Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati akimuwakilisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa kwenye kongamano la Vyama vya Ushirika wa Akiba na Mikopo Afrika linalofanyika mkoani Mwanza katika ukumbi wa Malaika Beach Resort leo tarehe 27 Machi 2019.
Sehemu ya washiriki wa kongamano la Vyama vya Ushirika wa Akiba na Mikopo Afrika linalofanyika mkoani Mwanza katika ukumbi wa Malaika Beach Resort leo tarehe 27 Machi 2019 wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi-Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb).
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati akimuwakilisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa kwenye kongamano la Vyama vya Ushirika wa Akiba na Mikopo Afrika linalofanyika mkoani Mwanza katika ukumbi wa Malaika Beach Resort leo tarehe 27 Machi 2019.
Mrajis wa Vyama vya Ushirika Tanzania Ndg Tito Haule akizungumza jambo mbele ya Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) kwenye kongamano la Vyama vya Ushirika wa Akiba na Mikopo Afrika linalofanyika mkoani Mwanza katika ukumbi wa Malaika Beach Resort leo tarehe 27 Machi 2019.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa kongamano la Vyama vya Ushirika wa Akiba na Mikopo Afrika linalofanyika mkoani Mwanza katika ukumbi wa Malaika Beach Resort leo tarehe 27 Machi 2019 wakati akimuwakilisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa.
Na Mathias Canal,
Wizara ya Kilimo –Mwanza
Wizara zote zinazohusika na Vyama vya Ushirika kwa Akiba na Mikopo
(SCCULT) zimetakiwa kuhakikisha kwamba zinakuwa na dawati la Ushirika na
taarifa zake kuwasilishwa kwa Mrajis wa Vyama vya Ushirika Tanzania.
Pia, Tume ya Maendeleo ya Ushirika imetakiwa kuhakikisha kuwa
inasimamia, kudhibiti na kuhamasisha Vyama vya Ushirika viweze kufanya kazi
kikamilifu na kwa wakati kwa kuzingatia Sheria ya Ushirika Namba 6 ya mwaka 2013 na Kanuni zake za mwaka 2015; na kanuni za Vyama vya Ushirika
wa akiba na mikopo ya 2014.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameyasema hayo wakati
akimuwakilisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim
majaliwa kwenye kongamano la Vyama vya Ushirika wa Akiba na Mikopo Afrika
linalofanyika mkoani mwanza katika ukumbi wa Malaika Beach Resort leo tarehe 27
Machi 2019.
Mhe Hasunga alisema kuwa mamlaka zote zinazohusika na Maendeleo ya
Sekta ya Ushirika nchini zijiwekee malengo yanayotekelezeka ya kusukuma
gurudumu la Maendeleo ya ushirika na kujipima kila mara.
Kadhalika Serikali imesema kuwa itaendelea kuwachukulia hatua kali
za kisheria kwa wote wanaobainika kuhujumu dhamira njema ya maendeleo ya
ushirika kwani kufanya hivyo ni kwenda kinyume na matarajio ya kuanzishwa kwa
vyama hivyo.
Mhe Hasunga alisema kuwa Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na
Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeendelea
kuweka mikakati mbalimbali ili kuhakikisha kuwa Sekta ya Ushirika inakua na
kujisimamia vema katika utekelezaji wa majukumu yake japo bado kuna wabadhilifu
wachache wanaoendelea kubainika.
Alisema kuwa Ushirika wa Akiba na Mikopo una umuhimu mkubwa katika jamii kwani unajenga
Jamii yenye utamaduni wa kuweka akiba ya fedha mara kwa mara na kuwa na
matumizi bora ya fedha zao kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya siku za usoni, Kuanzishwa
kwa SACCOS nyingi katika maeneo mengi ya vijijini, ambazo zimesogeza karibu
huduma za kifedha kwa wananchi wa kawaida, Kuwawezesha
kumiliki na kuendesha taasisi yao wenyewe ya fedha; na Kutoa mikopo kwa
wanachama wake kwa masharti na riba nafuu wanayojiwekea wao wenyewe kwa mujibu
wa Sheria na Kanuni kwa ajili ya Kuboresha maendeleo ya kiuchumi na ya kijamii.
Vilevile umuhimu wake ni pamoja na Kushiriki katika mipango ya Serikali ikiwemo kuanzisha ajira na
kupunguza tatizo la ukosefu wa ajira, kwa kuajiri watendaji katika ngazi
mbalimbali kwenye SACCOS zenyewe na kwenye miradi inayoanzishwa na wanachama wa
SACCOS, Kujenga uelewa wa masuala ya fedha kwa wananchi wa kawaida na
kuimarisha nidhamu ya fedha, Kuwajengea Wanachama hali ya kujitegemea wao
wenyewe kwa kuwawezesha kukopa katika Chama chao badala ya kukopa kwa watu
binafsi au benki za biashara ambazo hutoa masharti magumu na Kuwawezesha
Wanachama kupata huduma za Bima katika shughuli zao.
Alisema SCCULT imejiendesha kwa udhaifu kwa kutotoa huduma stahiki
kwa wanachama wake kwa muda mrefu takribani Miaka 10, kipindi hicho ikiwa na
idadi ya Wanachama 1,247. Hadi kufikia
mwaka 2019 Januari zoezi la uhakiki juu ya uwepo wa wanachama hawa kama wapo
hai na wanafanya shughuli zao umebaini takribani Vyama wanachama 500 tu ambavyo
vipo hai na vinafanya kazi.
“Hivyo mnapaswa kuhamasisha wanachama kujiunga kwa wingi kwenye
SCCULT ili kuwa na wanachama wengi kama nchi za wenzetu zinavyofanya”
Alikaririwa Mhe Hasunga
Alisema kuwa ni lazima kuwe na mikakati thabiti Ili kuvifikia
vyama vyote hivyo na kuvifanya viweze kushiriki kwenye shughuli mbalimbali za
SCCULT, na kuhakikisha kuwa SCCULT inatekeleza ipasavyo malengo ya kuanzishwa
kwake ikiwa ni pamoja na kuhamasisha vyama ambavyo havijajiunga na SCCULT
viweze kujiunga ili viwe na sauti moja kama nchi za wenzetu zinavyofanya.
Mhe Hasunga alizitaja baadhi ya changamoto zinazoikabili Sekta ya
Ushirika nchini Tanzania kuwa ni pamoja na Kuporomoka kwa imani ya ushirika
miongoni mwa jamii na kwa baadhi ya wanachama kutokana na Vyama vya Ushirika
kushindwa kukidhi mahitaji ya wanachama wake, Wizi na Ubadhirifu wa rasilimali
za Ushirika kwa baadhi ya viongozi na watendaji wa Vyama vya Ushirika waliopewa
dhamana ya kuvisimamia na kuviendesha Vyama vya Ushirika kwa maslahi ya
wanachama, na Ukosefu wa elimu ya kutosha ya ushirika miongoni mwa Wanachama,
Viongozi na watendaji wa Vyama vya Ushirika.
MWISHO.
0 comments:
Post a Comment