Baadhi ya watoto walionaswa na
kamera ya BMG wakicheza katika korongo hatari la Bolelo lililopo Kata ya
Kumsenga, Halmashauri ya Mji wa Kasulu mkoani Kigoma ambapo korongo
hilo linaelezwa kuwa uwanja wa vitendo viovu ikiwemo ushirikina.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Pia
korongo la Bolelo licha ya kwamba ni hatari kwa jinsi lilivyo, bado
linapendwa na watoto wakiwemo wanafunzi wa shule za msingi zilizopo
jirani ambapo wamekuwa wakilitumia kwa kucheza/ kujificha wanapotoroka
shuleni.
Nyakati
za usiku inaelezwa korongo hili ni hatari kwa wakazi wanaokatisha hapa
kwani baadhi ya wahalifu hulitumia kufanya uhalifu kama vile ukabaji.
Mwalimu
Mkuu wa Shule ya Msingi Mwenge wilayani Kasulu, Mwl. John Edson
akieleza mbele ya wanahabari namna uwepo wa korongo la Bolelo jirani na
shule hiyo unavyoathiri masomo kwa wanafunzi ambao wamekuwa wakitoroka
na kwenda kujifisha humo.
Mkurugenzi
wa Shirika la Kutetea Haki za Watoto na Wanawake KIVULINI, Yassin Ally
(kushoto) akizungumza na Mkuu wa Shule ya Msingi Mwenge, Mwl. John Edson
kuhusiana na mathara ya korongo ya Bolelo kwa wanafunzi.
0 comments:
Post a Comment