Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akimkabidhi cheti,
Janeth Ibrahim miongoni mwa wanafunzi aliyehitimu darasa la saba katika
shule ya msingi ya Waja Springs wakati wa mahafali ya saba yaliyofanyika katika
shule hiyo iliyopo mkoani Geita.
Wahitimu
wa darasa la saba wa shule ya msingi ya WAJA Springs wakiwa pamoja na wanafunzi
wenzao wakiimba wimbo wa taifa mara baada ya mgeni rasmi, Naibu Waziri wa
Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu kuwasili katika shule hiyo kwa
ajili ya mahafali ya darasa la saba
Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akimkabidhi zawadi
mwanafunzi bora aliyekuwa akifanya vizuri kwenye masomo yake, Charles Zungu
kwenye mahafali ya darasa la saba katika shule ya msingi ya Waja Springs
iliyopo mkoani Geita.
Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Geita mjini,
Mhe.Constantine Kanyasu amewahimiza wazazi wenye watoto waliomaliza darasa la
saba mwezi huu nchini wahakikishe wanawalinda watoto hao wasijiingize
katika makundi yasiyofaa.
Akizungumza
kwenye mahafali ya saba ya wanafunzi 69 waliomaliza darasa la saba katika shule
ya msingi ya Waja Springs ya mkoani Geita,Mhe.Kanyasu amewataka wazazi wawe
mstari wa mbele katika malezi bora ya watoto wao
.Aidha,
Mhe.Kanyasu amewataka pia wahitimu hao wakawe mfano bora katika jamii kwa kuwa
kuwasaidia wazazi wao kwa kufanya kazi za majumbani badala ya kuacha kazi zote
zifanywe na Wafanyakazi wa ndani
Katika
hatua nyingine, Mhe. Kanyasu ameipongeza shule hiyo kwa kufanya vizuri katika
mitihani ya Taifa na kuufanya mkoa wa Geita kuwa miongoni mwa mkoa
inayokuwepo kwenye tano bora kitaifa.
Pia,
Mhe.Kanyasu amewataka wanafunzi hao watumie muda mwingi kujisomea vitabu vya
hadithi badala ya kutumia muda mwingi kuangalia Televisheni hasa vipindi
visivyofaa
Katika
hatua nyingine, Mhe.Kanyasu ameuhakikishia Uongozi wa shule hiyo kutafuta
ufumbuzi wa tatizo la barabara iinayoelekea katika shule hiyo pamoja tatizo
maji machafu wakati mvua ikinyesha .
Kwa
upande wake Meneja wa Shule hiyo, Mhandisi.Chacha Wambura amewaasa wazazi
kujiepusha kuwapatia simu watoto wao ili wasiweze kuingia katika vishawishi
katika kipindi hili kifupi walichohitimu masomo yao.
"
Wazazi jiepusheni kuwapa simu zenu hawa watoto, hii mitandao ya kijamii
inawapelekea watoto kuanza kuangalia mambo yasiyofaa " alisisitiza
Wambura.
Aidha,
Amewataka Wahitimu hao waache kuzitumia simu za wazazi wao pindi wakiwa
majumbani badala yake wasome vitabu kama walivyokuwa wakifundishwa shuleni
Naye,
Janeth Ndibalema ambaye ni mzazi wa mhitimu wa darasa la saba, Amesema malezi
ya watoto kwa sasa yamekuwa na changamoto nyingi kutokana na wazazi kuacha
jukumu la malezi kwa Wasichana wa kazi hali inatopelekea watoto
wengi kuharibikiwa.
Kufuatia
hali hiyo, Ndibalema ametoa wito kwa wazazi kutenga muda kukaa na watoto wao
badala ya kujikita kwenye majukumu ya kazi ili kuwasaidia watoto wao kujiepusha
kufanya mambo yasiyofaa yatakayowafanya wasiweze kuendelea na shule.
0 comments:
Post a Comment