Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Innocent Bashungwa (Mb) akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Muhunze kilichopo katika Wilaya ya Kishapu wakati wa ziara ya Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan Mkoani Shinyanga leo tarehe 28 Februari 2019. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Baadhi ya wananchi wakifatilia mkutano wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan wakati akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Muhunze kilichopo katika Wilaya ya Kishapu wakati wa ziara ya kikazi Mkoani Shinyanga leo tarehe 28 Februari 2019.
Naibu Waziri wa ardhi, Nyumba na Maendeleo ya makazi Dkt Angeline Mabula (Mb) akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Muhunze kilichopo katika Wilaya ya Kishapu wakati wa ziara ya Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan Mkoani Shinyanga leo tarehe 28 Februari 2019.
Kutoka kushoto ni Naibu Waziri wa Tawala za mikoa na serikali za mitaa TAMISEM Mhe Mwita Waitara, Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Innocent Bashungwa (Mb), Naibu Waziri wa Madini Mhe Stanslaus Nyongo wakifatilia mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Muhunze kilichopo katika Wilaya ya Kishapu wakati wa ziara ya Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan Mkoani Shinyanga leo tarehe 28 Februari 2019.
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Shinyanga
Serikali imeeleza kuwa imejipanga kuimarisha zao la Pamba ili
kuongeza uzalishaji nchini kwani kufanya hivyo wakulima watanufaika katika
uzalishaji wenye tija na kuimarisha biashara.
Ili kuongeza uzalishaji wa Pamba dhamira ya serikali ni kuanzisha
Pamba mbegu vipara ili kuondokana na utumiaji wa pamba manyoya ambayo
imezoeleka lakini tija yake ni ndogo katika uzalishaji kuliko Pamba Manyonya.
Naibu Waziri wa Kilimo ameyasema hayo leo tarehe 28 Februari
2019 wakati akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha
Muhunze kilichopo katika Wilaya ya Kishapu wakati wa ziara ya Makamu wa Rais
Mhe Samia Suluhu Hassan Mkoani Shinyanga.
Alisema kuwa elimu itatolewa kuhusu matumizi ya Pamba mbegu
vipara ili kuwajengea uelewa wananchi na serikali kufikia hatua ya kufungamanisha
kilimo cha Pamba na uchumi wa viwanda.
Mhe Bashungwa aliongeza kuwa serikali ya awamu ya tano
inayoongozwa na Mhe Rais Dkt JKohn Pombe Magufuli imejipanga kuhakikisha kuwa
kilimo kinawakomboa wananchi ili kuimarisha uchumi wa mtu mmoja mmoja na Taifa
kwa ujumla wake.
“Sisi kama Wizara tutakuwa na jukumu la kushawishi wawezaji ili
kuwekeza kwenye viwanda vya Pamba nyuzi pamoja na viwanda vya nguo na kufanya
hivyo tutakuwa tumetekeleza vyema maelekezo yaliyoainishwa kwenye ilani ya
Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi yam waka 2015-2020” Alikaririwa
Aidha, alisema kuwa Wizara ya Kilimo imejipanga vyema katika
kutafuta masoko ya mazao ya wakulima ambapo kwa upande wa zao la mahindi tayari
soko limepatikana kupitia Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) imesaini
mkataba wa mauziano ya mahindi ya Tani 36,000 na Mpango wa Chakula Duniani
(WFP).
Katika hatua nyingine alisema kuwa wakulima wa Wilaya ya
Kishapu ni miongoni mwa wakulima wa zao la Mtama hivyo kupitia Mpango wa
Chakula Duniani (WFP) serikali ya Tanzania inaendelea kujiridhisha uhitaji wa
mtama nchini Sudani Kusini ili kuwaunganuisha wakulima na soko hilo.
Katika hatua nyingine Naibu Waziri huyo ameiagiza Bodi ya
Pamba kuhakikisha viuadudu (Viuatifu) vinapatika haraka katika Wilaya ya
kishapu ili kuondoa haraka changamoto inayowakumba wakulima kwa kukosekana
viuatilifu kwa wakati.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment