Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe wakati
alipozindua X-Ray ya kidigitali kwenye hospitali ya Rufaa ya mkoa wa
Ruvuma, Januari 5, 2019. Kulia ni Naibu Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt, Faustine Ndugulile na kushoto
ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Christina Mndeme. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akiongozwa na Kaimu Mganga
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Majura Magafu (kulia)
kukagua ukarabati wa jengo la wakinamama wajawazito wanaosubiri
kujifungua katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Ruvuma mjini Songea,
Januari 5, 2019. Wapili kulia ni Naibu Waziri wa
Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulie na
kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Christina Mndeme. (Picha na Ofisi ya Waziri
Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpa pole mtoto, Patric
Chenya wakati alipotembelea wodi ya watoto katika hospitali ya Rufaa
ya Mkoa wa Ruvuma mjini Songea, Januari 5, 2019. Kulia ni Waziri wa
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kuhusu Mashine ya
Kidigitali aliyoizindua katika hospitali ya Mkoa wa Ruvuma kutoka Mtalaam
wa tiba ya mionzi (Medical Technologist), Lincleth Gingo kwenye hospitali ya
Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma mjini Songea, Januari 5,2019. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa
wa Ruvuma, Christina Mndeme na wapili kushoto ni Naibu Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Wtoto, Dkt. Faustine Ndugulile. (Picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza baada ya kuzindua mashine ya X-
Ray ya Kidigitali kwenye hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma mjini Songea,
Januari 5, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Ni la
wajawazito wanaosubiri kujifungua, limegharimu sh. milioni 129
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amenusa
harufu ya ufisadi katika mradi wa ukarabati wa jengo la mama na mtoto
katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma (HOMSO) na amesema kwamba
hajaridhishwa na kiasi ya sh. milioni 129 zilizotumika.
Hivyo,
amemuagiza Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Dkt.
Faustine Ndungulile afuatilie suala hilo ili kumbaini mtu ambaye amehusika
katika kupitisha zabuni ya ukarabati wa jengo hilo na kisha kumpelekea taarifa.
Waziri
Mkuu amenusa harufu ya ufisadi katika mradi huo leo (Jumamosi, Januari 5, 2019)
wakati alipotembelea hospitali hiyo na kukagua ukarabati wa jengo la akinamama
wajawazito wanaosubiri kujifungua (mama ngojea) ambalo umegharimu sh. milioni
129.
“Sijaridhishwa
na gharama za ukarabati wa jengo hilo kutokana na kiasi kikubwa cha fedha
kilichotumika kwani Serikali inajenga vituo vya afya vyenye jengo la maabara,
jengo la kujifungulia, wodi ya mama na mtoto, chumba cha upasuaji, nyumba ya
watumishi kwa gharama za sh. milioni 400 hadi 500 sasa inawezekajane jengo moja
linalokarabatiwa ligharimu kiasi hicho.”
Waziri
Mkuu amesema kila mtumishi wa umma lazima azingatie maadili ya kiutumishi na
kutekeleza maelekezo yote yanayotolewa na Serikali. Amesema Serikali imeagiza
miradi ijengwe kwa kutumia force accountna kuhakikisha miradi
inalingana na thamani ya fedha.
Kadhalika,
Waziri Mkuu amewaagiza wakuu wa mikoa na wilaya kusimamia kikamilifu utoaji wa
huduma ya watoto waliochini ya miaka mitano zinazotolewa katika hospitali kwani
baadhi ya wahudumu wa afya wamekuwa wakiwatoza gharama za dawa wakati
wanatakiwa watibiwe bure.
Waziri
Mkuu amesema hayo baada ya Kanisia Fusi ambaye amelazwa na mtoto wake katika
hospitali hiyo kumueleza kwamba ameandikiwa dawa na kuambia akanunue wakati
mtoto wake mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu anatakiwa atibiwe bure.
Pia
baada ya Dkt. Ndungulile kuangalia cheti cha mtoto huyo alisema dawa
aliyoandikiwa ipo hospitalini hapo jambo ambalo lilithibitishwa na Mganga
Mfawidhi wa hopitali hiyo Dkt. Majura Magafu, hivyo Waziri Mkuu amemuagiza
mganga huyo amtafute mtendaji aliyemuambia mama huyo akanunue.
Wakati
huo huo, Waziri Mkuu amezindua mpango wa usambazaji wa
x-ray za kidigitali ambazo zitazambazwa kwenye hospitali mbalimbali za rufaa za
mikoa ili kuboresha utoaji wa huduma zinazotolewa kwa njia ya mionzi.
Waziri
Mkuu amesema kwa kuanzia x-ray hizo zitasambazwa kwenye hospitali za rufani
katika mikoa 11 na kisha baadae zitasambazwa kwenye hospitali zingine 20, lengo
ni kuhakikisha hospitali zote za rufaa za mikoa zinakuwa na x-ray hizo.
Kwa
upande wake, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia na Watoto, Dkt. Ndungulile amesema Serikali ya Awamu ya Tano
inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli imeendelea kutoa kipaumbele katika
kuboresha huduma za nchini.
Amesema
lengo la Serikali ni kuhakikisha huduma za afya zinawafikia Watanzania wote
karibu na maeneo yao ya makazi tena kwa gharama nafuu. ”Katika kufikia azma hii
moja wapo ya kipaumbele ni kununua vifaa vya kisasa vinavyoendana na teknolojia
iliyopo.”
Amesema
kwa sasa wizara hiyo imenunua mashine 11 za x-ray za kidigitali zenye thamani
ya zaidi ya shilingi 2,027,029,794.60 ambazo zimekusudiwa kupelekwa kwenye
hospitali 11 zenye x-ray za zamani. Hospitali hizo ni Amana, Bukoba, Katavi,
Morogoro, Njombe, Ruvuma, Simiyu, Singida na zingine tatu zitafungwa katika
hospitali za wilaya za Chato, Magu na Nzega.
0 comments:
Post a Comment