Na Bahati Mollel,TAA
TIMU za michezo
mbalimbali za Uchukuzi SC zimeiva kutokana na mazoezi zinazofanya kwenye
viwanja vya shule ya sekondari ya Airwing, kwa ajili ya mashindano ya Kombe la
Mei Mosi yatakayoanza Aprili 17 hadi Mei 1 kwenye viwanja mbalimbali Jijini
Arusha,
Kocha Mkuu wa timu ya
soka, Zeno Mputa amesema wachezaji wake wameiva na wapo tayari kwa mashindano
ya Mei Mosi, kutokana na kuripoti kwa wingi na kufanya mazoezi kwa bidii.
Mputa amesema amewapima
wachezaji wake kwa kuwapa mazoezi magumu kwa siku tatu mfululizo, lakini wote
waliweza kufika kwenye mazoezi kwa siku zilizofuata.
“Yale mazoezi magumu ni
kama copper test na nilifanya hivyo nikiwa na lengo la kupima utimilifu wa
mwili, na wamefuzu wote kutokana na kuendelea na mazoezi, siku zilivyofuata
tofauti na awali nilidhani watakuwa wamechoka na kushindwa kufanya mazoezi
tena,” amesema Mputa.
Hata hivyo, anasema
tayari wameshacheza mechi moja ya kirafiki na timu ya Kipunguni na kutoa sare
ya bao 1-1, lakini wanategemea mechi nyingine mbili zitakazochezwa baadaye wiki
hii ili kujiweka imara zaidi.
Naye kocha wa timu ya
kamba kwa wanawake na wanaume, Abunu Issa amesema wachezaji wake wamekuwa
wakiripoti mazoezi kila siku na kufanya mazoezi makali, ikiwemo kuvuta kamba
wenyewe kwa wenyewe.
“Timu zangu hizi
zimekuwa zikijituma hivyo naamini pia tutafanya vizuri katika mashindano, kwani
nimekuwa nikiwapima kila baada ya mazoezi kwa wanawake kuvutana na wanaume na
kiwango chao ni kizuri,” amesema Abunu.
Kwa upande wa riadha,
Kocha wake Kingsley Marwilo amejihakikishia wachezaji wake kufanya vyema
kutokana na mazoezi wanayofanya, yakiwemo ya kujijengea misuli ikiwa ni kufanya
mazoezi na wachezaji wa soka.
Timu ya netiboli,
inayofundishwa na Kocha Judith Ilunda nayo imeendelea na mazoezi kwenye viwanja
vya Bandari Kurasini, ambapo sasa wanacheza na timu za Zanzibar zinazoshiriki
tamasha la Pasaka linalofanyika kwa kupokezana na Tanzania Bara.
Uchukuzi SC ndio
mabingwa watetezi kwenye michezo ya kuvuta kamba kwa wanaume na wanawake,
wakati kwa netiboli walitwaa ushindi wa pili sawa na karata, bao, draft na
baiskeli wanawake, huku katika soka
walishika nafai ya tatu.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment