Mkurugenzi wa MISA Tanzania, Sengiyumva
Gasirigwa akifafanua jambo kwenye mafunzo kwa viongozi (wahariri na
mameneja) wa vyombo mbalimbali vya habari hapa nchini.
Na George Binagi, Mwanza
Mtaalam Mkufunzi kutoka nchini Ufaransa, Linda Hervieux akiwasilisha mada kwenye mafunzo hayo.
Wakili wa Mahakama Kuu Tanzania, James Marenga akiwasilisha mada kuhusu sheria mbalimbali za habari kwenye mafunzo hayo.
Washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia mada kutoka kwa Wakili James Marenga.
Mhariri kutoka kampuni ya Sahara Media Group (Star TV) ya jijini Mwanza, Leonard Mapuli akichangia mada kwenye mafunzo hayo.
Mkuu wa Kituo cha Luninga Sitar TV
(Sahara Media Group), Moses Buhilya (wa tatu kulia) akiongoza
wanakikundi wenzake kufanya kazi za makundi kwenye mafunzi hayo.
Baadhi ya washiriki Deogratius Nsokolo
(kushoto) kutoka ITV Mkoa Kigoma pamoja na Veronica Natalis (kulia)
kutoka DW Mkoa Shinyanga wakijadiliana jambo kwenye mafunzo hayo.
Japhet Sanga kutoka Ubalozi wa Marekani
nchini Tanzania (kulia) pamoja na Sarah Bushman kutoka taasisi ya IREX
Marekani (kushoto) wakifuatilia mafunzo hayo.
Washiriki wakitoa mrejesho wa kile walichojifunza kwenye mafunzo hayo.
Mhariri kutoka Clouds Media Group, Joyce
Shebe (kushoto) akitoa mrejesho wa kile alichojifunza kwenye mafunzo
hayo mbele ya wenzake.
Mkuu wa Kituo Msaidizi kutoma Redio
Victoria FM iliyopo Msoma mkoani Mara akitoa mrejesho kuhusu
alichojifunza kwenye mafunzo mafunzo hayo.
Mafunzo
hayo ya siku tano yalianza Jumatatu Julai 22, 2019 hadi Ijumaa Julai
26, 2019 katika hotel ya Aden Palace Hotel jijini Mwanza, yakiandaliwa
na taasisi ya MISA Tanzania kwa kushirikiana na ile ya IREX kutoka
Marekani pamoja na Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania.
Mada
mbalimbali zinawasilishwa kwenye mafunzo hayo kwa viongozi wa vyombo vya habari
nchini Tanzania ili kuwajengea uwezo wa kusimamia weledi kazini ikiwemo kuhakikisha habari linganifu hususani kipindi
cha uchaguzi zinapewa kipaumbele.
Mada
nyingine ni pamoja na jukumu la vyombo vya habari katika kukuza demokrasia,
uandishi wa habari unaozingatia maadili, usalama wa waandishi wa habari mtandaoni, nafasi
ya mwanamke katika vyombo vya habari na chaguzi mbalimbali pamoja na tahadhari
wanazohitaji waandishi wa habari wakiwa kwenye mazingira hatarishi ya kazi.
0 comments:
Post a Comment