Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na baadhi ya wataalam
wa Mkoa huo Mamlaka ya Chakula na Dawa, wakati wa uzinduzi wa Ofisi ya
Mamlaka hiyo Kanda ya Ziwa Mashariki itakayohudumia mikoa ya Simiyu,
Mara na Shinyanga na makao makuu yake yakiwa Bariadi Mjini, Uzinduzi
umefanyika Juni 20, 2019 Mjini Bariadi.
Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Chakula na
Dawa(TFDA) Kanda ya Ziwa Mashariki, Bi. Nuru Mwasulama akitoa taarifa
fupi ya uanzishwaji wa Kanda hiyo itakayohudumia mikoa ya Simiyu, Mara
na Shinyanga na makao makuu yake yakiwa Bariadi Mjini, katika uzinduzi
waa kanda hiyo uliofanyika Juni 20, 2019 Mjini Bariadi.
Baadhi
ya wataalam wa mkoa wa Simiyu na Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA)
wakifuatilia masuala mbalimbali ambayo yaliyokuwa yanaendelea katika
Uzinduzi wa Ofisi ya Mamlaka hiyo Kanda ya Ziwa Mashariki itakayohudumia
mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga na makao makuu yake yakiwa Bariadi
Mjini, Uzinduzi umefanyika Juni 20, 2019 Mjini Bariadi.Baadhi
ya viongozi, wataalam wa mkoa wa Simiyu na Mamlaka ya Chakula na
Dawa(TFDA) wakifuatilia masuala mbalimbali ambayo yaliyokuwa yanaendelea
katika Uzinduzi wa Ofisi ya Mamlaka hiyo Kanda ya Ziwa Mashariki
itakayohudumia mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga na makao makuu yake
yakiwa Bariadi Mjini, Uzinduzi umefanyika Juni 20, 2019 Mjini Bariadi.Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akimueleza jambo Kaimu Meneja wa
Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA) Kanda ya Ziwa Mashariki, Bi. Nuru
Mwasulama mara baada ya kuzindua rasmi Kanda ya Ziwa Mashariki ya
Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) itakayohudumia mikoa ya Simiyu, Mara
na Shinyanga, Juni 20, 2019 Mjini Bariadi.
Kaimu Mganga mkuu wa Mkoa, Dkt. Mugune
Maeka akitoa neno la shukrani mra baada ya kuhitishwa kwa uzinduzi wa
Kanda ya Ziwa Mashariki ya Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA)
itakayohudumia mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga, Juni 20, 2019 Mjini
Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony
Mtaka (katikati mbele) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya
viongozi, wataalam wa mkoa wa Simiyu na Mamlaka ya Chakula na
Dawa(TFDA) mara baada ya Uzinduzi wa Ofisi ya Mamlaka hiyo Kanda ya
Ziwa Mashariki itakayohudumia mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga na
makao makuu yake yakiwa Bariadi Mjini, Uzinduzi umefanyika Juni 20, 2019
Mjini Bariadi.
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na baadhi ya wataalam
wa Mkoa huo Mamlaka ya Chakula na Dawa, wakati wa uzinduzi wa Ofisi ya
Mamlaka hiyo Kanda ya Ziwa Mashariki itakayohudumia mikoa ya Simiyu,
Mara na Shinyanga na makao makuu yake yakiwa Bariadi Mjini, Uzinduzi
umefanyika Juni 20, 2019 Mjini Bariadi.
………………….
Na Stella Kalinga, Simiyu
Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA)
imefungua rasmi Ofisi ya Kanda mpya ya Ziwa Mashariki itakayohudumia
mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga ambapo makao makuu ya kanda hiyo
yatakuwa Mjini Bariadi mkoani Simiyu.
Akitoa taarifa kwa Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, Kaimu Meneja wa TFDA Kanda ya Ziwa
Mashariki, Bi. Nuru Mwasulama amesema mamlaka hiyo imeanzisha Kanda Mpya
ya Ziwa Mashariki inayojumuisha mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga ili
kusogeza huduma kwa wananchi na kuharakisha ukuaji wa uchumi wa kati
unaotegemea viwanda.
Amesema ofisi hii itajishughulisha na
usajili wa maeneo yanayo jihusisha na uzalishaji na uuzaji wa chakula,
dawa, vipodozi na vifaa tiba, kupokea maombi ya usajili wa bidhaa za
vyakula vinavyofungashwa, kufanya ukaguzi wa bidhaa za vyakula katika
soko kuwalinda walaji na kudhibiti usindikaji wa chakula dawa na
vipodozi.
Kazi nyingine zitakazofanywa na kanda hii
ni kutoa vibali vya uingizaji nchini na usafirishaji wa chakula nje ya
nchi, kufanya ufuatiliaji wa bidhaa za vyakula katika soko, kuhamasisha
matumizi sahihi ya dawa, vipodozi na vifaa tiba pamoja na kuelimisha na
kutoa taarifa kwa wadau na wananchi kwa ujumla kuhusu bidhaa
zinazothibitiwa na mamlaka.
Aidha, Mwasulama amesema Ofisi ya kanda
hii itatekeleza majukumu yake kwa kushirikiana na Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa, ambapo wataalam waliopo kwenye wilaya, manispaa, miji
na majiji watasimamia sheria ya chakula na dawa kwa mujibu wa kanuni ya
kukasimu baadhi ya majukumu na madaraka ya TFDA katika Halmashauri.
Akizungumza na baadhi ya wataalam wa Mkoa
wa Simiyu na TFDA katika ufunguzi huo, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.
Anthony Mtaka amesema ni vema Taasisi nyingine zinazohitajika katika
uwekezaji wa viwanda na maeneo mengine ya uwekezaji zikaiga mfano wa
TFDA kwa kusogeza huduma karibu na wananchi ili waweze kupata huduma
kwa wakati.
“Hiki kilichofanywa na TFDA ni vizuri
taasisi nyingine nazo ziige, kama leo TFDA ipo Simiyu kama Kanda ya Ziwa
Mashariki ningetamani kuwaona TBS, NEMC, OSHA wako Simiyu kama Kanda ya
Ziwa Mashariki na Taasisi zote ambazo kwenye uwekezaji wa viwanda na
maeneo mengine ya uwekezaji zinakuwa karibu na maeneo ya kutolea huduma”
alisisitiza Mtaka.
Katika hatua nyingine Mtaka ametoa wito
kwa watumishi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa wanaotekeleza majukumu
waliyokasimiwa na TFDA kufanya majukumu hayo kwa mujibu sheria huku
akiwaasa kuacha tabia ya kufungia biashara za wananchi bila
kuwaelimisha badala yake wawasaidie kuwapa elimu ili wazalishe bidhaa
bora kwa walaji.
Naye Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji wa
Bariadi, Dkt. Mike Mabimbi akizungumza kwa niaba ya waganga wakuu wa
wilaya ambao ni Makatibu wa kamati za ukaguzi wa chakula na dawa amesema
watahakikisha wanasimamia utekelezaji wa majukumu wanayokasimiwa na
TFDA kwa mujibu wa sheria na akashukuru TFDA kusogeza huduma karibu na
wananchi.
0 comments:
Post a Comment