Naibu meya wa halmashauri ya manispaa ya Iringa Joseph Lyata kupitia chama cha mapinduzi akikagua utekelezaji wa ahadi waliyoitoa kwa wananchi wa kata ya Mkimbizi mtaa wa Ugele manispaa ya Iringa
Naibu meya wa halmashauri ya manispaa ya Iringa Joseph Lyata akiwa sambamba na Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM Manispaa ya Iringa Edwin Bashir pamoja na mwenyekiti wa vijana kata ya Mkimbizi wakikagua utekelezaji wa ahadi yao
Naibu meya wa halmashauri ya manispaa ya Iringa Joseph Lyata akiwa sambamba na Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM Manispaa ya Iringa Edwin Bashir pamoja na diwani wa kata ya Mwangata Nguvu Chengula wakifurahi jambo na wananchi wa mtaa wa Ugele mara baada ya kutekeleza ahadi ya ujenzi wa barabara
Naibu meya wa halmashauri ya manispaa ya Iringa Joseph Lyata akiwa sambamba na Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM Manispaa ya Iringa Edwin Bashir pamoja na diwani wa kata ya Mwangata Nguvu Chengula wakifurahi jambo na wananchi wa mtaa wa Ugele mara baada ya kutekeleza ahadi ya ujenzi wa barabara
NA
FREDY MGUNDA,IRINGA.
NAIBU
meya wa manispaa ya Iringa amewataka wananchi wa manispaa ya Iringa kumkataa
mbunge wa jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa kwa kushindwa kutekeleza
wajibu wa kuleta maendeleo kwa wananchi waliompa kura.
Akizungumza
na wananchi wa kata ya Mkimbizi mtaa wa Ugele,Naibu meya Joseph Lyata alisema kuwa mfuko wa mbunge
unapesa nyingi za kusaidia kuleta maendeleo kwa wananchi lakini hali imekuwa
tofauti kwa mbunge huyo kushindwa kutatua changamoto za wananchi.
“Mbunge
anauwezo wa kuwatembelea wananchi wa Ugele na kuja kutatua changamoto mlizonazo
kwa kuwa anapesa za mfuko wa mbunge ambao anauwezo wa kutoa pesa kwa ajili ya
kukarabati barabara hii ambayo imekuwa kikwazo kikubwa katika kuleta maendeleo
ya eneo hili” alisema Lyata
Lyata
alisema kuwa wananchi wa mtaa wa Ugele wanakabiliwa na tatizo la kukosa huduma
bora za afya kwa kuwa mbunge wa jimbo hilo hayupo tayari kuwasaidia kutatua
changamoto hizo.
“Mlifanya
kosa kubwa sana kumchagua mbunge huyo kwa kuwa hajawai kuja kuwasikiliza kero
zeo na kuzitatua ndio maana maumivu hayo mnayapa hii leo kwa kuwa hakuna
maendeleo ambayo mmefanyiwa na mbunge huyo” alisema Lyata
Lyata
amewataka wananchi wa mtaa wa Ugele kutomchagua tena mbunge huyo kuwa kuwa hana
faida ya kimaendeleo kwa wananchi kwa kuwa ameshindwa kuleta maendeleo kwa
kushindwa kuboresha sekta ya afya,elimu na miundombinu.
“Mmemchagua
kiongozi ambaye hawasikilizi na anashindwa kutatua kero za wananchi ndio maana
hadi hii leo mnateseka kwa kushindwa kutatuliwa kero zenu huyo sio kiongozi na
hafai tena kuwa kiongozi” alisema Lyata
Aidha
Lyata alisema kuwa chama cha mapinduzi manispaa ya Iringa kimeamua kutatua kero
zenu kwa kuwa hamna kiongozi ambaye anaweza kuwatatulia kero kwa kuwa mbunge
mliyemchagua ameshindwa kutatua kero hizo.
Naye Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM Manispaa ya Iringa Edwin Bashir aliwataka wananchi wa
mtaa huo kuendelea kuwa na imani na chama cha mapinduzi kwa kuwa kinafanya kazi
ya kuleta maendeleo kwa vitendo.
“Tulikuja
hapa kukiwa hakuna barabara lakini tulifanya mkutano wa hadhara na kuwasikiliza
kero zetu hatimaye mkatupa kero ya barabara na zahanati hivyo sasa tumeanza
kutengeza barabara kwa kiwango bora kinachosaidia kuleta maendeleo kwa
wananchi” alisema Bashir
Bashir
alisema kwa sasa hakuna chama kinachoweza kutekeleza ahadi zake kwa umakini
kama chama cha mapinduzi hivyo wananchi mnatakiwa kuendelea kuwa na imani na
chama hicho.
“Jamani
mnatakiwa kuendelea kukienzi na kukitunza chama hiki bora ambacho ndio chama
bora kwa kuleta maendeleo ya kweli kwa wananchi wake na sio vyama vingine”
alisema Bashir
Kwa
upande wake diwani wa kata ya Mwangata Nguvu Chengula alisema kuwa chama cha
mapinduzi na naibu meya wa manispaa ya Iringa walikuwa hawalali kwa ajili ya
kutatua tatizo la barabara ya Ugele kwa
kuwa wananchi hao wanahitaji kufanya kazi za kimaendeleo
“Wananchi
wa kata ya Ugele wanahitaji kufanya maendeleo kwa kuwa wamekuwa wachapa kazi
wakubwa lakini mbunge wao amekuwa hawasaidie kwa lolote hivyo ndio chama na
Naibu Meya walipobebe jukumu la kutatua changamoto hiyo” alisema Chegula
Chegula
alisema kuwa kipaumbele kilikuwa kutatua changamoto ya barabara ndipo
wanatafuta njia nyingine ya kutatua changamoto nyingine zilizopo katika mtaa wa
Ugele ili wananchi wafanye kazi kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
anavyotaka.
Nao wananchi wa Mtaa
wa Ugele Manyigi Uliopo Kata ya Mkimbizi Manispaa ya Iringa wameishukuru
serikali Chini ya Naibu Meya Manispaa ya Iringa kwa kuwakarabatia barabara
ambayo ilikuwa awali ilikuwa kero kwao.
“Baadhi ya wananchi wa
Mtaa huo wamesema kuwa awali kabla ya ukarabati wa barabara hiyo, wajawazito
walikuwa wanapata shida pindi wanapoelekea mjini kupata huduma za afya”
walisema wananchi
Mwenyekiti wa Mtaa wa
Ugele Manyigi Aloyce Laurent amemshukuru Naibu Meya Joseph Lyata kwa kupeleka
Greda katika Mataa wake na kurekebisha barabara ambayo ilikuwa kero kwa
wananchi wake.
0 comments:
Post a Comment