Mashindano ya michezo yanayoendeshwa na Taasisi ya The Angeline Foundation yanayotarajiwa kuanza siku chache zijazo yatagawa vifaa vya michezo kwa timu shiriki kutoka makundi mbalimbali yaliyopo ndani ya Jimbo la Ilemela
Kauli hiyo imetolewa leo na mgeni rasmi wa fainali za mashindano ya mpira wa miguu Mhe Bhiku Kotecha ambae ni Naibu Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza yaliyoshirikisha Timu zaidi ya 14 huku Timu 9 zikiwa ni za matawi ya Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi UVCCM na Timu 5 zikitoka makundi maalumu kama Vyuo Vikuu, Waendesha Matoroli, Waendesha bodaboda na Jeshi la polisi yaliyojukikana kama Ramadhani Cup ambapo akiwasilisha salamu za Mbunge wa Jimbo la Ilemela Mhe Dkt Angeline Mabula amesema kuwa Mbunge wa Jimbo hilo atagawa vifaa vya michezo kwa Timu zote zitakazoshiriki mashindano ya Jimbo Cup pamoja na kusisitiza juu ya kukubali matokeo iwe kushindwa ama kushindwa ili kuepusha vitendo vya uvunjifu wa amani
'... Waziri kaniagiza niwaambie yupo pamoja nanyi na katika mashindano ya mwaka huu atagawa vifaa vya michezo na mipira kwa timu zote zitakazoshiriki lakini mtambue tu katika michezo kuna kushinda na kushindwa ni lazima tuwe teyari kwa lolote litakalojitokeza ...' Alisema
Aidha Mhe Kotecha ameziasa timu za Taasisi kuhakikisha zinashiriki mashindano hayo sanjari na kuwataka vijana wa mkoa wa Mwanza kuwa mstari wa mbele katika kutumia fursa mbalimbali za kujiletea maendeleo zinazojitokeza.
Kwa upande wake Katibu wa UVCCM kata ya Kirumba Comrade Amiri Biliyomo amefafanua juu ya malengo ya kuanzisha mashindano hayo ya Ramadhan Cup ikiwa ni pamoja na kurudisha hamasa kwa vijana katika kuungana pamoja, kujiepusha na vitendo viovu ikiwemo matumizi ya madawa ya kulevya, wizi na vitendo vingine vya uvunjifu wa amani.
Mashindano ya Ramadhan Cup yalihudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo UVCCM mkoa Mwanza walioongozwa na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, UWT walioongozwa na Katibu wa Jumuiya hiyo ngazi ya mkoa, Viongozi wa Chama na Jumuiya zote za wilaya ya Ilemela ambapo yaliisha kwa Timu ya Polisi Ilemela kuicharaza vikali Timu ya Kirumba Kati goli moja kwa sifuri lililofungwa katika kipindi cha Pili dakika ya 35 na mchezaji wao machachari Emmanuel Maba na kujifanya timu hiyo kuondoka na mbuzi wawili pamoja na kombe.
' Ilemela ni yetu, tushirikiane kuijenga '
Imetolewa na
Ofisi ya mbunge
Jimbo la Ilemela
27.05.2018.
0 comments:
Post a Comment