Jumla
ya watu 168 wamenusurika na ajali ya Treni iliyotokea mkoani Dodoma
katika maeneo ya level cross ya hazina katika halamshauri ya jiji la
Dodoma.
Ajali
hiyo imehusisha Gari lenye no za usajili T 860 APW aina ya isuzu
likiendeshwa na Dereva Hamis Salamu (49) mkazi wa Nkuhungu ambapo
gari hilo liligonga Treni ya abiria No, Y 12,ikiendeshwa na Michael
Mdachi (44) mkazi wa kisasa Jijini hapa na Guard Abdala Ngola (59)
ambaye ni mkazi wa Area c Dodoma.
Akizungumza
katika eneo la tukio, Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma Gilles Muroto
amesema Treni hiyo ilikuwa ikitokea kigoma ,mwanza na mpanda kuelekea
Dar es salaam ikiwa na behewa 9 za daraja tatu mbili za daraja
kwanza,Behewa la mgahawa moja,Behea la vifurushi moja na Behea la Breki
Moja na kusababisha majeruhi kwa abiria 32 waliokuwa kwenye Behewa namba
3648 na 3607 ambayo yalianguka.
”Mnamo tarehe 17a ya 11/06/2019 majira ya
saa 11:25 usiku ilianza safari kutoka Tabora kuelekea Dar es Salaam
ikiwa na mabehewa 14 kama yalivyotajwa hapo juu na ilipofika maeneo ya
kuvuka makutano ya Reli na kugongwa na gari”amesema Muroto
Muroto amesema kuwa chanzo cha ajali hiyo
ni uzembe wa dereva wa gari kutochukua tahadhari alipokuwa akivuka
makutano ya Reli na barabara hivyo gari kuzima likiwa katikati ya Reli
na Dereva wa gari aliruka na kukimbilia Polisi Kujisalimisha
Aidha, kamanda muroto ameongeza kuwa hali ya abiria waliopata ajali hiyo kati ya abiria 32 watatu hali sio za kuridhisha.
Kwa
upande wake mkuu wa wilaya ya Dodoma mjini Patrobasi katambi ameliomba
jeshi la polisi kuendelea kufanya uchunguzi wa kina ili kujua chanzo
cha ajali hiyo.
0 comments:
Post a Comment