Na Saida Issa,Dodoma
Mbunge wa Moshi mjini Priscus Tarimo alisema kuwa kuwepo na kutokuwepo kwa vyama vingi hakuna sababu ya kupima maendeleo bali kukiwa na viongozi Imara kutasaidia Nchi kupiga hatua.
Mbunge huyo aliyasema katika viwanja vya Bunge alipokuwa akizungumzia hali ya siasa kwa sasa mara baada ya vyama vingi kuanza mikutano.
Alisema kuwa kupitia chama cha Mapinduzi wameweza kutekeleza ahadi walizoahidi na kuwataka wananchi kuweza kutathmini yaliyofanyika kwa kipindi Cha miaka 5.
"Wananchi wanatakiwa kutizama yale tuliyoyafanya kupitia chama Cha Mapinduzi kwa kipindi Cha miaka 5 na mimi kama mbunge wa CCM sina tatizo na uwepo wa vyama vingi,"alisema.
Aidha alisema kuwa wanaweza kuwa wanafanya vizuri hata bila kuwepo kwa vyama vingi lakini pia kuwepo kwa vyama hivyo ni chachu ya kuendelea kufanya vizuri zaidi.
0 comments:
Post a Comment