Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Innocent Bashungwa (Mb) akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Bia Tanzania (TBL) katika nchi za Tanzania na Uganda Ndg Philiph Redmaw baada ya kukutana na kufanya mazungumzo leo tarehe 26 Machi 2019, Jijini Dodoma. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Baadhi ya watendaji wakifatilia kikao kazi cha Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Innocent Bashungwa (Mb) na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Bia Tanzania (TBL) katika nchi za Tanzania na Uganda Ndg Philiph Redmaw leo tarehe 26 Machi 2019, Jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Innocent Bashungwa (Mb) akisisitiza jambo wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Bia Tanzania (TBL) katika nchi za Tanzania na Uganda Ndg Philiph Redmaw leo tarehe 26 Machi 2019, Jijini Dodoma.
Baadhi ya watendaji wakifatilia kikao kazi cha Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Innocent Bashungwa (Mb) na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Bia Tanzania (TBL) katika nchi za Tanzania na Uganda Ndg Philiph Redmaw leo tarehe 26 Machi 2019, Jijini Dodoma.
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo – Dodoma
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Innocent Bashungwa (Mb)
amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Bia
Tanzania (TBL) katika nchi za Tanzania na Uganda Ndg Philiph Redmaw kujadili
namna ya kufungamanisha uchumi kupitia sekta ya Kilimo na Viwanda.
Akizungumza katika kikao kazi kilichofanyika katika
ukumbi wa mikutano maarufu kama Kilimo (IV) Jijini Dodoma leo tarehe 26 Machi
2019, Mhe Bashungwa alisema kuwa kampuni hiyo inazalisha bia kwa wingi nchini
Tanzania hivyo makubaliano hayo yanaongeza chachu na tija katika kuongeza
masoko ya wakulima nchini.
Kwa kauli moja kikao hicho kimeridhia mkataba huo
kusainiwa mwezi Aprili mwaka huu “Tutasaini mkataba wa makubaliano kati yetu
serikali na kampuni ya TBL ili kuimarisha soko la wakulima kwani TBL
wanategemea bidhaa zitokanazo na mazao ya mtama, zabibu, shairi na mahindi”
Alisema
Katika kikao hicho Mhe Bashungwa amesema kuwa makubaliano
hayo punde yatakaposainiwa yataongeza mtazamo wa jumla kwa wakulima nchini kujipatia
masoko ya mazao hayo ya mvinyo.
Katika zaao la mahindi pekee nchini wakulima wana
ziada ya Tani 810,000 huku bei ikiwa chini hivyo makubaliano hayo yametazama
zaidi mahitaji ya TBL kwenye mahindi na kuzingatia ubora ili wakulima waweze
kunufaika na fursa hiyo” Alikaririwa Mhe Bashungwa
Alisema kuwa moja ya mikakati ya serikali ya awamu
tano inayoongozwa na Mhe Rais Dkt John Pombe Magufuli ni pamoja na kutafuta
masoko ya mazao ya wakulima nchini ili wakulima wa mazao yote waweze kunufaika
na utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi.
“Tumeamua kuingia makubaliano na TBL kwa kuwa
katika kipindi cha muda mrefu wakulima wamekuwa wakihakikishiwa na kampuni za
vinywaji kulima mazao mengi kwamba soko lipo lakini baada ya mavuno kampuni
zinaingia mitini bila manufaa kwa wakulima wetu, sasa hatutaki kurudi huko huu
ni mkakati kabambe wa kuwanufaisha” Alikaririwa Mhe Bashungwa
Makubaliano hayo yatabainisha majukumu ya kila
mmoja ndani ya TBL na wizara ya kilimo ambapo Benki ya Maendeleo ya kilimo
(TADB) kutoa ushirikiano kwa mkulima kuanzia hatua za awali za uzalishaji mbegu
kwenda kwa mkulima sambamba na elimu kutolewa kwa mkulima kuhusu kuzingatia
kanuni bora za kilimo.
Alisema kuwa kikao hicho pia kimetazama namna
ambavyo TADB itaweza kusaidia Wakala wa Mbegu Tanzania (ASA) ili kuzalisha kwa
wingi mbegu bora zitakazosambazwa kwa wakulima ili wakulima hao waweze
kuzalisha mazao bora na yenye tija katika soko.
Bashungwa amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli kwa kuakisi utendaji na mkakati wake wa kuimarisha masoko ya wakulima nchini.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment