Naibu Waziri wa
Kilimo Mhe Omary Mgumba yupo kwenye ziara ya kikazi ya siku nane (8) kuanzia tarehe
07 Januri mpaka tarehe 14 Januari 2019 kwenye Mikoa ya Kilimanjaro, Morogoro na
Pwani yenye Lengo la kuhamasisha uzalishaji na tija wa Miwa na Sukari ili
kumaliza tatizo la upungufu wa Sukari Nchini.
Naibu Waziri huyo
amesema kuwa Tanzania ina miaka 57 ya Uhuru lakini kama Taifa halijawahi
kujitosheleza kwa Sukari badala yake inaagizwa toka nje ya nchi wakati uwezo wa
kuzalisha upo, ardhi na Rasilimali watu zote zipo hivyo jambo hilo linapoteza
fedha za kigeni na ajira kwenda nchi zingine.
Alisema kuwa Serikali
imeazimia kubaini sababu na changamoto zinazokabili sekta ya Sukari, wadau,
Wakulima wadogo na wakubwa wa miwa na wawekezaji wa viwanda vya sukari nchini
ili kwa pamoja kuwa na mkakati kabambe wa kukamilisha upungugu huo ndani ya
muda mfupi.
Kwa sasa Mahitaji
ya Sukari nchini yanakadiriwa kufikia zaidi ya Tani 670,000 Mts kwa pamoja ya
Sukari ya Mezani na viwandani. Sukari ya Mezani ni Tani 515,000 na Sukari ya
Viwandnai Tani 155,000 Mts.
Uwezo wa Viwanda
vya ndani ni kuzalisha ni Tani 350,000 Mts na kuwa na upungufu wa Tani 320,000 Mts
za Mezani na Viwandani kiasi ambacho kinaagizwa kila mwaka toka nje ya nchi.
Katika ziara hiyo Mhe
Mgumba amewahimiza wakulima kuzalisha zaidi na kuwaomba wawekezaji waliopo
kupanua uwezo wa viwanda vyao ili kuongeza uzalishahi na kuwahamasisha pia
wakulima kuongeza uzalishaji wa kilimo na kuwaomba wawekezaji wengine wa ndani
na nje ya nchi kutumia fursa hiyo kuwekeza nchini kwa sababu soko lipo na
mazingira ya Biadhara yanaendelea kuboreshwa kila siku.
Katika Ziara hiyo
Mh Mgumba aliambatana na Mhe Joseph Kakunda ambaye ni Waziri wa Viwanda, Biashara
na Uwekezaji mwenye dhamana ya kusimamia sekta ya viwanda nchini.
Baada ya ziara hiyo
watatembelea pia Mkoani Kagera kwa lengo kama hilo ili kuweza kufahamu
changamoto za wadau wote katika sekta hiyo.
0 comments:
Post a Comment