Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akizungumza wakati akifungua kongamano la siku tatu la Kitaifa la Kisayansi kuhusu Bioanuwai, Visumbufu na matumizi sahihi na salama ya teknolojia za viuatilifu linalofanyika katika ukumbi wa Taasisi ya kusimamia na kudhibiti Viuatilifu-TPRI Jijini Arusha, leo tarehe 28 Machi 2019. (Picha Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Baadhi ya washiriki wa kongamano la siku tatu la Kitaifa la Kisayansi kuhusu Bioanuwai, Visumbufu na matumizi sahihi na salama ya teknolojia za viuatilifu linalofanyika katika ukumbi wa Taasisi ya kusimamia na kudhibiti Viuatilifu-TPRI Jijini Arusha wakifatilia hotuba ya Mgeni rasmi-Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) wakati wa ufunguzi wa kongamano hilo, leo tarehe 28 Machi 2019.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akizindua tovuti wakati akifungua kongamano la siku tatu la Kitaifa la Kisayansi kuhusu Bioanuwai, Visumbufu na matumizi sahihi na salama ya teknolojia za viuatilifu linalofanyika katika ukumbi wa Taasisi ya kusimamia na kudhibiti Viuatilifu-TPRI Jijini Arusha, leo tarehe 28 Machi 2019.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akizungumza wakati akifungua kongamano la siku tatu la Kitaifa la Kisayansi kuhusu Bioanuwai, Visumbufu na matumizi sahihi na salama ya teknolojia za viuatilifu linalofanyika katika ukumbi wa Taasisi ya kusimamia na kudhibiti Viuatilifu-TPRI Jijini Arusha, leo tarehe 28 Machi 2019.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akikagua mbegu mbalimbali mara baada ya kutembelea kampuni ya wazalishaji na wasambazaji wa mbegu bora ya Suba Agro wakati wa kongamano la siku tatu la Kitaifa la Kisayansi kuhusu Bioanuwai, Visumbufu na matumizi sahihi na salama ya teknolojia za viuatilifu linalofanyika katika ukumbi wa Taasisi ya kusimamia na kudhibiti Viuatilifu-TPRI Jijini Arusha, leo tarehe 28 Machi 2019.
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo –Arusha
Sanjari na matumizi sahihi na salama ya viuatilifu na
uhifadhi wa mazingira yanayotuzunguka, bado sekta ya viuatilifu imekuwa na
changamoto nyingi.
Kutokana na ukubwa wa nchi ya Tanzania na mipaka yake sambamba
na kupakana na nchi nyingine nyingi pamekuwapo na upitishwaji usio
rasmi wa viuatilifu katika mipaka na hususani kwa mikoa ya mipakani unaofanywa
na wafanyabiashara na wananchi wasiowaaminifu. Hali hiyo imepelekea kuwepo kwa viuatilifu visivyo na ubora kwa
wakulima kwa baadhi ya maeneo.
Waziri
wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameyasema hayo leo tarehe 28 Machi 2019 wakati
akifungua kongamano la siku tatu la Kitaifa la Kisayansi kuhusu Bioanuwai, Visumbufu
na matumizi sahihi na salama ya teknolojia za viuatilifu linalofanyika katika
ukumbi wa Taasisi ya kusimamia na kudhibiti Viuatilifu-TPRI Jijini Arusha.
Mhe Hasunga amewataka Wakaguzi wa
viuatilifu wa TPRI, Maafisa ugani pamoja na vyombo vya dola kushirikiana kwa karibu katika kubaini
ufumbuzi wa jambo hilo na punde watakapowabaini waagizaji na wasambazaji wa
viuatilifu feki nchini kuwanyang’anya leseni zao sambamba na kuwachukulia hatua
za kisheria.
Kadhalika, TPRI imetakiwa
kutojihusisha na rushwa katika usajili wa viuatilifu nchini na endapo kuna
mtendaji atabainika akijihusisha na rushwa ya uzembe ama kitaaluma atachukuliwa
hatua kali za kisheria.
Pia amewataka TPRI kuhakikisha
kuwa wanasimamia uteketezaji wa viuatilifu vyote ambavyo vimebainika kuwa feki
sambamba na kuandaa mpango maalumu wa utekelezaji wa majukumu hayo.
Alisema kupitia mpango wa TPRI wa kufungua Ofisi na matawi yake katika Kanda
nne nchini zikiwepo Nyanda za Juu Kusini, Kanda ya Ziwa, Kanda ya Kusini na
Kanda ya Kaskazini, kutekleza vyema majukumu yake ili kubaini na kuwachukulia
hatua kali za kisheria wahujumu wa uingizaji na usambazaji wa viuatilifu kwa
wakulima nchini.
Alisema mkakati huo utaowaongezea uwezo katika kupambana na tatizo hilo la uingizaji wa
viuatilifu kwa njia za panya.
“Kuna
madhara makubwa kwa mwananchi mmojammoja na Taifa kwa ujumla wake kutokana na
usambazaji wa viuatilifu feki hivyo kama Waziri mwenye dhamana ya kusimamia
sekta ya kilimo nitahakikisha tunaikabili na kubaini chanzo chake ili kuiondoa
changamoto hii” Alikaririwa Mhe Hasunga
Alisema, Sekta ya Kilimo
imendelea kuwa ni mhimili mkubwa wa
uchumi wa Tanzania na katika mwaka 2017 sekta hiyo imetoa ajira kwa asilimia
65.5 na kuchangia asilimia 65 ya malighafi za viwanda. Aidha , mchango wa sekta
katika pato la Taifa ni asilimia 30.1 ambapo Sekta ndogo ya mazao imechangia
asilimia 17 pekee.
Kutokana na umuhimu huo, Serikali
inaendelea kutekeleza mikakati ya kuongeza kasi ya kukuza kilimo, ili kuchochea
na kufikia uchumi wa viwanda sawa sawa na Azma ya Serikaliya Awamu ya
Tano.
Mhe Hasunga alisema kuwa Mabadiliko
ya tabia nchi ni mtiririko wa mfumo wa mabadiliko ya hali ya hewa yanayochukua
muda mrefu au mfupi na kusababisha hali mbaya za hewa ama uchache wa hali
inayohitajika au wingi wa hali isiyohitajika na kusababisha madhara kwa jamii
na nchi kwa ujumla.
Kwa zaidi ya miaka 50, hali ya
hewa duniani imekuwa ikibadilika kwa sababu ya kuongezeka gesi chafu
zinazozalishwa na mvuke wa maji, methane na
kaboni dayoksaidi, hasa kutokana
na kuungua kwa mafuta na makaa ya mawe,
ukataji hovyo wa miti na shughuli
nyingine za kibinadamu kama kilimo, Ukuaji wa miji na uchimbaji wa madini.
Hali hii ya mabadiliko ya tabia
nchi imesababisha kuwepo kwa ongezeko la visumbufu vya mazao kama vile wadudu
kuzaliana kwa wingi kutokana na ongezeko la joto, kuingia kwa magonjwa mapya ya
mazao kama (Maize necrosis), Viwavi jeshi vamizi (Fall army worms) kuenea kwa
magugu vamizi na hata ongezeko la mbu kwa mikoa na miji ile iliyokuwa na hali
ya baridi miaka ya nyuma.
Kongamano
hilo la siku tatu litakuwa na muktadha wa kujadili Bioanuwai, Visumbufu na
Matumizi Sahihi na Salama ya Teknolojia za Viuatilifu katika kukuza kilimo ili
kujenga Tanzania ya Viwanda. Na kuwa na mawasilisho katika nyanja za Ubunifu na
Ugunduzi wa Teknolojia na mbinu mbalimbali
katika kudhibiti visumbufu vya mazao yakiwa shambani na ghalani; Teknolojia
katika uzalishaji viuatilifu na madhara ya mabaki yake katika mzingira; Matumizi
ya Viuatilifu katika kudhibiti wadudu waenezao magonjwa ya binadamu na mifugo; Masuala
ya kisheria katika matumizi sahihi na
salama ya viuatilifu na Matumizi endelevu ya bioanuwai katika kukuza viwanda.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment