Wadau wa elimu na viongozi mbalimbali wa mkoa wa Simiyu wakichangia katika harambee ya kuchangia ujenzi wa vyumba vya madarasa wilayani Busega, iliyofanyika Mjini Nyashimo lengo likiwa ni kukabiliana na changamoto ya vyumba vya madarasa wilayani humo.
Mkuu wa Wilaya ya Busega Mhe. Tano Mwera (kushoto) na Mbunge wa Busega,Mhe. Dkt. Raphael Chegeni wakiteta jambo katika harambee ya kuchangia ujenzi wa vyumba vya madarasa wilayani Busega, iliyofanyika Mjini Nyashimo lengo likiwa ni kukabiliana na changamoto ya vyumba vya madarasa wilayani humo.
Kutoka kushoto Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini, Mkuu wa Wilaya ya Maswa, mhe. Dkt. Seif Shekalaghe na Mbunge wa Jimbo la Busega, Mhe. Dkt. Raphael Chegeni wakiteta jambo, katika harambee ya kuchangia ujenzi wa vyumba vya madarasa wilayani Busega, iliyofanyika Mjini Nyashimo lengo likiwa ni kukabiliana na changamoto ya vyumba vya madarasa wilayani humo.
Na Stella Kalinga, Simiyu
Wadau
mbalimbali wa elimu wamechangia ujenzi wa vyumba vya madarasa katika
Halmashauri ya Wilaya ya Busega mkoani Simiyu katika Harambee iliyofanyika
Mjini Nyashimo, ambapo zimepatikana jumla ya shilingi 254, 969,000/= fedha
taslimu zikiwa ni shilingi 15,360,000/= ahadi shilingi 241,809,000/= na mifuko
ya saruji 127.
Akiongea
na wadau hao Mwakilishi wa Mkuu wa Majeshi Jenerali Venance Mabeyo ambaye
alialikwa kama Mgeni rasmi wa Harambee hiyo, Luteni Kanali Josephat Mshashi,
Mkuu wa Kikosi cha 27 Makoko Musoma amesema upo umuhimu wa kuhakikisha watoto
wanapata elimu kwa kuwa elimu ni urithi hivyo kila mmoja awe na uchungu wa
kuona watoto wanasoma.
“Hakuna
urithi tunaoweza kuwapa watoto wetu zaidi ya elimu tusipowapa elimu rasilimali
zote ambazo tunazipigania leo hii, tunavyopambana kulikomboa Taifa letu
kiuchumi itakuwa kazi bure kwa sababu tutabaki na Taifa la watu ambao ni
watumwa wa watu wenye elimu” alisema Mshashi
Awali
akitoa taarifa ya hali ya vyumba vya madarasa Mkurugenzi Mtendaji wa
Halmashauri ya Wilaya ya Busega, Bw. Anderson Njinginya amesema halmashauri
hiyo ina upungufu wa vyumba vya madarasa 107.
Mmoja
wa Wadau wa elimu katika Wilaya ya Busega, Bw. Deo Kumalija ambaye alichangia
katika harambee hiyo ametoa wito wadau wa maendeleo na wananchi kuchangia
shughuli za maendeleo katika maeneo waliyopo, ikiwemo ujenzi wa shule kwa kuwa
maendeleo yao yataletwa na wao wenyewe.
Naye
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka ameupongeza uongozi wa wilaya ya
Busega kuandaa harambee hiyo huku akiwataka kusimamia fedha zilizopatikana, ili
zifanye kazi iliyokusudiwa, na kuwasisitiza wazazi, walezi na jamii yote kwa
ujumla kuhakikisha wanafunzi wote waliochaguliwa kwenda kidato cha kwanza
wanaenda shule.
“Nawapongeza
sana viongozi wa wilaya ya Busega wakiongozwa na Mhe. DC kwa kuandaa harambee
hii, fedha hizi mhakikishe zinasimamiwa vizuri na zifanye kazi iliyokusudiwa,
lakini pia mhakikishe watoto wote waliochaguliwa wanaenda shule, haiwezekani
juhudi kubwa namna hii ifanyike kuchangia halafu watoto wasiende shule” alisema
Mtaka.
Mkuu
wa Wilaya ya Busega Mhe. Tano Mwera amemhakikishia Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.
Anthony Mtaka kuwa Viongozi watasimamia fedha yote iliyopatikana na kuhakikisha
inafanya kazi itakayokuwa na thamani halisi ya fedha hiyo(value for money).
Akitoa
shukrani kwa viongozi na wadau mbalimbali wa elimu waliochangia katika harambee
hiyo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Busega, Mhe. Vumi Magoti ametoa wito
kwa madiwani kuwahamasisha wananchi kuchangia ujenzi wa vyumba vya madarasa
katika kata zao, ili fedha zilizopatikana ziweze kuwasaidia katika
ukamilishaji.
Pamoja
na kutafuta wadua wa elimu waliochangia zaidi ya shilingi milioni 70 katika
harambee hiyo Mbunge wa Jimbo la Busega, Mhe. Dkt. Raphael Chegeni amesema kwa
kushirikiana na wadau ameshatoa vifaa vya ujenzi ikiwemo mabati 1700 na mifuko
ya saruji 640 ambavyo vimeshasambazwa na kusaidia katika ujenzi wa vyumba vya
madarasa wilayani humo.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment