MISRI na Nigeria zimefungua milango ya
hatua ya 16 Bora ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2019
baada ya ushindi dhidi ya wapinzani wao Jumatano usiku.
Nigeria ‘Super Eagles’ ilikuwa ya kwanza kutinga hatua ya mtoano baada
ya kuichapa 1-0 Guinea bao pekee la beki wa Leganes ya Hispania, Kenneth
Josiah Omeruo dakika ya 73 Uwanja wa Alexandria nchini Misri katika
mchezo wa Kundi B.
Maana yake, timu ya kocha Mjerumani mwenye umri wa miaka 65, Gernot Rohr
inafikisha pointi sita katika mchezo wa pili ikiendelea kuongoza Kundi B
mbele ya Madagascar na Guinea zenye pointi moja kila moja, wakati
Burundi haina pointi.
Nayo Misri ikaichapa Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo (DRC) 2-0, mabao ya Ahmed El Mohamady dakika ya 25
na Mohamed Salah dakika ya 43 katika mchezo wa Kundi A Uwanja wa
Kimataifa wa Cairo.
Mafarao sasa wana pointi sita baada ya mechi mbili, wakiendelea kuongoza
Kundi A wakifuatiwa na Uganda wenye pointi nne baada ya sare ya 1-1 na
Zimbabwe leo, wakati DRC inashika mkia ikiwa haina na pointi na
imekwishatolewa.
Mshambuliaji wa Simba SC ya Tanzania, Emmanuel Okwi alianza kuwafungia
Uganda dakika ya 12, kabla ya kiungo wa Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini,
K. Billiat kuwasawazishia Zimbabwe dakika ya 40.
Uganda sasa itahitaji hata sare kwenye mchezo wake wa mwisho dhidi ya Misri ili kwenda hatua ya mtoano iipiku Zimbabwe.
MICHUANO hiyo itaendelea Alhamisi kwa mechi tatu, Kundi C Madagascar
itamenyana na Burundi kuanzia Saa 11:3 jioni mchezo wa Kundi B Uwanja
wa 11:30 jioni.
Mchezo huo utafuatiwa ne mechi mbili za Kundi C, kwanza Senegal na
Algeria Saa 20:00 usiku na baadate Saa 5:00 usiku Uwanja wa Juni 30
mjini Cairo.
0 comments:
Post a Comment