Waziri
wa Viwanda na Biashara Mhe. Innocent Bashungwa (kushoto) akimsikiliza
Mkurugenzi wa Mahusiano kutoka kampuni ya Sigara Tanzania (TCC) Bw.
Godson Killiza aliyefika Ofisi ndogo za Wizara Dar es salaam kwa
mazungumo.Waziri
wa Viwanda na Biashara Mhe. Innocent Bashungwa (kulia) akiagana na Bw.
Godson Killiza Mkurugenzi wa mahusiano wa kampuni ya Sigara Tanzania
(TCC) aliyefika Ofisi ndogo za Wizara Dar es salaam kwa mazungumoWaziri
wa Viwanda na Biashara Mhe. Innocent Bashungwa wa tatu (kulia) akiwa
katika picha ya pamoja na wawakilishi kutoka TCC na Watumishi wa Wizara
ya Viwanda na Biashara.
……………..
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.
Innocent Bashungwa amesema Serikali itatafuta wanunuzi wa zao la Tumbaku
endapo Kamapuni iliyokuwa inanunua awali ya TLTC haitaendelea na
ununuzi huo.
Amesema kuwa tayari Kampuni ya GTI imekubali kushirikiana na Serikali kununua zao hilo kutoka kwa wakulima msimu ujao.
Mhe. Bashungwa ameyasema hayo leo
alipokutana na wawakilishi wa Kampuni ya Sigara Tanzania (TCC) ambapo
aliahidi kufanya mazungumzo na Waziri wa Kilimo kwa lengo la
kujadiliana namna ya kupata kampuni itakayoweza kununua zao la tumbaku
kutoka kwa wakulima.
‘’Tutazungumza na kampuni ya awali
iliyokuwa ikinunua tumbaku kama watakubali kuendelea kununua zao hilo au
kama hawawezi basi serikali itatafuta wanunuzi wengine watakaonunua zao
hilo kwa wakulima msimu ujao,’’ alisisitiza.
Aliongeza kuwa wadau wengi wameipongeza
serikali kwa kuwa na bajeti rafiki iliyosikiliza wadau wa viwanda na
biashara kuhusu masuala ya tozo na kodi mbalimbali.
Bashungwa alisema Serikali itaendelea
kuondoa vikwazo vilivyokuwepo kwenye sekta ya biashara kwa lengo la
kuleta unafuu na kukuza biashara, ajira na mazingira rafiki kwa
wafanyabiashara wa sekta binafsi.
Naye, Mkurugenzi wa Mahusiano Godson
Killiza kutoka TCC alisema kitendo cha serikali kupunguza kodi ya bidhaa
mbalimbali ni jambo linaloleta faida kwa wafanyabiashara watanzania
kutumia malighafi za ndani kuzalisha bidhaa.
Alisema bajeti ya serikali ya 2019/2020
italeta faida katika ukuaji wa uchumi, kukuza biashara na kupunguza
gharama za uzalishaji kwa kampuni nyingi.
Killiza alisema ongezeko la Kodi ya
Ongezeko la Thamani (VAT) kwa asilimia nane katika biashara yao
imesaidia kuongeza ulipaji wa kodi kutoka Sh bilioni 227 mwaka 2017 hadi
Sh bilioni 234 mwaka jana.
0 comments:
Post a Comment