Mkurugenzi
wa Masoko wa MeTL Group, Fatema Dewji-Jaffer akielezea kampeni ya
USIKATE TAMAA na jinsi inavyoweza kubadili maisha ya watu waliokata
tamaa ya kufanikiwa kimaisha.kulia na Kaimu Meneja Masoko Msaidiz wa
Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL Group), Zainul Mzige.
Mkurugenzi
wa Masoko wa MeTL Group, Fatema Dewji-Jaffer akizungumza kuhusu kampeni
ya USIKATE TAMAA, Kushoto ni mwanamuziki Shetta na kulia na Kaimu
Meneja Masoko Msaidizi wa Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL
Group), Zainul Mzige.
Mwanamuziki,
Nurdin Bilal Ali maarufu kama Shetta akielezea safari yake ya muziki
hadi kufika hatua aliyopo sasa ambayo mwenyewe amesema kuwa kwake ni
mafanikio makubwa. Katikati ni Mkurugenzi wa Masoko wa MeTL Group,
Fatema Dewji-Jaffer. kulia na Kaimu Meneja Masoko Msaidizi wa Mohammed
Enterprises Tanzania Limited (MeTL Group), Zainul Mzige.
Mkurugenzi
wa Masoko wa MeTL Group, Fatema Dewji-Jaffer akifafanua jambo katika
mkutano na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
wa Masoko wa MeTL Group, Fatema Dewji-Jaffer akiwa katika picha ya
pamoja na Mwanamuziki, Nurdin Bilal Ali maarufu kama Shetta, kuashiria
kuwa kampeni ya USIKATE TAMAA imezinduliwa rasmi.
Na Modewjiblog
Kwa
kutambua hali ambayo inawakuta watu wengi katika jamii na kupoteza
matumaini ya kufanikiwa kimaisha, kampuni ya Mohammed Enterprises
Tanzania Limited (MeTL Group) imefanya uzinduzi wa kampeni ambayo
imepewa jina la USIKATE TAMAA ikiwa na lengo la kuhamasisha watu
waliokata tamaa kuwa nao wana nafasi ya kufanikiwa.
Akizungumzia
kampeni hiyo, Mkurugenzi wa Masoko wa MeTL Group, Fatema Dewji-Jaffer
alisema kuwa kampeni hiyo inalenga kuleta matumaini mapya katika jamii
kwa watu ambao wamekuwa wakipoteza matumaini kutokana na hali ya ugumu
wa kimaisha ambayo imekuwa ikiwakabili.
Alisema
kampeni hiyo itakuwa ikitumia watu mbalimbali ambao wamefanikiwa na
watakuwa wakitoa historia zao katika maeneo mbalimbali ambayo
watatembelea, wakielezea jinsi walivyokuwa na maisha magumu hapo awali
na sasa wamefanikiwa kimaisha.
“Kuna
watu hawana uwezo na wanazungukwa na watu ambao wamekuwa wakiwaambia
kuwa hawawezi kufanikiwa lakini kupitia kampeni ya USIKATE TAMAA
wataweza kupata matumaini kutoka kwa watu ambao walipita katika maisha
magumu na baadae wakafanya vyema,” alisema Fatema.
Mkurugenzi
wa masoko huyo aliongeza kuwa kampuni ya MeTL pamoja na kufanya
biashara lakini pia inaijali jamii na inapenda kuona watu wakifanikiwa
kimaisha hivyo kupitia kampeni ya USIKATE TAMAA itaweza kusaidia watu wa
aina mbalimbali waliopo katika jamii ya kitanzania wakipata matumaini
mapya na kuongeza juhudi ili wafanikiwe.
“MeTL
kupitia chapa yake ya MO inataka kuona watu wakiendelea kupambana na
kufanikiwa, tunataka watu wafanikiwe na tuwape tuzo, tuwape sauti ya
kusikika na huu ni mwanzo tu, kampeni hii itafanyika kwa muda mrefu
zaidi,” alisema Fatema.
Kwa
upande wa mwanamuziki, Nurdin Bilal Ali (Shetta) ambaye ametumika kama
mmoja wa watu ambao wamefanikiwa, alielezea safari yake ya kimuziki na
kusema kuwa awali alikuwa akiishi kwa moja ya wasanii wa muziki nchini
na alikuwa akifanya kazi za nyumbani kwa mtu huyo lakini akiwa na nia ya
kutafuta njia ya kutoka kimuziki na juhudi alizozionyesha zimemwezesha
kuwa moja ya wasanii waliofanikiwa nchini.
“Unaweza
kuwa unajiamini katika kipaji chako lakini bado watu wanakudharau, mimi
nimewahi kuishi na mwanamuziki mkubwa nchini lakini najijua nina kipaji
lakini kwakuwa nilikuwa natafuta njia ya kutoka kimuziki ilinibidi
nifanye hivyo,
“Ilikuwa
naosha gari lake, naosha vyombo na hata kumwogesha mdogo wake lakini
nilikuwa najua nini nafanya na nini nataka, msanii yule alikuwa
anafahamiana na watu wengi na mimi ikanisaidia kupata njia ya kutokea na
leo kwa hatua niliyofikia nimefanikiwa,” alisema Shetta.
0 comments:
Post a Comment