Waziri wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga (Mb)
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mhandisi Mathew Mtigumwe anapenda
kuwataarifu Wakuu wa Taasisi za Utafiti katika Sekta ya Kilimo pamoja Watendaji
Wakuu wa Sekta Ndogo ya Mazao ya Kilimo na Sekta Binafsi kwamba, kutakuwa na
Mkutano Maalum baina ya Waziri wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga (Mb) na Wadau hao
utakaofanyika tarehe 11 Februari 2019 (kwa watafiti) na tarehe 12 Februari 2019
(sekta binafsi) kuanzia saa 4:00 asubuhi.
Mkutano huo utafanyika katika Ukumbi wa Kilimo I, Wizara ya
Kilimo, Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Kilimo atatumia Mikutano hiyo kubadilishana uzoefu
pamoja na kujadili mambo mbalimbali kuhusiana na maendeleo ya Sekta ya Kilimo.
Aidha, atapenda kufahamu mchango wa kila Taasisi na wadau wa sekta binafsi
katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za kilimo ikiwa ni pamoja na Programu
ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo Awamu ya Pili (ASDP II) pamoja na changamoto zilizopo
na utatuzi wake.
Imetolewa na:-
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Kilimo
DODOMA
Huu mkutano wa watafiti utahusu waliopo serikalini tu au wote?
ReplyDeleteHuu wa sekta binafsi (Feb12) una watu maalum au yeyote anaweza kuhudhuria?
Mm i nakuwaje wanao lima tusiwepo
DeleteNimuhimu sana kushiriki. Ngoja tufuatilie ikiwa naweza kushiriki mkutano huu muhimu.
ReplyDelete