Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akiwakabidhi vitendea kazi baadhi ya Wajumbe wa Bodi aliyoizindua leo wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Bodi hiyo iliyofanyika Hospitali ya Mirembe Mkoani Dodoma 08/02/2017.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Hospitali ya Mirembe kwenye hafla ya Uzinduzi wa Bodi hiyo iliyofanyika Hospitali ya Mirembe Mkoani Dodoma 08/02/2017. PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-WHUSM
Na. Benedict Liwenga-WHUSM.
SERIKALI imesema kwamba tatizo la
maradhi yasiyoambukiza yakiwemo magonjwa ya akili yamekuwa yakiongezeka
siku hadi siku huku vyanzo vyake vikiwa ni pamoja na urithi, matumizi ya
madawa ya kulevya, pombe, matatizo ya kisaikolojia pamoja na hali ngumu
ya maisha.
Kauli hiyo imetolewa leo mjini Dodoma na
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy
Mwalimu wakati alipokuwa akizindua Bodi ya Hospitali ya Mrembe Mkoani
hapo.
Akiongea na mbele ya Watendaji wa Bodi
hiyo, wageni waalikwa pamoja na Viongozi wa hospitalini hapo, Waziri
Ummy amesema kuwa, kundi lililoathirika Zaidi na kdhai hiyo ni vijana
ambao ni nguvu kazi ya Taifa, ambapo alitaja taarifa ya Shirikala Afya
Ulimwenguni (WHO) ya mwaka 2016n inayoonyesha takribani watu milioni
15.3 Duniani wanapata matatizo ya kiafya yatokanayo na matumizi ya dawa
za kulevya pamoja na matumizi ya pombe kupita kiasi.
“Matatizo haya yamekuwa yakisababisha
vifo milioni 3.3 kila mwaka Duniani kote, hata hivyo taarifa ya Wizata
yangu inaonyesha kwamba idadi ya watu wanaougua magonjwa ya akili
inaongezeka kwa kasi kubwa kutoka wagonjwa 136,710 mwaka 2011/2012 hado
wagonjwa 448,997 mwaka 2015/2016”, alisema Ummy.
Ameongeza kuwa, takwimu za hospitali ya
Mirembe zinaonyesha kuwa, katika kipindi cha miaka mine kuanzia mwaka
2012 hadi 2016, jumla ya wagonjwa Zaidi ya 60,000 wenye magonjwa ya
akili na waathirika wa dawa za kulevya walipatiwa huduma za afya na
utengamao.
Aidha, kwa kutambua majukumu makubwa ya
hospitali hiyo na kutatua changamoto zinazohusiana na magonjwa hayo,
Serikali imeamua kuunda Bodi ya hospitalini hapo lengo likiwa ni
kutekeleza dhana ya Utawala Bora na Utoaji wa Huduma Bora za Afya ya
Akili kwa mujibu wa mapango mkakati na sera za nchi.
“Ninayo furaja leo kushiriki nanyi
katika uzinduzi wa Bodi hii ya Hospitali ya Afya ya Akili Mirembe, na
bodi hii itaongozwa na Mwenyekiti pamoja na Wajumbe waliouteuliwa kutoka
maeneo mbaimbali ya kiujuzi hapa nchini”, alisema Waziri Ummy.
Amesema kuwa, bodi hiyo itakuwa na
majukumu mbalimbali yakiwemo kusimamia utendaji wa hospitali hiyo na
Taasisi ya Isanga, kuhakikisha kuwa Sheria ya uanzishwaji wa hospitali
inapatikana kwa wakati, kushauri kuhusu muundo wa hospitali, kuunda
kamati ndogo ndogo, kushauri kuhusu mpango wa muda mrefu ili kuboresha
huduma pamoja na kushauri jinsi ya kupunguza gharama za uendeshaji
hospitalini hapo.
Sambamba na kuzindua bodi hiyo, Waziri
Ummy ameitaka jamii kushirikiana na Serikali katika kupiga vita matumizi
ya madawa ya kulevya hususan kwa vijana ili nguvu kazi ya Taifa isizidi
kupotea.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi hiyo,
Profesa Gadi Kilonzo amempongeza Waziri Ummy na kwa kuzindua bodi hiyo
na amemuhakikishia kuwa bodi hiyo itatekeleza maagizo yote pamoja na
majukumu iliyopewa ili kuboresha utendaji kazi hospitakini hapo.
“Dhama uliyotupa sisi Wajumbe wa Bodi ni
kubwa, tunaieheshimu sana na pia nakuahidi kuwa, tutatekeleza kwa bidii
majukumu yote ya kuisimamia hospitali hii, tutajitahidi kwa uwezo wetu
wote kutatua changamoto za hospitali hii kwa kushirikiana na wadau
wengine wa afya kupitia Wizara yako, pia tunashukuru kwa vifaa vya kazi
ulivyotupatia kwa ajili ya kutumia wakati wa utendaji wetu”, alisem
Kilonzo.
Wajumbe waliochaguliwa kuunda bodi hiyo
ni Profesa Gadi Kilonzo ambaye ndio Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Dkt.
Erasmus Mndeme ambaye ni Katibu wa Bodi na Mganga Mkuu wa Hospitali ya
Mirembe, Dkt. Mpona Boniventura ambaye ni Mwakilishi kutoka chuo Kikuu
cha Dodoma, Profesa Joseph Mbatia, Ndugu John Sipendi, Ndugu Ernest
Kabohola, Ndugu Jane Magembe pamoja na Ndugu Clavery Lyela.
0 comments:
Post a Comment