambayo imewekewa mitambo pamoja na vifaa vya kufundishia
iliyogharimu kiasi cha shilingi bilioni 1.2.
0 comments:
Post a Comment