Mwenyekiti wa Halmashuri ya wilaya ya Iringa, Stephen Mhapa akikabidhiwa funguo za gari aina ya Toyota Hiece na mwakilishi wa IBO Iringa DC, Paola Ghezzi alisema kuwa shirika lisilo
la kiserikali la IBO limekuwa likijishughulisha na elimu maalumu kwa kuwasaidia
watoto wenye mahitaji maalumu,watoto wenye mazingira magumu na watoto wenye
ulemavu. Mwenyekiti wa Halmashuri ya wilaya ya Iringa, Stephen Mhapa akiwa kwenye gari hilo aina ya Toyota Hiece baada ya kukabidhiwa na shirika lisilo la kiserikali
la IBO lililoko nchini Italy kwa ufandhili wa wadau kama Waldesian
Church,Emilia-romagna Region,Ferrara Town,Helpicare na Nyumba ya Ali
Gari aina ya Toyota Hiece lilokabidhiwa na shirika lisilo la kiserikali
la IBO lililoko nchini Italy kwa ufandhili wa wadau kama Waldesian
Church,Emilia-romagna Region,Ferrara Town,Helpicare na Nyumba ya Ali
Baadhi ya wafanyakazi wa Halmashauri ya Iringa wakifurahia kupokea kwa msaada wa Gari hilo
NA FREDY MGUNDA, IRINGA.
Baadhi ya wafanyakazi wa Halmashauri ya Iringa wakifurahia kupokea kwa msaada wa Gari hilo
HALMASHAURI ya wilaya ya Iringa
imepokea msaada wa gari aina ya Toyota Hiece kwa ajili ya wanafunzi wa elimu
maalumu katika shule ya msingi Kipera kutoka kwa shirika lisilo la kiserikali
la IBO lililoko nchini Italy kwa ufandhili wa wadau kama Waldesian
Church,Emilia-romagna Region,Ferrara Town,Helpicare na Nyumba ya Ali.
Akizungumza wakati wa kukabidhi
Gari hilo mwakilishi wa IBO Iringa DC, Paola Ghezzi alisema kuwa shirika lisilo
la kiserikali la IBO limekuwa likijishughulisha na elimu maalumu kwa kuwasaidia
watoto wenye mahitaji maalumu,watoto wenye mazingira magumu na watoto wenye
ulemavu.
“Shirika hili linafanya kazi na
halmashuri ya Iringa kwa kusaidia watoto wenye changamoto hizo hapo juu kwa
lengo la kuwasaidia kiuchumi na kuwawezesha kupata mahitaji yao kama ilivyo kwa
watoto wengine wanaopata mahitaji yote muhimu” alisema Ghezzi
Ghezzi alisema kuwa shirka hilo
tayari limeshasaidia ujenzi wa jiko la shule ya msingi Kipera yenye watoto
mchanganyiko na watoto wenye ulemavu na
ujenzi huo bado unaendelea katika shule hiyo kwa lengo la kutoa hudumu bora kwa
wanafunzi wa shule hiyo.
“Tumefanikiwa kujenga Ramps
katika shule nne za halmashauri ya Iringa ambazo ni Ismani,Idodi,Ihehelo na Tungamalenga
kwa lengo la kuwasaidia watoto wenye ulemavu kupita bila kupata usumbufu wowote
ule” alisema Ghezzi
Aidha Ghezzi alisema kuwa
shirika hilo limefanikiwa kutoa mafunzo kwa walimu zaidi ya arobaini (40) kwa
kuwaongezea maarifa kwa ajili ya kufundisha elimu maalumu kwa wanafunzi
wanahitaji elimu hiyo katika halmashauri ya Iringa katika kata za Idodi na Ismani
tayari washapewa mafunzo.
“Tumefanikiwa kutoa semina na
maonesho kwa jamii juu ya umuhimu wa elimu maalumu kwa kata ya Ismani ambapo
shirika limefanikiwa kutoa elimu hiyo kwa jamii hadi hivi sasa” alisema Ghezzi
Akipokea gari hilo aina ya Toyota
Hiece mwenyekiti wa halmashuri ya wilaya ya Iringa, Stephen Mhapa aliwakikishia
shirika la IBO kuwa msaada ambao wamekuwa wakiutoa katika halmashauri hiyo
utatumika kama ulivyokusudiwa na miradi yote itatunzwa kikamilifu.
“Mmetusaidia sana miradi mingi
hivyo sisi tunaahidi kutunza na kuthamini miradi na uwepo wenu katika
halmashauri hii ambapo mmetusaidia kuwaokoa watoto wenye mahitaji maalumu,watoto
wenye mazingira magumu na watoto wenye ulemavu” alisema Mhapa
Mhapa alisema kuwa imekuwa
vigumu mno kumlea mtoto mwenye mahitaji maalumu,mtoto mwenye mazingira magumu
na mtoto mwenye ulemavu kwa kuwa inahitaji uangalizi mkubwa mno ila shirika la
IBO limetusaidia kulea watoto hao.
“Namna ilivyo tabu kumlea mtoto
mwenye mahitaji maalumu,mtoto mwenye mazingira magumu na mtoto mwenye ulemavu,wakina
mama mnajua ilivyo kuwa kazi ngumu hivyo tunaomba kutoa shukrani zetu kwa wadau
ambao wanatusaidia kulea watoto hao” alisema Mhapa
Mhapa alimalizia kwa kuagiza
mkurugenzi wa halmashauri ya Iringa kuhakikisha wanawaandikia barua ya shukrani
kwa shirika la IBO kwa kuasiadia miradi mbali mbali ambayo imekuwa ikiwasaidia watoto
wenye mahitaji maalumu,watoto wenye mazingira magumu na watoto wenye ulemavu.
Lakini Mhapa aliomba shirika
hilo kuendelea kuwasaidia katika mahitaji mbalimbali kwa kuwa bado halmashauri
hiyo inakabiliwa na changamoto nyingi za watoto hao na nyingi zinazoshabiana na
changamoto hizo hivyo mkipata kitu tunaomba mtukumbuke ili tuendelee kutatua
changamoto hizo.
0 comments:
Post a Comment