METDO Tanzania

METDO Tanzania

Friday, June 15, 2018

DC MUWANGO AZIMA MGOMO WA MASAA SABA WILAYANI NACHINGWEA

Utatuzi wa kinachoitwa sintofahamu kati ya wafanyabiashara wa soko kuu la Wilaya ya Nachingwea Mkoani Lindi na uongozi wa Mamlaka ya mji mdogo wa Nachingwea umefika ukomo.

Mkuu wa Wilayani hiyo  Mhe Muwango amesema kuwa mgomo huo umefikia ukomo kwa makubaliano ya kwamba tozo zote zifanyiwe mapitio ili kuondoa "tozo mzigo" kwa ajili ya kuwanusuru wafanyabiashara wadogo, wakati na wakubwa, ili kila mmoja alipe kulingana na uwezo wake.

Mhe Muwango amemuagiza Mkurugenzi wa Halamshauri ya Wilayani ya Nachingwea katika kipindi cha wiki mbili kuanza mchakato wa kuanza ukarabati wa soko, kwa kuwa fedha ilitengwa katika bajeti hivyo kinachotakiwa ni utekelezaji.

Katika mkutano wa hadhara akizungumza na wananchi wakiwemo wafanyabiashara Wilayani humo Mhe Muwango amewashukuru wafanyabiashara kwa kuwa wasikivu, na hatimaye kurejesha  huduma kwa kufungua maduka mara baada ya kikao hicho.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com