Na Saida Issa, Dodoma
MBUNGE wa Tandahimba Katani Ahmad katani amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuruhusu mikutano ya kisiasa huku akiwataka watanzania kuendelea kuwa na Imani na kuiunga mkono Serikali ya Chama Cha Mapinduzi.
Mbunge huyo alisema hayo Leo Katika viwanja vya Bunge Jijini hapa alipokuwa akieleza maamuzi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuruhusu mikutano ya vyama vya siasa nchini.
Alisema kuwa kuruhusiwa kwa mikutano ya vyama vya siasa kutaleta maendeleo ya Taifa sababu wapinzani watasaidia katika kukosoa yale ambayo yanafanya na Serikali na kuwashauri watumie mikutano hiyo kama njia ya kunadi sera zao na kukosea Serikali pasipo kutumia lugha za matusi.
"Mheshimiwa Rais kuruhusu suala hili kutasaidia mengi sana ikiwemo Serikali kukosolewa kwani mkiwa watu wa Serikali moja kunawakati mnaweza msijikosoe kwaiyo Kwa kuruhusiwa kwa vyama vya siasa kutasaidia kuifanya Serikali kufanya vizuri zaidi,
Tutapata muda mwingi wa kuelezwa mapungufu na wapinzani nasisi tutahakikisha tunafanya vizuri zaidi na sisi hatuna shaka na kuwepo kwa upinzani kwani tayari miradi mingi imefanyika chini ya serikali ya chama Cha Mapinduzi,"alisema.
Aidha alisema kuwa Taifa ni lakila mmoja hata wapinzani pia wanahaki ya kuyasema yale mapunguvu wanayoyaona na kuwahakikishia wananchi kuwa Mheshimiwa Rais anaendelea kufanya makubwa katika kutekeleza ilani ya chama Cha Mapinduzi.
0 comments:
Post a Comment