Na mwandishi wetu
Balozi wa Morocco nchini Tanzania, Mheshimiwa Abdelilah Benryane
ametembelea Ofisi za Benki
ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) ili kufuatilia utekelezaji wa
Mkataba wa Ushirikiano uliosainiwa kati ya Serikali ya Tanzania
na Morocco wakati wa Ziara ya Mfalme wa Morocco Mtukufu Mohammed VI
alipotembelea nchini Tanzania mwezi Oktaba mwaka jana.
Mheshimiwa Benryane
ambaye alifuatana na uongozi wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo ya Morocco
(GCAM), ulioko nchini kwa ajili ya kikao cha pamoja cha ushirikiano na
kufuatilia utekelezaji wa miradi ya kilimo inayotekelezwa kati ya Benki
hiyo na TADB.
Akizungumza
wakati wa kikao cha pamoja kati ya GCAM na TADB, Mheshimiwa Benryane
alisema kuwa utekelezaji wa makubaliano kati ya Mfalme wa Morocco na
Rais Dkt. John Pombe Magufuli yanaendelea vizuri na kutolea mfano
mashirikiano kati ya benki hizo mbili kwa upande wa miradi ya kilimo.
“Ni
chini ya mwaka mmoja tangu viongozi wetu wakubaliane utekelezaji wa
mikataba 21 katika nyanja mbalimbali zikiwamo za kilimo, gesi, madini na
na usafiri wa anga,” amesema.
Kwa
upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga
aliishukuru GCAM kuichagua TADB kusimamia miradi ya utekelezaji wa
makubaliano hayo kwa upande wa kilimo.
Kwa
mujibu wa Bw. Assenga, pamoja na kupanga mikakati hiyo, ujumbe huo
ulipata fursa ya kukagua miradi kadhaa ya kilimo na ufugaji ambayo
Tanzania inaweza kuianzisha kwa mafanikio.
TADB
imeanzishwa kwa malengo makuu ya Kusaidia upatikanaji wa utoshelezi na
usalama wa chakula ambao ni endelevu nchini Tanzania; na Kuchagiza na
kusaidia Mapinduzi ya Kilimo kutoka
kilimo cha kujikimu kwenda cha kibiashara ili kuchangia kwenye ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini.
0 comments:
Post a Comment