Na Mathias Canal,
Wizara ya Kilimo-Dar es salaam
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) leo tarehe 12
Januari 2019 amekutana na kufanya mazungumzo na wadau wa kuendeleza tasnia ya
mbegu nchini.
Katika Kikao kazi hicho kilichofanyika katika Ukumbi wa
Wizara ya Kilimo maarufu kama Kilimo I Jijini Dar es salaam pamoja na wadau
kutoka Wakala wa Mbegu za Kilimo (ASA), Taasisi ya kudhibiti ubora wa mbegu (TOSCI),
na Taasisi ya utafiti Tanzania (TARI), vilevile walialikwa wadau kutoka Bill
& Melinda Gates kupitia kampuni ya ushauri ya mradi wa AGRI Experience.
Akizungumza katika kikao kazi hicho Waziri wa Kilimo Mhe
Japhet Hasunga alisisitiza kuwa serikali imedhamiria kuleta mapinduzi ya kilimo
kwa kuongeza tija katika uzalishaji kwa kuongeza matumizi ya teknolojia ikiwemo
mbegu bora.
Alisema pamoja na mambo mengine serikali ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Mhe Dkt John Pombe Magufuli imjidhartiti
katika kuhakikisha kuwa nchi inajitosheleza kwa mafuta ya kula na hivyo
serikali inataka mradi huo kuondoa chanagmoto katika sekta ya mbegu kwa
kuzalisha mbegu za mafuta hasa za alizeti na michikichi.
Mhe Hasunga amewapongeza wadau kutoka Bill & Melinda
Gates kupitia kampuni ya ushauri ya mradi wa AGRI Experience kwa ushirikiano na
serikali ya Tanzania kutekeleza mradi huo.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment