Na
Issa Mtuwa Songea
Makamu
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Mhe. Mariam
Ditopile Mzuzuri amesema kamati yake inaipongeza na itaendelea kuiunga mkono
Wizara ya Madini kwa kazi nzuri wanayoifanya.
Akiongea
na waandishi wa habari mbele ya kamati yake Machi 13, 2019 mjini songea baada
ya kukagua ujenzi wa kituo cha umahiri (Centre of excellence) kwa mkoa wa
ruvuma, Mzuzuri amesema kamati yake inaridhishwa na kazi za Wizara ya Madini na
wataendelea kuiunga mkono (support) hasa swala la wachimbaji wadogo.
“Tunawapongeza
sana Wizara ya Madini, mnafanya kazi nzuri na sisi kama kamati niseme
tutaendelea kuwaunga mkono (support) hasa hili la wachimbaji wadogo” alisema
Mzuzuri.
Naibu
Wziri wa Madini Mhe. Stanslaus Nyongo ameiambia kamati kuwa wizara yake
imejipanga katika kukamilisha ujenzi wa vituo vyote vya umairi kikiwemo cha
Songea kwa kuzingatia ubora. Amesema ujenzi wa vituo vyote unakwenda vizuri,
hata hivyo kituo cha songea kilichelewa ujenzi wake tofauti na vituo vingine
kwa sababu mbalimbali ikiwemo uhaba wa upatikanaji wa kokoto tatizo ambalo
lilisha tatuliwa na kwa sasa ujenzi unaendelea kwa kasi.
“Mheshimiwa
Mwenyekiti, Wizara imekusudia kukamilisha ujenzi wa kituo hiki na vingine kwa
wakati na kama nilivyo tangulia kusema zile changamoto zimesha tatuliwa na
tuaendelea vizuri. Naishukuru kamati yako kwa kutuunga mkono na ushauri wote
uliotolewa tutauzingatia.” Alisema Nyongo.
Nae
Katibu Tawala wa mkoa wa Ruvuma Prof. Riziki Shemdoe akiongea kwa niaba ya mkuu
wa mkoa huo amewambia wajumbe wa kamati kuwa ni kweli kuna kipindi mkoa wa
Ruvuma ulikumbwa na changamoto za upatikanaji wa kokoto na miradi mingi ya
serikali ilisimama kutokana na kuwa na kampuni moja tu ya uzalishaji wa kokoto
mkoa nzima, mara baada ya mitambo yake kuharibika na uzalishaji kusimama
upatikanaji wa kokoto ulikuwa ni tatiizo.
Kituo
cha Umahiri Songea ni miongoni mwa vituo mbalimbali vinavyo jengwa hapa nchini
katika maeneo mbalimbali kama vile, kituo cha Bukoba, Simiyu, Tanga, Chuya kwa
lengo la kuwasaidia wachimbaji wadogo kujifunza na kupata uelewa wa masuala
mbalimbali madini.
XXXX XXXX XXXX XXXX
Caption ya Picha
1.
Naibu Waziri wa Madini Stanslaus
Nyongo alie mbele akikagua na kutoa maelekezo kwa Meja Atupele Mwamfupe Meneja
wa Ujenzi SUMA JKT Kanda ya Kusini kulia kwa Meja ni Mkurugenzi wa Utawala na
Raslimali watu wa Wizara ya Madini Issa
Nchasi kabla ya kuwasili kwa kamati ya Bunge ya Nishati na Madini (Picha Na.
124859-3)
2.
Meneja wa Kanda ya Ujenzi SUMA JKT,
Meja Atupele Mwamfup akitoa maelezo kuhusu ujenzi wa kituo na kutafsiri michoro
mbalimbali ya jengo. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Utawala na Raslimali Watu
Wizara ya Madini Issa Nchasi, Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo, Makamu Mwenyekiti
Mhe. Mriam Mzuzuri na wajumbe wengine. (Picha Na. 143451-8)
3.
Naibu Waziri wa Madini Stanslaus
Nyongo akitoa maelezo ya ujenzi wa kituo cha umahiri songea kwa Makamu
Mwenyekiti wa kamati Mhe. Mariam Mzuzuri kushoto kwake. Wa kwanza kushoto ni
Mkurugenzi wa Utawala na Raslimali Watu Wizara ya Madini Issa Nchasi na Meja
Atupele Mwamfupe Meneja wa Ujenzi SUMA JKT Kanda ya Kusini. (Picha Na. 143702-4)
4.
Makamu Mwenyekiti wa kamati ya kudumu
ya Bunge ya Nishati na Madini, Mhe. Mariam Mzuzuri akimueleza jambo Naibu
Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo wa kulia kwake mara baada ya kukagua ujenzi
wa kituo cha umairi. (Picha Na. 145341-9)
0 comments:
Post a Comment