
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey
Mwanri akiwahamasisha jana Madreva wa Bajaji na Bodaboda katika
Manispaa ya Tabora kujiunga na Mfuko wa Bima ya Afya ili waweze
kunufaika na huduma za matibabu.

Meneja wa Bima ya Afya Mkoa wa
Tabora Adam Salum akiwaelimisha jana Madreva wa Bajaji na Boda boda wa
Manispaa ya Tabora utaratibu wanaotakiwa kuchukua kujiunga na Bima ya
Afya ili waweze kupata matibabu pindi wanapokuwa wagonjwa.

Baadhi ya Madreva wa Bajaji na
Boda boda na wananchi wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Tabora (hayupo
katika picha) alipokuwa akiwaeleza umuhimu wa kujiunga na Bima ya Afya.
Picha na Tiganya Vincent
*********************************
NA TIGANYA VINCENT
UMOJA wa Madreva wa Bajaji na
Bodaboda Mkoani Tabora wameipongeza Serikali kwa kuwasaidia kuingia
katika Mfumo wa kupata huduma za matibabu kupitia Bima ya Afya.
Hatua hiyo itasaidia kuwapa fursa
ya kuokoa maisha yao wanapopata matatizo mbalimbali ikiwemo wanapopata
ajali na wakati mwingine kuugua.
Kauli hiyo imetolewa jana na
Makamu Mwenyekiti wa Madreva Bajaji Waziri Kipusi wakati wa ziara ya
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri ya kuwahamasisha Madreva Bajaji na
Bodaboda kujiunga na Bima ya Afya.
Alisema kabla ya kuanza kwa
utaratibu huo haujaanza walikuwa wakilazimika kusema uongo ili wenzao
waliopata ajali wapate matibabu.
“Ikitokea mwenzetu amepata ajali
na tunaposhindwa kuchangishana ilibidi wakati mwingine tusema uongo ili
tumuoke mwezetu aliyepata majanga… na wakati mwingine tuliwadanganya
Maafisa Ustawi wa Jamii ili watupe kibali cha kupata matibabu kwa mkopo
wa matibabu” alisema.
Naye Mwenyekiti wa Umoja wa
Madreva Bajaji Mkoa Said Maganga alisema kuwa hatua hiyo itasaidia
kuwawezesha kuwa na uhakika wa kupata matibabu wakati wote na kuendelea
na shughuli za kujiingizia kipato.
Kwa upande wa Mkuu wa Mkoa Aggrey
Mwanri aliwataka Vijana wote wanaojihusisha na usafirishaji wa abiria
kwa kutumia Bajaji na Pikipiki maarufu kama bodaboda kuchangamkia fursa
hiyo iliyotolewa kwao na Serikali ya awamu ya tano.
Alisema kupitia utaratibu huo
watanufaika kwa kupata huduma za Bima ya afya kwa kuchangia shilingi
100,000/- kwa mwaka badala ya ule wa mtu mmoja kulipa shilingi 1.5 kwa
mwaka ili kupata huduma hizo.
Mwanri alisema Serikali imeamua
kuwapunguzia mzigo kwa wale Bodaboda na Bajaji ambao watakuwa wako
katika umoja ili waweze kupata huduma za afya kwa gharama nafuu.
Naye Meneja wa Bima ya Afya Mkoa
wa Tabora Adam Salum alisema siku za nyuma Mfuko wa Bima ya Afya ulikuwa
ukihudumia watumishi wa umma pekee lakini hivi sasa umeiongia makundi
mbalimbali kama vile Wajasiriamali , Umoja wa Boda boda na Bajaji.
0 comments:
Post a Comment