Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akikagua Banda la Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) wakati akikagua maandalizi ya Maadhimisho ya 27 ya sikukuu ya wakulima maarufu kama (Nane Nane) yatakayofanyika kuanzia tarehe 1-8 Agosti 2019 Katika viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akiwa na watumishi wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) wakati akikagua maandalizi ya Maadhimisho ya 27 ya sikukuu ya wakulima maarufu kama (Nane Nane) yatakayofanyika kuanzia tarehe 1-8 Agosti 2019 Katika viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akipewa maelezo kuhusu matumizi ya mifuko ya kuhifadhia mahindi ya PIC'S wakati alipotembelea Banda la Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) wakati akikagua maandalizi ya Maadhimisho ya 27 ya sikukuu ya wakulima maarufu kama (Nane Nane) yatakayofanyika kuanzia tarehe 1-8 Agosti 2019 Katika viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu.
Na Mathias Canal, Wizara ya
Kilimo-Simiyu
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet
Hasunga jana tarehe 30 Julai 2019 ametembelea na kujionea maandalizi ya
Maadhimisho ya 27 ya sikukuu ya wakulima maarufu kama (Nane Nane) yenye lengo
la kuwatambua na kuwaenzi Wadau Wakuu wa Sekta ya Kilimo ambao ni Wakulima,
Wafugaji, Wavuvi, Wanaushirika, Wasindikaji wa mazao ya kilimo, mifugo, uvuvi
na maliasili kwa mchango wao mkubwa wanaoutoa katika kuendeleza uchumi wa nchi
yetu.
Mhe Hasunga pamoja na mambo
mengine akiwa katika Banda la Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA)
ameutaka uongozi wa taasisi huyo kuongeza juhudi za utoaji elimu kwa
wananchi kuhusu umuhimu wa matumizi ya mifuko maalumu ya kuhifadhia nafaka ya
PIC'S.
Mhe Hasunga amesema kuwa
NFRA inapaswa kutoa elimu hiyo ili iwafikie wakulima wengi kwani kufanya hivyo
itarahisisha huduma za uhifadhi wa mahindi ya wakulima ambao kwa muda mrefu
wamekumbwa na kadhia ya kushindwa kuhifadhi mahindi kwa ufasaha.
Pamoja na NFRA kutoa elimu
kwa wakulima kupitia vipindi mbalimbali vinavyorushwa na Televisheni lakini pia
amesisitiza kuwa NFRA inapaswa kuongeza uwezekano wa kuwafikia wakulima wengi
zaidi.
Mwaka huu wa 2019, sherehe
za Nanenane zinafanyika Kitaifa mjini Bariadi katika Viwanja vya maonesho ya
kilimo Nyakabindi katika Mkoa wa Simiyu hivyo Mhe Hasunga amepongeza Uongozi wa
mikoa ya Simiyu, Shinyanga na Mara kwa juhudi zao za kufanikisha kuingiza
uwanjani huduma za msingi ambazo ni maji na umeme.
Alisema kuwa jukumu hilo
kwa Serikali na Wadau wa Sekta Binafsi ni kuendeleza viwanja hivyo vya
Nyakabindi kwa kujenga mabanda ya maonesho ya kudumu na kuboresha huduma muhimu
za kijamii ili kuwe na maonesho endelevu yenye sura ya Kitaifa na Kimataifa.
Wakala wa Taifa wa Hifadhi
ya Chakula NFRA pamoja na Taasisi zingine za wizara ya Kilimo zimetuama Mkoani
Simiyu kwa ajili ya kutoa elimu kwa wakulima kuhusu majukumu wayafanyayo
kadhalika namna bora ya kuwa na Kilimo bora na chenye tija.
MWISHO.
0 comments:
Post a Comment