Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akizungumza na Wakazi wa Kikwajuni Vijibweni wilaya ya Kigamboni alipokwenda kutatua mgogoro kati ya Mwekezaji Registered Trustees Korea Church Mission jijini Dar es Salaam jana.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akitembea kuelekea eneo lenye mgogoro kati ya Wananchi wa Mkwajuni Vijibweni wilaya ya Kigamboni maarufu kama kwa Mkorea na Mwekezaji wakati alipokwenda kutatua mgogoro katika eneo hilo jana.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akimsikiliza mwananchi wa Mkwajuni Vijibweni Mariam Kange alipokwenda kuatatua mgogoro wa ardhi baina ya wananchi wa eneo hilo maarufu kwa Mkorea na Mwekezaji Registered Trustees Korea Church Mission (PICHA NA WIZARA YA ARDHI)
Na Munir
Shemweta
Waziri
wa Adhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William lukuvi amewaonya wenyeviti wa
Serikali za Mitaa kutojihusisha na masuala ya uuzaji ardhi katika maeneo
mbalimbali kwa kuwa hapaswi kisheria kufanya kazi hiyo.
Lukuvi
alitoa onyo hilo jana wakati alipokwenda kusuluhisha mgogoro wa ardhi kati ya
wananchi wa Kikwajuni Vijibweni maarufu kama kwa Mkorea wilayani Kigamboni mkoa
wa Dar es Salaam na Mwekezaji ‘Registered Trustee of Korea Church
Mission’ katika eneo hilo la ukubwa wa ekari 305.
Lukuvi
alisema sheria ya ardhi haisemi kama wenyeviti wa mitaa wanaruhusiwa kusimamia
uuzaji ardhi na kusisitiza kuwa wenyeviti hao hawana mamlaka ya kufanya hivyo
na mwenye jukumu la kusimamia masuala ya ardhi katika miji ni halmashauri za
mji au Manispaa.
Waziri
wa Ardhi alisema mtu yeyote atakayeuziwa ardhi kupitia wenyeviti hao wa mitaa
au mtu mwingine asiyetambuliwa kisheria basi atakuwa ameuziwa ‘bomu’ na
kuwataka wananchi kuwa makini na suala hilo na kuwashauri kabla ya kununua eneo
lolote ni vyema wakaiuliza mamlaka husika iwapo eneo husika limepangwa kwa
matumizi ya aina gani ili kuepuka kubomolewa.
‘’Ukitaka
kununua kiwanja kwanza kaulize Manispaa maana unaweza kununua eneo kumbe ni la
kuzikia kwani manispaa ndiyo inayojua kama eneo hilo ni salama’’ alisema Lukuvi
Katika hatua nyingine, Waziri Lukuvi ametoa siku
kumi kwa halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni jijini Dar es Salaam kufanya
uhakiki kwa wananchi wote wanaoishi eneo lenye mgogoro na Mwekezaji la
Kikwajuni Vijibweni Kigamboni maarufu kwa Mkorea ili kupata taarifa sahihi za
wananchi hao.
Aidha,
amemtaka Kamishna Msaidizi wa Ardhi Kanda ya Dar es Salaam Methew Mhonge kupata
nakala ya hukumu ya kesi ya wananchi hao dhidi ya Mwekezaji ‘Registered
Trustees Korea Church Mission’ inayoonesha kuwa wananchi wa eneo hilo
wameshindwa kesi na wanatakiwa kuondoka.
Maagizo
hayo ya Lukuvi yanafuatia kuelezwa na wananchi 22 wa Kikwajuni kupitia
mwakilishi wao Meja Mstaafu Peter Ismail kuwa haki haikutendeka wakati wa zoezi
la ulipaji fidia kwa wananchi wa eneo hilo jambo lililosababisha kukataa
kuchukua fidia na wengine 6 kudai nyongeza ya fidia huku wananchi 95
wakilalamika.
Meja
Mstaafu Ismail alisema, wao walichukua uamuzi wa kutokubaliana na mwekezaji
aliyetaka kuwafidia laki nne kwa ekari moja wakati wao walitaka kulipwa shilingi
milioni moja kwa ekari moja na kufafanua kuwa kilichowashangaza ni Mwekezaji
kulipa fidia mwaka 2015 wakati zoezi hilo lilitakiwa kufanyika miezi sita baada
ya Agosti 2004.
Kwa
upande wa wananchi sita wanaotaka kuongezewa fidia wananchi hao kupitia
mwakilishi wao Hamza Rashid walidai kesi yao iliamuliwa kupatiwa taarifa halisi
ya uthamni na siyo nakala kama walivyofanyiwa jambo walilolieleza kuwa
halikufanyika.
Kufuatia
hali hiyo, Waziri Lukuvi aliagiza taarifa zote muhimu zipatikane kipindi cha siku
kumi ikiwemo Mwekezaji kuwasilisha mpango wa jinsi atakavyolitumia eneo hilo la
ekari 305 sambamba na chanzo cha mtaji wa uwekezaji huo.
Eneo
la Kikwajuni Vijibweni maarufu kwa Mkorea kwa muda mrefu tangu mwaka 2004
limekuwa na mgogoro wa ardhi kati ya wananchi wa eneo hilo na Mwekezaji
‘Registered Trustees Korea Church Mission’ anayetaka kujenga chuo Kikuu.
------------------------------ -----------MWISHO------------- ------------------------
0 comments:
Post a Comment