Tumeamka na mabishano makali sana baada ya kunyukwa 2-0 na timu ya taifa ya SENEGAL “simba wa milima ya Teranga”
Kikubwa anatafutwa mbuzi wa kafara kwa kipigo hicho, wa kwanza anaetajwa
ni Emmanuel Amunike, kocha mkuu wa Taifa stars, Fei toto, Mwantika na
wengine kwamba hawa ndiyo sababu ya kufungwa kwetu.
Siku zote kwenye mpira zinapopambana timu mbili huangaliwa aliye bora yaani “favorite” na dhaifu yaani “under dog”, na hapo kinachoangaliwa zaidi ni takwimu za ubora na kiwango halisi kwa wakati husika.
Tumecheza na timu ambayo imeshacheza kombe la dunia angalau mara mbili
na moja ikifika robo fainali, imeshacheza AFCON angalau mara 12 kati ya
hizo iliweza kushika nafasi ya 4 mara 3, na nafasi ya 2 mara moja.
Kile kikosi kilichocheza thamani yake ya chini ni Euro milioni 231.5
huku kikiwa kimekusanya wachezaji kutoka mataifa 6 ya ulaya Italia,
Hispania, Ubelgiji, Ujerumani, England na Ufaransa.
Tukumbuke pia kwamba hili ni taifa namba 1 kwa ubora wa soka Afrika na namba 22 duniani.
Kwa mazingira haya unahitaji mbinu za mwalimu kidogo huku ukitegemea
zaidi jitihada zaidi za wachezaji ili kupunguza kipigo cha aibu.
Kama uliona rafu tulizocheza hatukucheza kwa makusudi bali tulilazimishwa kuzicheza kwa uzoefu wao.
Wasifu wa timu yenyewe ilivuruga saikolojia yetu, kumbuka pia misingi
yetu ya soka na “ABC” zake ilivyo mibovu, hebu tuwape HESHIMA Simba hawa
wa milima ya Teranga.
Hatukucheza vibaya ila tulilazimishwa kucheza vibaya, tatizo huwa
hatujifunzi na kufanya marekebisho ya mapungufu yetu, tukirudi
utashangaa tunaishi vile vile huku tukitegemea matokeo tofauti.
Kazi yetu kubwa ni kujenga misingi ya soka tuache kubahatisha #kila_la_heri_Stars
0 comments:
Post a Comment