Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko (wa pili) akifuatiwa na Katibu Mkuu wa Madini Prof. Simon Msanjila wakitoka katika jengo la ofisi za mwekezaji wa hifadhi za wanyamapori ya Makao, Mwiba Limited kuelekea eneo linalosadikiwa kuendesha shughuli za Uchimbaji hifadhini humo.
Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (wakwanza kulia) akifuatiwa na Katibu Mkuu wa Madini, Prof. Simon Msanjila na wajumbe aliambatana nao wakiwa katika eneo linaloonesha dalili za uchimbaji wa madini katikati ya hifadhi ya wanyama ya Makao wilayani Meatu
Aeleza itafika kokote madini
yanakochimbwa pasipo vibali halali
Na Nuru Mwasampeta
Naibu
Waziri wa Madini, Doto Biteko amewaeleza watanzania wasiofuata Sheria katika utafutaji,
uchimbaji na biashara ya madini nchini kuwa Serikali inaona na itafika popote
madini yanapochibwa pasipo vibali halali vya kufanya shughuli hiyo.
Biteko
ameyasema hayo mwishoni mwa wiki, Tarehe 5 mwezi Januari, 2019 alipofanya ziara
ya kukagua eneo ambako shughuli za uchimbaji wa madini ya shaba ulifanywa
pasipo kibali na kubaini viashiria vya uchimbaji katika hifadhi ya Wanyama pori
ya Makao iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Meatu Mkoani Simiyu.
Akizungumzia
lengo la ziara hiyo, Biteko alisema kumekuwa na viashiria vya kuwepo kwa watu
wasiokuwa waaminifu na kujiingiza katika shughuli ya uchimbaji pasipokuwa na
vibali jambo ambalo halikubaliki na halitavumilika. “Sisi madini yanatuuma,
tukisikia kuna watu wanachimba tutafika mahali popote kujua madini hayo
yanachimbwa na kupelekwa wapi” Biteko alikazia.
Aliendelea
kwa kusema, huu mchezo ulifanyika sana na sasa nimekuja kuwaambia hautajirudia
tena. Endapo mtu yeyote anataka kuchimba madini ya yoyote ikiwa ni pamoja na madini
ya ujenzi kama vile mchanga wa kutengenezea barabara sharti afike katika ofisi
zetu za madini aeleze nia na eneo analotakiwa kutengeneza barabara na wahusika
watamuonesha eneo la kuchimba mchanga kwa utaratibu wa kisheria kwa matumizi
hayo si kujiamlia tu.
Biteko
alisisitiza kuwa lengo la ziara hiyo si kutoa kibali kwa watu kuchimba katika
hifadhi hiyo. “Sisi hatujaja kupromote watu wachimbe bali tumekuja
kwa sababu watu wanachimba pasipo taratibu.
Alibainisha
kuwa ili mtu yeyote apate kibali cha kuchimba katika hifadhi hiyo sharti apate
kibali kutoka mamlaka kuu nne ambazo ni Wizara ya Maliasili na Utalii, Wizara
ya Maji kwa sababu katika hifadhi hiyo kuna vyanzo vya maji, Mamlaka ya
Mazingira (NEMC)pamoja na Wizara ya Madini.
Katika
ziara hiyo ya kushtukiza Biteko aliambatana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini,
Profesa Simon Msanjila aliyeelezea sheria na taratibu zinazopaswa kufuatwa ili
mtu yeyote kuweza kujihusisha na shughuli za Madini.
Aidha,
Profesa Msanjila aliwataka watanzania kujua kuwa rasilimali madini
zinazopatikana nchini ni kwa manufaa ya watanzania wote hivyo ni lazima wafuate
utaratibu ili mapato yatokanayo na tozo mbalimbali kutokana na utafiti,
uchimbaji na biashara ya madini ziwanufaishe watanzania wote. “Lazima niwaambie
haya madini ni ya watanzania wote” alikazia.
Akizungumzia
chanzo cha taarifa ya kuwepo kwa uchimbaji katika hifadhi hiyo Leons Welenseile
(Mjiolojia) alisema mnamo mwaka 2016 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu alifanya ziara
iliyolenga kutatua mgogoro baina ya kampuni ya inayomiliki leseni ya uwindaji
wanyamapori katika hifadhi hiyo Mwiba Holdings Limited na wananchi wanaozunguka
hifadhi hiyo baada ya wananchi kutoridhishwa na kile walichokuwa wakikipata
kutoka kwa mwekezaji huyo.
Walipokuwa
njiani kutoka katika kusuluhisha mgogoro huo ndipo wataalamu wa madini katika
mkoa huo walikutana na loli lililobeba mchanga pasipokuwa na vibali halali vya
kufanya uchimbaji huo nakubaini kuwa
shughuli hiyo ilikuwa ikifanywa na kampuni hiyo ya mwiba kwa lengo la
kukarabati barabara katika hifadhi hiyo pasipo kujua kuwa walipaswa kuwa na
leseni ya kuchimba mchanga huo na kupigiwa hesabu iliyopelekea kulipa mrabaha
wa milioni 50 baada ya kukiri kufanya shughuli hiyo kwa muda mrefu.
Kwa
upande wake Mkuu wa Wilaya ya Meatu Dkt. Joseph Eliaza Chilongani alikiri
kutokuwa na taarifa za uchimbaji huo na kuwataka wataalamu na maafisa madini
katika eneo lake kutoa taarifa pindi masuala ya ukiukwaji wa taratibu na sheria
za nchi yanapotokea katika eneo lake ili kuweza kushirikiana katika kutatua
changamoto hizo.
0 comments:
Post a Comment