Mkuu wa mkoa wa Iringa Ali Hapi akizungumza na wananchi wa tarafa ya Kiponzelo wilaya ya Iringa kuhusu na nishati ya umeme na jinsi gani serikali inahakikisha wananchi wanapata umeme kwa gharama nafuu
Mkuu
wa mkoa wa Iringa Ali Hapi akizungumza na wananchi wa tarafa ya
Kiponzelo wilaya ya Iringa kuhusu na nishati ya umeme na jinsi gani
serikali inahakikisha wananchi wanapata umeme kwa gharama nafuu
NA FREDY MGUNDA,IRINGA.
Tanzania imetajwa kuwa ni nchi ya kwanza
barani Africa kuwawezesha wananchi
waishio vijijini kupata umeme kwa gharama nafuu ikiwa ni njia mojawapo ya
kuwawezesha wananchi kukabiliana na changamoto ya kiuchumi kwa kukuza
miundombinu wezeshi ya uchumi vijijini.
Akizungumza wakati wa ziara ya awamu ya
pili ya Iringa Mpya Mkuu wa mkoa wa Iringa Ali Hapi alisema kuwa serikali
imekuwa ikitekeleza ahadi ya kutoa huduma ya nishati ya umeme vijijini kwa
gharama ambazo hakuna nchi nyingine barani Afrika inatoa.
Akiwa katika tarafa ya Kiponzelo Hapi
alisema kuwa wananchi wanatakiwa kuwa na subira wakati serikali imejipanga
kuhakikisha inamalizia kuwapa umeme katika vitongoji vyote nchi nzima
vilivyobaki.
“Rais wetu amekuwa anapambana kila
kukicha kuhakikisha wananchi wanakuza uchumi wao na kupata maendeleo kwa wakati
na ndio maana nishati ya umeme imekuwa ikitolewa kwa gharama nafuu nchi nzima”
alisema Hapi
Aidha Hapi aliongeza kuwa viongozi wote
waliopo ngazi za chini wanatakiwa kutekeleza majukumu yao kwa nafasi zao
kiufasaha na kuhakikisha wanatatua changamoto za wananchi ili kuhakikisha
wanakuza uchumi wa wananchi wa kawaida kuanzia ngazi za vitongoji.
Pia aliwataka wananchi wote kuacha tabia
ya kuendekeza maneno ya kinafiki kwa watendaji wa serikali kwa kuwazushia
taarifa ambazo zitawavunja moyo kufanya kazi kwa nguvu ili kumsaidia Mh. Rais
kuijenga Tanzania mpya ya viwanda na biashara nchini.
Alisema “ tumetumwa na rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania ili kuwasikiliza na kuwatataulia changamoto zilizopo
ndani ya uwezo wetu, nyinyi ndio ambao mmetuajiri kwahiyo ni lazima tuwatumikie
na kuhakikisha mnakuwa na maisha mazuri na kupunguza umasikini katika kaya
zenu”
Akijibia baadhi ya hoja za wananchi
kaimu meneja wa tanesco mkoa wa Iringa injia Festo Ndamenya alisema kuwa
serikali imekuwa ikigharamia gharama kubwa kuhakikisha wananchi wanapata umeme
kwa kulipia kiasi cha shilingi 27000 tu kwa kila nyumba ambayo inahitaji
nishati hiyo kwa matumizi ya kimaendeleo.
Ndamenya alisema kuwa umeme wa REA
umekuwa na awamu tatu tofauti ambazo kwa kifupi zimeleta maendeleo makubwa ya
kiuchumi kwa wananchi.
Mkuu wa wilaya Iringa Richard Kasesera
alisema kuwa wananchi wanatakiwa kutambua umuhimu wa kufanya kazi kwa bidii
katika kukuza pato lao ndani ya kaya ikiwa ni pamoja na kujali afya zao kwa
kujiunga na bima ya afya ili waweze kutibiwa kwa ufasaha.
Hata hivyo, baadhi ya wananchi wa tarafa
Kiponzelo walitoa changamoto zao, ikiwa ni pamoja na ubovu wa barabara,
wawekezaji kutojali maslahi ya vijiji, uhaba wa madawa kwenye vituo vya afya,
na changamoto ya ardhi kupewa wawekezaji bila ridhaa ya mikutano ya vijiji.
0 comments:
Post a Comment