METDO Tanzania

METDO Tanzania

Tuesday, January 31, 2023

SHULE BORA PROGRAMU, WAANDISHI HABARI KUSHIRIKIANA KUINUA ELIMU YA AWALI NA MSINGI

 

Meneja wa Mawasiliano kutoka Programu ya  ya Serikali ya Shule Bora Raymond Kanyambo akizungumza na Wawakilishi wa waandishi na wasimamizi wa vyombo vya habari mkoani Singida wakati wa Mkutano wa Uhamasishaji wa programu hiyo uliofanyika  jana January 31 Mjini Manyoni  


Afisa elimu Mkoa wa Singida Maria Lyimo akizungumza kwenye mkutano wa uhamasishaji programu ya serikali ya Shule bora hapo jana.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida Mwl. Dorothy Mwaluko azungumza na Wawakilishi wa vyombo vya habari mkoa Singida katika wa Mkutano wa Uhamasishaji wa programu hiyo uliofanyika  jana January 31 Mjini Manyoni  

Mkutano ukiendelea




Na Hamis Hussein - Manyoni, Singida

PROGRAM ya Serikali ya Tanzania chini ya ufadhili wa serikali ya Uingereza inayotekelezwa katika mikoa 9 ikiwa na lengo la kuinua ubora wa elimu ya awali na msingi ijulikanayo kwa jina la SHULE BORA imewahimiza Wawakilishi,Wasimamizi na wahariri wa vyombo vya habari Mkoa wa Singida kushiriki kikamilifu katika program hiyo kwa kuandika na kuripoti changamoto na vikwazo vinavyowakwamisha watoto kushindwa kupata elimu bora hapa nchini.

Akizungumzia Programu  hiyo kwenye Mkutano wa uhamasishaji wa programu ya shule bora kwa wasimamizi na wahariri wa vyombo vya habari mkoani hapa Raymond Kanyambo  amesema shule bora inabaini changamoto zinazokwamisha ujifunzaji na ufundishaji wa watoto elimu ya awali na msingi na kuzitafutia ufumbuzi ili kila mtoto wa kitanzania anapata elimu bora .

Kanyambo amesema kwenye program hiyo kundi la waandishi wa Habari litakuwa msaada mkubwa endapo litashirikiana na shule bora kuzibaini changamoto hizo zinazokwamisha ujifunzaji na ufundishaji wa watoto shuleni hivyo akatoa wito kwa wandishi wa Habari Kuwajibika katika suala hilo.

“Tunategemea mshiriki katika programu hii kuzibaini baadhi ya changamoto zinazopelekea watoto wasisome ama wasipate elimu bora na kisha itafutwe njia ya kuondoa changamoto hiyo, kama waandishi mnahaki ya kuhoji hali ya uandikishaji wa wanafunzi wangapi wameripoti, wangapi wamefaulu, je kundi wenye ulemavu lipo vipi kitaluuma?, hivyo mshirikiane na sisi katika kuinua  elimu kwa watoto wetu ” Alisema Kanyambo.

Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano Serikalini kutoka TAMISEMI Nteghenjwa Hosea akiongoza majadiliano ya namna waandishi watakavyoshirikishwa katika kuandika habari mbalimbali ikiwemo zile za mradi ya shule bora.

 Afisa Habari Mkoa wa Singida Bashir Juma (Kulia) na Mwandishi wa habari Imani Musigwa( Kushoto) Wakiandika mambo muhimu kwenye Mkutano huo.


Kaimu Afisa Habari Halmashauri ya Itigi  Bw. Luganuzi akichangia mada ya ushirikishwaji wa wandishi wa habari mkoani Singida . 

Meneja wa Mawasiliano wa Shule Bora Raymond Kanyambo akiwasilisha mambo mbalimbali kwenye  mkutano huo.

Ameongeza kwa kutaja malengo ya shule bora kuwa ni pamoja na kuboresha Ujifunzaji wa watoto wote shuleni kuhakikisha watoto wote wanaenda shule na kusoma, Kuboresha Ufundishaji wa walimu ili wawasaidie watoto kupata elimu bora , Ujumwishaji wa watoto wote shuleni  kuhakikisha wanapata elimu bora katika mazingira salama na wezeshi huku lengo lingine akitaja kuwa ni kuimarisha mifumo ya usimamiaji elimu ambapo kundi lililolengwa ni la wasimamizi wa ubora wa elimu wakiemo viongozi wa halmashauri na wadhibiti ubora.

 Awali akifungua Mkutano huyo wa shule bora na waandishi wa habari  Katibu Tawala Mkoa wa Singida, Mwalimu Dorothy Mwaluko,aliwataka wasimamizi wa program ya  wa Shule Bora inayotekelezwa katika mikoa tisa nchini kutengeneza mfumo wa kutoa mafunzo kwa walimu wa Mkoa wa Singida ili kuinua viwango cha elimu mkoani humo

"Msiwe na kituo cha mafunzo sehemu moja, Mnatakiwa kuwa na vituo walau Kila halmashauri kuwe na 'trainers' Pamoja na Vituo vya kufanyia Mafunzo na kuwakutanisha walimu wengi ili wote waguswe kwa wakati mmoja" amesema

Mwl. Mwaluko alitumia nafasi hiyo kuwasistiza waandishi wa Mkoa wa Singida katika kuelekea kilele cha maadhimisho ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwake ,kuandika habari za kutanga vivutio vilivyopo ndani ya mkoa pamoja na zile zitakazo saidia kutatua changamoto kwenye jamii kuliko zitachochea mifarakano na kurudisha nyuma Maendeleo ya wananchi 

Mratibu wa Program hiyo Mkoa wa Singida, Samwel Daniel alisema program hiyo inawahusu wanafunzi wa shule za awali na msingi na kuwa walitoa mafunzo endelevu kwa walimu wakuu, mahiri na taaluma ambapo walimu 1774 wamenufaika nayo.

Programu ya Shule Bora imefadhiliwa na Uingereza kwa Paundi milioni 89 ambazo ni sawa na Bilioni 271 za kitanzania, ambazo zitatumika kwaajili ya uinua ubora wa elimu kwenye mikoa yote 9 ili kuhakikisha watoto wote hata wale wenye changamoto mbalimbali wanapata fursa ya kusoma.



Washiriki wa Mkutano huyo ulioandaliwa na shule bora kwa ufadhili wa Serikali ya Uingereza wakiwa kwenye picha ya Pamoja baada ya ufunguzi kufanyika.






 

 

 

 

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com