Naibu Waziri Omary Mgumba akiwa pamoja Meneja wa Kampuni ya
OCP Tanzania, Dkt. Mshindo Msolla katika ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya kilimo
Jijini Dodoma, tarehe 4/4/2019
Naibu Waziri Omary
Mgumba akiwa pamoja Mgeni wake Makamu wa Rais wa Kampuni ya OCP Afrika
Mashariki, Wakuu wa Idara na Taasisi za Wizara ya Kilimo pamoja na Watendaji wa
Kampuni ya OCP Barani Afrika katika ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya kilimo
Jijini Dodoma
Naibu Waziri Omary
Mgumba akiwa pamoja Mgeni wake Makamu wa Rais wa Kampuni ya OCP Afrika
Mashariki, Bwana Faysal Benameur (Kulia kwake) pamoja na Watendaji wa Kampuni
ya OCP Barani Afrika na Wakuu wa Idara na Taasisi za Wizara ya Kilimo mara
baada ya kumalizika kwa Mikutano wao, Jijini Dodoma
Naibu
Waziri wa Wizara ya Kilimo, Mhe. Omary Mgumba amewaeleza Wawekezaji kutoka
nchini Morocco ambao ni Kampuni ya Mbolea ya Taifa (OCP) ya nchini kuwa Tanzania
inaunga mkono juhudi za kuendeleza kilimo na amewahakikishia kuwa Serikali
itahakikisha inawasaidia ili wafanikishe azma yao ya kujenga kiwanda cha mbolea
mkoani Lindi katika wilya ya Kilwa.
Naibu
Waziri Mgumba akiwa pamoja na Wakuu wa Idara na Taasisi za Wizara ya Kilimo
katika ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya kilimo Jijini Dodoma amemwambia Makamu
wa Rais wa Kampuni ya OCP Afrika Mashariki, Bwana Faysal Benameur mapema leo
kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kumwinua Mkulima wa Tanzania ambapo
mkazo umewekwa katika kuongeza uzalishaji na tija kwenye mazao ya chakula na
biashara na kwamba ujenzi wa Kiwanda cha mbolea nchini utachochea katika ongezeko
la uzalishaji na tija.
Waziri
Mgumba amesema nchi zote zilizoendelea, zimepiga hatua kubwa katika Sekta ya
Kilimo kwa kuwa zinazingatia matumizi makubwa ya mbolea yanaenda sambamba na
eneo la uzalishaji pamoja na kujibu hitaji la mapungufu ya virutubisho vilivyo kwenye
udongo na si ilimradi kutumia mbolea tu.
Naibu
Waziri wa Kilimo Mgumba ameongeza kuwa uwiano wa matumizi ya mbolea na eneo la
kilimo hapa nchini upo chini sana, ukilinganisha na nchi za Afrika na zile zilizoendelea,
akitoa mfano amesema, hapa Tanzania, matumizi ya mbolea ni kilo 20 kwa hekta, Ethiopia
na nchi nyengine za Afrika ni kilo 100 kwa hekta wakati nchini Marekani na nchi
nyingine, zilizoendelea matumizi yao ya mbolea ni kilo 1,000 (Sawa tani 1) kwa
hekta.
“Kwa
uwiano huu, hatuwezi kuzalisha kwa kiwango kikubwa na ndiyo maana tija ipo
chini, nitoe mfano, kwenye uzalishaji wa mahindi, Tanzania tunazalisha tani
mbili (2) kwa hekta huku Ethiopia ikizalisha tani sita (6) kwa hekta wakati
Marekani, wanazalisha tani kumi (10) hadi kumi na mbili (12). Amekaririwa Mhe.
Mgumba.
“Napenda
Wakulima wa Tanzania wafahamu kuwa suala la muhimu si kutumia tu mbolea, lazima
tujenge mazingira mazuri ya kufahamu mahitaji halisi ya virutubisho
vinavyokosekana kwenye udongo, ardhi yetu imelimwa na mababu na mababu, na
wazazi wetu, na wao wameshafariki, hatutaweza kuzalisha kwa tija bila kutumia
mbolea”. Amesisitiza Naibu Waziri Mgumba.
“Nawapongeza
Kampuni ya OCP kwa kuliona jambo hilo na huo ndiyo msimamo wao na watatusaidia
kwa kuwa wanavifaa vya kufanya tathmini ya udongo kabla ya kuwauzia Wakulima
mbolea.” Amekaririwa Mhe. Mgumba.
Naye
Meneja wa Kampuni ya Mbolea ya OCP (Tanzania) Dkt. Mshindo Msolla amesema Kampuni
hiyo inataraji kujenga Vituo vya kufanya majaribio ya kuonyesha namna zoezi la upimaji
wa udongo linavyofanyika, matokeo baada ya kupima na matumizi ya mbolea za OCP kulingana
na matokeo ya taarifa hizo na kuongeza kuwa tarehe 8 Aprili wanataraji kuzindua
Kituo kimoja Mkoani Songwe.
Waziri
Mgumba amesisitiza kuwa Vituo (Ward Resources Centre) kama hivyo vinapaswa
kujengwa katika ngazi ya Tarafa ambapo Serikali ilishajenga vituo hivyo kupitia
Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo Awamu ya Kwanza (ASDP I) na kuongeza
sasa ni wakati muhafaka wa kuviendeleza.
Kampuni
ya Mbolea ya OCP ipo katika mazungumzo ya kujenga kiwanda cha mbolea katika
mkoa wa Lindi Wilaya ya Kilwa ambapo jumla ya dola bilioni 1.7 zinataraji
kuwekezwa katika mradi huo mkubwa ambapo kwa kuanzia Kampuni ya OCP imeanza
kujenga mashine ya kuchanga virutubisho ya madini mbalimbali ili kupata mbolea
za iana tofauti hapa nchini.
Imeelezwa
kuwa ujenzi wa Kiwanda hicho cha mbolea utasaidia kupunguza gharama ya bei ya
mbolea kwa zaidi ya asilimia 30 hadi 40.
0 comments:
Post a Comment