Ikumbukwe siongei kwa niaba ya Taasisi Fulani bali naongea
kama MNEC. Napenda kumpongeza Rais wangu Dr. John Pombe Joseph magufuli kwa
uchapakazi wake anaouonesha siku hadi siku kwani katika kipindi kifupi Mh. Rais
amejipambanua kutatua shida za wananchi, tumeshuhudia miundo mbinu inayojengwa
siku hadi siku, ufufuaji wa shirika la ndege Tanzania (ATCL), anajenga
hospitali, ujenzi wa reli ya kisasa (SGR), ujenzi wa barabara za juu na wapo watu
wanaosema maendeleo ya watu kwanza ila niwaambie hakuna maendeleo ya watu
pasipo maendeleo ya vitu nikimnukuu Rashid NM, and Ngalawa F 2016 katika
kulinganisha kwao logistic industry ya Tanzania na turkey walisema kukua kwa
miundombinu ya Tanzania na sekta ya usafiri ni msingi kwa maendeleo ya Taifa.
Sasa watu wasiongee bila ya kusoma tusiwapoteze watanzania
katika ramani ya kumtia Moyo Rais wetu kipenz Dr. magufuli na niwaambie
sitawavumilia tena kuzungumza uongo wenu, kejeli zenu na mipasho yenu.
Tumuunge mkono Rais wetu, uzalendo hauna bei mimi
namfananisha huyu mzalendo magufuli kama Mussa katika biblia maana Mussa
alipopewa kazi na Mungu aliifanya kwa moyo wote huku akilaumiwa na wana wa
Israel waliokuwa wakitolewa misri kwenda kanani, niseme tu Rais Magufuli ndio
mtu sahihi wa kutupeleka katika nchi yenye maziwa na asali na Tanzania yenye
neema inakuja na imeshaanza kuja, tunapobadilika kutoka sehemu tuliyozoea kuja
mpya lazima tuumie kidogo ila tunaumia kwa manufaa ya taifa, kwa ajili ya
vizazi vyetu vijavyo, mimi sitokuwa tayari watoto wangu kufukua mifupa yangu
siku nakuwa marehemu na kusema baba wewe ulikuwa wapi kutomtetea Rais magufuli
wakati anatukanwa, siko tayari kupigwa viboko na wanangu siku ninapokuwa siko
hapa duniani. TUMUUNGE MKONO
1. Niwashukuru mahakama kuu kutupilia mbali shauri batili la
muungano wa vyama vya siasa uchwara, hawa wanaojiita wapinzani lakin kiuhalisia
sio wapinzani wenye tija, wanaupinga sana huu muswada na kusema unampa mamlaka
makubwa msajili wa vyama vya kisiasa mimi nauona muswada huu hauna shida kabisa
na wao wanaukataa sababu unawabana juu ya pesa za uma walizozoea kuzitumbua,
pesa zilikuwa zikitumika kiholela sasa msajilli atakuwa na jicho la karibu hili
ndio linalowafanya waukatae muswada ila wanatumia sababu zingine zisizo na
tija, zito na wenzake wanalia wakijua biashara zao za kuzitafuna hizi pesa
kihasara hasara ndio mwisho wake.
Shauri walilolipeleka linakiuka kifungu 8 (2) cha sharia za
haki za msingi na wajibu sababu hawakufuata taratibu ‘mtu yoyote anayedai haki
zake zinakiukwa ama zinaelekea kukiukwa anapaswa kutafuta nafuu kwa kutumia
njia nyingine zilizopo kwanza kabla ya mahakamani’ sasa zito kama kawaida yake
moja kwa moja akakimbilia mahakamani kutafuta huruma ya wananchi kupitia vyombo
vya habari, alidhani ataiyumbisha mahakama yetu, ila nawapongeza muhimili huu
muhimu wa sheria kwa hili jambo kwani wamefanya jambo zito sana na zuri
niwaombe mahakama kufanya kazi kwa misingi na taratibu za kisheria.
2. Nimpongeze CAG kwa kuitikia wito wa bunge kwani kauonesha
ukomavu mkubwa na wenye tija kweli kupita maelezo sasa zito aache kufuatilia
mambo yasiyomuhusu asiwe ni mtu anayefanya siasa za matukio kama ameshindwa
siasa arudi nyumban na nimhakikishie zitoo mwaka 2020 harudi bungeni, kwa mfano
hili jambo la CAG aliiomba mahakama imlinde CAG sasa mimi nizishauri mamlaka
zote na vyombo vyote kuwa yoyote yule bila kujali nyadhifa yake akienda popote
na kutukana taasis yoyote kama taifa wasimvumilie na kama ningekuwa na mamlaka
ningeanza na huyu Lissu anavyoropokaropoka huko nje ya nchi, ningepambana nae
kisawasawa.
3. Zitto Amani tuliyonayo Tanzania ni kubwa sana na
watanzania tumekuwa tukifurahia hii amani tuliyonayo sasa tabia yako ya
kujifungia chumbani na kutunga unataka kuuliwa tabia hiyo ikome mara moja, maana
imekuwa ni kawaida yako kuvibuni hivi vitu, usalama wa taifa wanapambana
kuhakikisha taifa tuko salama katika kila Nyanja, kazi wanayofanya ni nzuri
nakuomba uache kutengeneza hofu katika akili za watu unasema umetishiwa kuuwawa
sisi tutajuaje kama umetishiwa ama umetunga tupe ushahidi tujihakikishie na
nikukumbushe bungeni palikuwa na wananchi wa kawaida wengi tu wakulima, wafanya
biashara kama aliyekuambia hivyo alikuwa mwananchi wa kawaida tena mwananchi
wako wa kigoma kukuambia dawa yako ni kukuua maana hauna tija katika jimbo lako
sisi tutajuaje? Lakini kuua haina maana moja ipo maana nyingine ya mtu kuuliwa
kisiasa yani kumalizwa hivyo nenda tumikia wananchi wako nina uhakika kama
uliambiwa vile basi yamkini ni mwananchi wako wa kigoma ila bungeni hawakuwa ma
afisa usalama tu bali walikuwa watu mchanganyiko mchanganyiko kutokana na
shuguli yenyewe ya kupokea maoni.
4. Huu muswada wa vyama vya siasa upo mpango mkakati wa
baadhi ya mabeberu ambao wamewekeza katika pesa zao kuhakikisha wabunge
wanashawishiwa kutoupitisha mimi niwaambie taarifa zenu zipo, account mlizoanza
kuingiziwa hizo fedha tunazijua. Hivi hamuwezi kufanya mambo bila kuwategemea
hao mabeberu? wanataka nini na Tanzania kwanini hawafanyi haya mambo kwao
niwakumbushe tu hakuna anayetoa pesa akiwa hana malengo na pesa yake hizo pesa
mtagawana ila adhma yenu mbovu itashindwa na huo ndio ukweli. Nia njema
itashinda daima na nia ya huu mswada ni njema huu muswada utakuwa sheria hakuna
namna.
5. Tundu Lisu Tundu Lisu Tundu Lisu nimekuita mara tatu
nataka nikuambie wanasingida hawajakuchagua ufanye ziara katika nchi za wenye
nia mbaya na Tanzania, filamu mnazotuchezea zimekosa weledi kwa waandishi
walioandika script hizo, nikuambie tu huko uliko hautafaidika na lolote ni
vyema utambue Tanzania ni nchi huru tulishakombolewa kutoka kwa mkoloni sasa
tumebaki kujikomboa kiuchumi kama taifa, umekosa uzalendo na utaifa na kuamua
kuitukana ardhi inayojua shida zako zote na ardhi utakayozikwa siku ukifa,
mwanaume hatukani katika nchi anazofadhiliwa, kama wewe kidume rudi Tanzania na
utukane ukiwa Tanzania hapo ndipo tutajua wewe ni mwanaume wa shoka, nikuase
uache tamaa na unayoendelea nayo katika nchi za watu, usitutusi kwa haki za
binadamu na demokrasia angali wewe unao uhuru wa kututukana pindi ukija Tanzania,
sasa nimepigiwa simu na wananchi wako wanataka nikawe mbunge wao sasa nikuambie
tu endapo ukichelewa nakuhakikishia nitakuwa mbunge.
Wako mtiifu
MUSSA MWAKITINYA – MNEC
Tunahitaji wabunge wenye uelewa mkubwa wa jamii ya Tanzania ukoje na inahitaji nini. Tanzania hatuhitaji aina ya demokrasia ambayo inahubiriwa duniani kote lakini hata mwanzilishi wake haifuati ipasavyo. Tanzania tunahitaji Uchumi wetu uwe wa kati, elimu iboreshwe, miundombinu iimarishwe ili hata bibi yangu kule kwimba mwanza aone manufaa yake. Atafaidi nini na ushoga,maandamano, mikutano ya kisiasa isokuwa na tija. Yemba bin Yemba
ReplyDeletesafi sana , taifa tunaitaji watu wazalendo kama wewe na kuwambia ukweli hawa vibaraka wasio jua mema katika nchi hii, mh jpm achape kazi wafia nchi tupo nyuma yake daima.
ReplyDeleteHaha unaweza kupata cheo kazana mnec
ReplyDelete