Naibu meya wa manispaa ya Iringa Joseph Lyata akiwa kiwandani hapo na kupiga
marufuku kwa shule zote za manispaa ya Iringa kununua chaki kutoka nje ya
kiwanda Dustless Smart Chalk kilichopo manispaa ya Iringa kwa kuwa kiwanda
hicho kinatengeneza chaki zilizo bora
Naibu meya wa manispaa ya Iringa Joseph Lyata akiandika kwa kutumia chaki zinazotengenezwa na
kiwanda Dustless Smart Chalk kilichopo manispaa ya Iringa kinachotengeneza chaki zilizo bora
Naibu meya wa manispaa ya Iringa Joseph Lyata akipata maelezo ya jinsi gani chaki hizo zinavyotengenezwa katika kiwanda Dustless Smart Chalk kilichopo manispaa ya Iringa
Hizi ni baadhi ya chaki zinazotengenezwa katika kiwanda Dustless Smart Chalk kilichopo manispaa ya Iringa
NA FREDY MGUNDA,IRINGA.
NAIBU meya wa manispaa ya
Iringa Joseph Lyata amepiga marufuku kwa shule zote za manispaa ya Iringa
kununua chaki kutoka nje ya kiwanda Dustless Smart Chalk kilichopo manispaa ya
Iringa kwa kuwa kiwanda hicho kinatengeneza chaki zilizo bora na zinazofaa
kutumiwa katika shule zote.
Akizungumza na blog Naibu
meya,alisema kuwa kiwanda cha chaki kilichopo katika manispaa ya Iringa
kinatengeneza chaki zilizo na kiwango bora cha kutumiwa na walimu wakati wa
kufundisha ili kuinua uchumi wa kiwanda hicho.
“Mimi nimekuwa mwalimu kwa
takribani miaka nane katika shule mbalimbali na nimefundisha na kuandikia chaki
kutoka katika kampuni mbalimbali ila hizi chaki ambazo zinatengemezwa hapa
manispaa ya Iringa zinaviwango vinavyotakiwa” alisema Lyata
Lyata alisema kuwa haiwezekani
kunakiwanda cha kutengeneza chaki lakini walimu wanatumia chaki kutoka nje ya
manispaa ya Iringa kutasababisha kuua mitaji na viwanda hivi vya vijana
wabunifu ambao wapo manispaa hapa.
“Tusipo waunga mkono vijana na
kiwanda hiki cha kutengeneza chaki tutakuwa tuaua uchumi wa wananchi wa
manispaa ya Iringa hivyo lazima walimu wa manispaa ya Iringa kuwaamuru kutumia
chaki zinazotengenezwa na kiwanda chetu kilichopo hapa manispaa ya Iringa”
alisema Lyata
Aidha Lyata aliwaomba wadau
mbalimbali kuendelea kuwasaidia vijana hao wenye kiwanda cha Dustless Smart Chalk
ambacho bado kinahitaji vitu vingi ili kuwa na kiwanga kikubwa zaidi na
kuongeza ajira kwa vijana wengine.
“Wadau naombe mjaribu
kuwatembelea wale vijana walipo pale Ipogolo SIDO kwa kuwa wanafanya kazi kubwa
na ubunifu mkubwa kwa lengo la kufanikiwa kuja kuwa na kiwanda kikubwa ambacho
kitasaidia kuongeza ajira kwa vijana wengine” alisema Lyata
Lyata alisema kuwa kiwanda cha Dustless
Smart Chalk kinakabiliwa na upungufu wa vifaa na vitendea kazi ambavyo
vinarudisha nyuma kazi zao hivyo wadau wanatakiwa kujitokeza na kuwasiadia
kununua vifaa pamoja kukiboresha kiwanda hicho kuwa cha kimataifa.
Lakini Lyata alimalizia kwa
kusema kuwa chaki hizo zinaubora wa kimataifa kwa kuwa hazina vumbi wala madhara
kwa binadamu yeyeto yule hivyo sasa ni muda muafaka kwa walimu kutumia chaki
hizo.
Awali akitoa taarifa kwa Naibu
meya mmoja wa wanakikundi wa kiwanda cha Dustless Smart Chalk Prisca Masalanga
alisema kuwa kiwanda hicho kinakabiliwa na changamoto mbalimbali hasa za vifaa
bora vya kuzalishia bidhaa hii ya chaki.
“Tunazalisha chaki zenye
kiwango bora lakini tunakumbana na uhaba wa vifaa vinavyopelekea kuanika chaki
hizi kwenye meza kwa kuwa hatuna sehemu sahihi ya kuanikia chaki hizi,bado
hatuna mashine kubwa bado tunatumia mashine ndogo” alisema Masalanga
Masalanga alisema kuwa
changamoto kubwa ambayo wanakumbana nao ni kukosa soko la kudumu la chaki
kutoka katika kiwanda hicho cha Dustless Smart Chalk ambacho kinauwezo wa
kuazalisha chaki zenye ubora unaotakiwa kufundishia mashuleni.
“Kwa kweli ndugu mwandishi
kiwanda chetu bado hatuna soko tunazalisha tu hizi chaki huku tukitafuta soko
na kuwaomba wadau kutusaidia kutafuta soko ili tuweze kuuza chaki hizi na
kukuza mitaji yetu na kuwa na kiwanda kikubwa ambacho kitaajili vijana wanzetu
wengi hapo baadae” alisema Masalanga
0 comments:
Post a Comment