Waziri wa Kilimo, Prof
Adolf Mkenda akizungumza mara baada ya kuzinduliwa Kituo Mahiri cha Usambazaji
Teknolojia za Kilimo kilichopo Nzuguni jijini Dodoma, leo, Septemba 24, 2021. (Picha
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Waziri wa Kilimo, Prof Adolf Mkenda (kulia) akimskiliza Mtaalam wa mazao ya Mtama, Ulezi na Uwele kutoka Dkt Robert Simbagige kutoka Taasisi ya Utafiti wa Kilimo (TARI), kituo cha Hombolo juu ya mbegu bora za zao la ulezi zinatengenezwa na kituo hicho mara baada ya uzinduzi wa Kituo Mahiri cha Usambazaji Teknolojia za Kilimo kilichopo Nzuguni jijini Dodoma, leo, Septemba 24, 2021
Waziri wa Kilimo, Prof Adolf Mkenda akikata utepe kuzindua Kituo Mahiri cha Usambazaji Teknolojia za Kilimo kilichopo Nzuguni, kilicho chini ya Taasisi ya Utafiti wa Kilimo (TARI) Jijini Dodoma leo, Septemba 24, 2021.
Sehemu ya Washiriki wakimsikiliza Waziri wa Kilimo, Prof Adolf Mkenda akisisitiza jambo kwa Watendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo (TARI) Nzuguni jijini Dodoma mara wakati akifungua kituo mahiri cha usambazaji teknolojia za kilimo, leo, Septemba 24., 2021.
Waziri wa Kilimo, Prof Adolf Mkenda akisisitiza jambo kwa Watendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo (TARI) juu ya mbegu za zao la ndizi wakati akiwa katika kitalu cha zao hilo katika Kituo Mahiri cha Usambazaji Teknolojia za Kilimo kilichopo Nzuguni jijini Dodoma mara baada ya kufungua kituo hicho, leo, Septemba 24, 2021.
Waziri wa Kilimo, Prof Adolf Mkenda akizungumza mara baada ya kuzinduliwa Kituo Mahiri cha Usambazaji Teknolojia za Kilimo kilichopo Nzuguni jijini Dodoma, leo, Septemba 24, 2021.
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma
Changamoto kubwa ya wakulima nchini ni pamoja na kutotumia mbinu
za kilimo bora kama vile kutotumia mbegu bora, kutozingatia nafasi kati ya mmea
na mmea, kutotumia mbolea kwa usahihi na matumizi hafifu ya viuatilifu.
Katika kukabiliana na changamoto hiyo serikali imeanzisha kituo
mahiri kitakachowasaidia wakulima kuongeza ufahamu wa kanuni za kilimo bora kwa
wadau hususani wakulima na kuongeza ushirikiano kati ya wakulima, wagani,
watafiti na wadau wa mbegu.
Waziri
wa Kilimo, Mhe Prof. Adolf Mkenda ameyasema hayo leo tarehe 24 Septemba 2021
wakati akizindua Kituo Mahiri cha Usambazaji Teknolojia za Kilimo kilichopo
Nzuguni, kilicho chini ya Taasisi ya Utafiti wa Kilimo (TARI) Jijini Dodoma.
Amesema kuwa kituo hicho kimeanzishwa muda muafaka wakati Wizara
ya Kilimo imeweka mkakati wa kuimarisha huduma za ugani nchini.
Waziri Mkenda ametoa rai kwa viongozi wa mikoa iliyo katika
kanda ya kati kukitumia kituo hicho kuwajengea uwezo kwa vitendo maafisa ugani
ili wasaidie kuwajengea uwezo wakulima katika maeneo yao ya kazi ili kuongeza
uzalishaji na tija, kuchangia kuwa na uhakika wa chakula, kipato, lishe bora na
ukuaji wa uchumi wa mtu mmoja mmoja, kaya na Taifa kwa ujumla.
Amesema kuwa kituo hicho mahiri cha kusambaza teknolojia za
kilimo kilichopo kwenye viwanja vya maonesho vya Nzuguni Jijini Dodoma kitatoa
mafunzo ya matumizi ya teknolojia za kilimo bora kama vile matumizi ya mbegu
bora, kupanda kwa nafasi pamoja na matumizi sahihi ya mbolea na viuatilifu.
Waziri Mkenda ameongeza kuwa "Matarajio yangu kituo hiki
kitakuwa chachu ya kuwaunganisha wadau wa kilimo na masoko, pia kuanzisha
kanzidata ya masoko ya mazao mbalimbali"
"Nawasihi viongozi wa Halmashauri zote kutoa fedha za
kutosha kwa ajili ya kuendesha shughuli za uhaulishaji/usambazaji wa teknolojia
bora za kilimo na kuimarisha huduma za ugani nchini" Amesisitiza Waziri
Mkenda
Kwa upande wake Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Dodoma Mhe Riziki
Lulida pamoja na kumpongeza waziri wa Kilimo lakini pia ameiomba serikali
kuhimiza mikakati ya uzalishaji wa alizeti kwa wingi kwa kutoa fedha za mikopo
kwa wanawake na hususani wakulima ili kuongeza tija na uzalishaji wa zao hilo.
Mhe Lulida amesema kuwa serikali imefanya kazi kubwa katika
kuwanufaisha wafanyakazi wa serikali na kutambulika hivyo inapaswa kuongeza
msisitizo wa kuwapatia vitendea kazi na kuwatambua maafisa ugani kutokana na
kazi kubwa na nzuri wanayoifanya kwa manufaa ya wakulima wote nchini.
Awali, akitoa taarifa ya Taasisi ya Utafiti wa Kilimo nchini-
TARI Mkurugenzi Mkuu wa taasisi hiyo Dkt Geofrey Mkamilo amesema kuwa njia
pekee ya wakulima kuongeza kipato ni pamoja na kuzingatia taratibu zote za
kilimo ikiwemo kupata mafunzo ya kilimo yanayotolewa katika vituo 17 vya
utafiti wa kilimo vilivyopo nchini.
Amesema kuwa TARI imekuja na mkakati wa kuhakikisha kuwa
wakulima wanaelimishwa kuhusu matumizi ya zana bora za kilimo, kupanda kwa
kufuata taratibu elekezi zinazotolewa na wataalamu ikiwemo kujifunza teknolojia
sahihi zitakazoleta mabadiliko makubwa katika sekta ya kilimo.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment