METDO Tanzania

METDO Tanzania

Thursday, March 14, 2019

WAZIRI HASUNGA NA MHANDISI METHEW MTIGUMWE, WARIDHISHWA NA KASI YA UJENZI WA OFISI ZA WIZARA YA KILIMO

Jengo la Wizara ya Kilimo likiwa katika hatua za mwisho kukamilika katika mji wa serikali Ihumwa Jijini Dodoma. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Methew Mtigumwe wakikagua ujenzi wa Ofisi za Wizara unaendelea kujengwa katika mji wa serikali Ihumwa Jijini Dodoma.
 Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Methew Mtigumwe wakikagua ujenzi wa Ofisi za Wizara unaendelea kujengwa katika mji wa serikali Ihumwa Jijini Dodoma.

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Methew Mtigumwe wakiwa katika picha ya pamoja na mafundi wa Ofisi za Wizara katika mji wa serikali Ihumwa Jijini Dodoma.

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Methew Mtigumwe kwa kauli moja wameridhishwa na ujenzi wa Ofisi za Wizara unaendelea kujengwa katika mji wa serikali Ihumwa Jijini Dodoma.

Mhe Hasunga amesema kuwa Ofisi hizo zimekamilika kwa asilimia nyingi hivyo wakati wowote kuanzia hivi sasa watumishi wa Wizara hiyo watapaswa kuhamia.

Ametoa kauli hiyo mara baada ya kutembelea na kukagua hatua zilizofikiwa za ujenzi wa Ofisi hizo leo Tarehe 14 Machi 2019.

Pamoja na mambo mengine Waziri Hasunga alimpongeza Rais wa Tanzania Mhe Dkt John pombe Magufuli kwa uamuzi wake ambao umetoa muelekeo wa serikali kuwa na mji wake maalumu jambo hilo litaongeza ufanisi katika kuwahudumia wananchi.

Alisema kuwa awali maamuzi ya Rais yalipotolewa wengi hawakuelewa makusudi ya ujenzi wa mji wa kiserikali lakini pindi watumishi wa wizara mbalimbali watakapohamia katika eneo hilo watabaini umuhimu wake.

Wakati huo huo Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Methew Mtigumwe alimueleza Waziri wa Kilimo kuwa ujenzi huo umefikia katika hatua za mwisho hivyo siku chache zijazo maandalizi ya kuhamia Ihumwa yatakamilika.

Aliwapongeza mafundi wanaoendelea na ujenzi huo kwa kuwa waaminifu na kukamilisha ujenzi wa majengo hayo kwa wakati muafaka.

Serikali kuhamia Dodoma ni sehemu ya kukamilisha safari iliyoanza miaka 42 iliyopita ya kuhamishia makao makuu ya Serikali mkoani Dodoma.

MWISHO
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com