Waziri wa
Habari Utamaduni,Sanaaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe (katikati)
akiwa katika picha ya pamoja na Uongozi wa Klabu ya Dar es Salaam Young
Africans (Yanga) uliofika kijitambulisha ofisini kwake Jijini Dododma
leo Juni 04,2019.
*****************************************
Shamimu Nyaki-WHUSM
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa
na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe ameutaka uongozi mpya wa Klabu
ya Dar es Salaam Young Africans (Yanga) kufanya kazi kwa weledi na
ubunifu katika kuiletea mafanikio klabu hiyo pamoja na kuhakikisha
maslahi ya timu hiyo yanalindwa.
Mhe. Mwakyembe ameyasema hayo leo
Jijini Dodoma alipokutana na Uongozi wa Klabu hiyo ulioongozwa na
Mwenyekiti wake Prof. Mshindo Msolla ambao ulikuja kujitambulisha rasmi
kwa Waziri.
“Nawapongeza sana kwa kuaminiwa
na wanachama pamoja na wapenzi wa Klabu hii ambayo ina historia kubwa
katika soka hapa nchini hivyo ni jukumu lenu kuhakikisha timu hii
inaendelea kufanya vizuri ndani na nje ya nchi” Mhe. Mwakyembe.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa
Klabu hiyo Prof. Mshindo Msolla ameishukuru Serikali kwa msimamo wake
wa kuhakikisha klabu hiyo inaendelea kusimama licha ya kukaa muda mrefu
bila uongozi rasmi pamoja na kusaidia kutatua mgogoro uliokuwepo ndani
ya klabu hiyo.
Prof. Msolla ameongeza kuwa Klabu
hiyo inatarajia kufanya hafla ya kuichangia klabu itakayofanyika tarehe
15,juni 2019 Jijini Dar es Salaam ambapo amewataka wanachi na wapenzi wa
klabu kujitokeza katika hafla hiyo.
0 comments:
Post a Comment