Mkurugenzi wa kampuni ya Haffiyy entertainment Hafidh Mkongwa akiongea na waandishi wa habari juu ya mikakati ya kampuni hiyo kuinua vipaji na kuirudhisha Iringa kwenye ramani ya burudani
NA FREDY MGUNDA,IRINGA.
KAMPUNI ya Haffiyy entertainment ya
mkoani Iringa imejipanga kuhakikisha inainua vipaji vya wasanii wa bongo fleva
mkoani Iringa kwa lengo la kuwakomboa vijana kuirudisha Iringa kwenye ramani ya
Muziki kama ilivyokuwa hapo awali.
Akizungumza na waandishi
wa habari mkoani Iringa mkurugenzi wa kampuni ya Haffiyy entertainment Hafidh Mkongwa
alisema kuwa lengo la kampuni hiyo ni kuhakikisha wanakuza vipaji vya wasanii
wa bongo flava kwa kuongeza ajira kwa vijana.
“Kuna wasanii
wengi wanavipaji lakini wanakosa wasimamizi wazuri hivyo kampuni yangu
imejipanga kuhakikisha inawasimamia vilivyo kwenye sanaa hii na kuwaongezea
kipato lakini kukuza pia vipaji vyao” alisema Mkongwa
Mkongwa
alisema kuwa mkoa wa Iringa umepotea kwenye ramani ya burudani kwa muda mrefu
hivyo kmapuni hiyo imeweka mikakati madhubuti kuhakikisha kuwa Iringa inarudi
kwenye ramani ya burudani.
“Miaka ya
nyuma Iringa ilikuwa kwenye ramani ya burudani na ilikuwa inazalisha vipaji
vingi hivyo hapa katika tumepotea kwenye ramani hiyo hivyo kamapuni yangu
imejipanga vilivyo kuhakikisha wasaniii wa mkoa wa Iringa wanarudi kwenye
ramani ya burudani” alisema Mkongwa
Mkongwa
alisema kwa sasa kampuni ya Haffiyy Entertainmet imeanza kuwasimamia baadhi ya
wasanii kutoka mkoani Iringa na nyanda za juu kusini na sasa wameanza
kumsimamia msanii aitwaye Meda Classic na msanii aitwaye Casso anatoka katika
wilaya ya Temeke
“Hawa ndio
baadhi tu ya wasanii ambao tumeingia nao mikataba ya kusimamia kazi zao lakini
bado nawasaidia wasanii wengi ambao bado hawana mikataba na kampuni yangu hivyo
mtaona jitihada zangu zimeanza kwa kasi kubwa” alisema Mkongwa
Aidha Mkongwa
aliwaomba wananchi na wadau wa burudani mkoani Iringa kuendelea kuwaunga mkono
kwa juhudi ambazo zinazofanywa na kampuni hiyo ili kukuza burudani na
kuirudisha Iringa kwenye Ramani ya burudani.
“Iringa tulikuwa
tunafanya kazi vizuri mno hivyo baada ya kupotea kwenye ramani niwaombe wadau
tushirikiane kuhakikisha tunarudi kwenye ramani ya burudani” alisema Mkongwa
Mkongwa
alimalizia kwa kuwaomba wasanii wenye vipaji na nidhamu ya kazi basi wamtafute
ili kuhakikisha kuwa wanapata nafasi kwenye kampuni hiyo yenye leongo la kuinua
vipaji vyao na kuwaongezea ajira vijana hao.
0 comments:
Post a Comment