Waziri wa Nchi – Ofisi
ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki (Mb) akitoa neno la
ufunguzi wakati wa mkutano wake na wawekezaji kutoka Marekani waliopo
nchini alipokutana nao 17 Juni, 2019 katika Ukumbi wa Mikutano wa Hyatt
Jijini Dar es Salaam ili kujadili masuala ya uwekezaji nchini.
Mkurugenzi Mtendaji wa
Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Bw. Geoffrey Mwambe akiwasilisha
mada ya masuala ya Uwekezaji nchini wakati wa kongamano hilo.
Waziri wa Nchi – Ofisi
ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki (katikati mwenye
kitenge cha kijani) pamoja na Kaimu Balozi wa Marekani Nchini Dkt. Inmi
Patterson (mwenye koti jeupe) wakifuatilia uwasilishwaji wa mada wakati
wa kongamano hilo.
Waziri wa Nchi – Ofisi
ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki (mb) akizungumza na
Kaimu Balozi wa Marekani Nchini Dkt. Inmi Patterson mara baada ya
kuwasili katika ukumbi wa Mikutano wa Hyatt Jijini Dar es Salaam
walipokutana kujadili masuala ya uwekezaji nchini wa kwanza kushoto ni
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof.
Palamagamba Kabudi.
Waziri wa Nchi – Ofisi
ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki (Mb) akizungumza na
waandishi wa habari masuala ua uwekezaji walipokutana nao wakati wa
kongamano la kujadili masuala hayo kwa wawekezaji wa Kimarekani, kulia
kwake ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe.
Prof. Palamagamba Kabudi.na kushoto kwake ni Kaimu Balozi wa Marekani
Nchini Dkt. Inmi Patterson.
………………………
NA.MWANDISHI WETU
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu
anayeshughulikia masuala ya Uwekezaji Mhe. Angellah Kairuki
amewahakikishia wawekezaji kutoka Marekani uwepo wa mazingira rafiki ya
uwekezaji nchini kwa kuzingatia mchango wao katika masuala ya uwekezaji.
Ametoa kauli hiyo wakati akifungua
kongamano la siku moja la kujadili masuala ya kuboresha mazingira ya
biashara pamoja na uwekezaji nchini lililofanyika tarehe 17 Juni, 2019
katika Ukumbi wa mikutano wa Hyatt Jijini Dar es Salaam.
Mazungumzo hayo yaliyolenga kujadili
changamoto zinazowakabili na kujadili namna bora ya kukabiliana nazo na
hatua mahsusi ambazo Serikali imeendelea kuzichukua ili kuboresha
mazingira ya biashara na uwekezaji.
Kongamano hilo limeandaliwa na Ubalozi wa
Marekani kwa kushirikiana na Chemba ya Wafanyabiashara wa Kimarekani
nchini Tanzania na kuhusisha wawakilishi wa Kampuni 47 kati ya 238 za
Kimarekani na kuhudhuriwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki Mhe. Profesa Palamagamba Kabudi, Maafisa Waandamizi wa
Serikali ya Tanzania, Wawakilishi wa Ubalozi wa Marekani pamoja na
Wanachama wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Kimarekani.
Waziri Kairuki alieeleza nia ya Serikali
ni kuendelea kuwa na mazingira wezeshi yanayowavutia wawekezaji nchini
katika kuendelea kuchangamkia fursa zilizopo na kupokea maoni yao ili
kutatua changamoto wanazokumbana nazo.
“Serikali itaendelea kuweka mkazo mkubwa
wa maboresho katika maeneo mbalimbali yatakayo kuvutia wawekezaji
ikiwani pamoja na uboreshwaji wa sekta ya mawasilino, miundombiu ya
barabara na usafirishaji ili kuwa na mazingira mazuri ya wawekezaji kuja
kuwekeza nchini,”alisema Waziri Kairuki.
Aliongeza kuwa ifikapo mwezi Julai mwaka
huu, serikali itaanza kutekeleza Mpango Kazi wa Uboreshaji wa Mazingira
ya Biashara na Uwekezaji ambao tayari umefanyiwa maboresho na
utekelezaji wake utaanza mapema mwaka ujao wa fedha wa 2019/ 2020.
Aidha waziri aliahidi kuendelea kusimamia
maeneo muhimu ikiwemo ushiriki wa sekta binafsi katika maeneo ya
uwekezaji na kueleza maboresho haya yatatekeleza hasa katika kuboresha
mifumo na kuwa na maziringa mazuri yanayotabirika kwa wawekezaji.
“Kwa kutambua umuhimu wa Sekta binafsi,
tutaendelea kusimamia ushiriki wao kikamilifu ili kuleta tija pasipo
kubagua sekta hiyo na kuendelea kuwa na mifumo inayotabirika kwa ajili
ya wawekezaji.
Naye Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi alifafanua
kuwa, jitihada za Serikali ni kuhakikisha kunakuwa na mahusiano mazuri
ya kidiplomasia baina ya nchi hizo mbili kwa kuzingatia zote
zinategemeana katika masuala hayo ya uwekezaji.
“Kimsingi tunapaswa kuwa na uelewa wa
pamoja kuwa, Tanzania na Marekani zinategemeana katika masuala haya ya
uwekezaji kwani mnatuhijai na sisi tunawahitaji hivyo lazima tukae meza
moja na kuyajenga endapo tunaona kuna maeneo ya kuboresha yenye tija ya
kuendeleza mahusiano mazuri yaliyopo ni vyema tukayafanyia kazi pamoja”,
Alisistiza Profesa Kabudi.
Kwa upande wake Kaimu Balozi wa Marekani
nchini Dkt. Inmi Patterson katika hotuba yake ya ufunguzi alieleza kuwa,
majadiliano hayo ni mwanzo mzuri wa kuendelea kutekeleza mabadiliko ya
kisera yatakayosaidia kuongeza uwazi na mazingira rafiki ya ufanyaji wa
biashara nchini.
“Majadiliano ya leo ni mwanzo wa
utekelezaji wa mabadiliko ya kisera yatakayoongeza uwazi na kuboresha
mazingira ya kufanya biashara na tunaunga mkono jitihada hizi za
Serikali ya Tanzania kwa kuzingatia mahusiano mazuri yaliyopo
sasa,”Alieleza Kaimu Balozi Patterson.
Aliongezea kuwa Serikali ya Marekani
itaendelea kuunga mkono ushiriki wa sekta binafsi katika jitihada za
maendeleo nchini humo kupitia ubia kati ya sekta binafsi na sekta ya
umma (Public private partnerships) ambao utaimarisha mazingira ya
kibiashara na ubunifu ambao utanufaisha Wananchi wa Tanzania.
Aidha alieleza kuwa nchi yake imeendelea
kuwa mstari wa mbele katika uwekezaji, kwa kuzingatia Takwimu za Kituo
cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Wafanyabiashara wa Kimarekani wamewekeza
zaidi ya Dola za Kimarekani bilioni 4.7 nchini Tanzania na kuzalisha
takriban nafasi za ajira 52,000 katika kipindi cha miaka 28 nchini kote
Tanzania.
0 comments:
Post a Comment