Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akipata maelezo ya kina juu ya maendeleo ya ujenzi wa Ofisi ya Makamu wa Rais
Ihumwa Dodoma kutoka kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na
Mazingira Mhe. January Makamba (kushoto). (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikagua maendeleo ya ujenzi wa Ofisi ya Makamu wa Rais Ihumwa Dodoma akiwa pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba (kushoto) na Katibu Mkuu wa ofisi hiyo Mhandisi Joseph Malongo. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimwagilia maji mti wa kumbukumbu mara baada ya kuupanda katika eneo ambalo Ofisi ya Makamu wa Rais inajengwa Ihumwa Dodoma (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).
Ujenzi wa Jengo la Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira ukiendelea kwa kasi nzuri Ihumwa Dodoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan amesema Ofisi ya Makamu wa Rais itakuwa ya mfano katika kutunza
mazingira.
Makamu wa Rais ameyasema hayo leo mara baada ya kukagua maendeleo ya
ujenzi wa Ofisi ya Makamu wa Rais Ihumwa, Dodoma.
“katika kupamba maofisi yetu kwa miti sisi ni watu wa
mazingira kwetu kuwe mfano wengine wakipita waseme kaangalieni ofisi
ya Makamu wa Rais kulivyo kwa hiyo miti yetu tuitunze na bustani zimwagiliwe”alisema Makamu wa
Rais.
Kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na
Mazingira Mhe. January Makamba amesema ofisi yake imejitahidi kwa kadri ya
uwezo wake kutekeleza maelekezo waliyopewa pamoja na kupanda miti katika eneo
hilo.
Wakati huo huo Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Joseph
Malongo alimueleza Makamu wa Rais kuwa Wizara zote zimepewa kiasi sawa cha pesa
hivyo Makatibu wa Kuu walikaa na kukubaliana mchoro utakaotumika kama ofisi.
Akitoa maelezo kwa Makamu wa Rais, Katibu Kamati ya Taifa ya
Kuratibu Mpango wa Serikali Kuhamia Dodoma Bw. Meshach Bandawe alisema kuwa
tangia uamuzi ulivyopitishwa na Serikali ujenzi ulianza mara moja kwa ofisi 21
pamoja na ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali pamoja na taasisi zingine na
Ofisi ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na eneo linalojengwa ofisi hizo
limeshalipiwa fidia, na umeme umeshasambazwa, kwa sasa majengo yanayojengwa
ofisi za chini lakini kila kiwanja kina eneo la kujenga ghorofa.
0 comments:
Post a Comment